Maalim Seif kutumbua nyongo kesho

Maalim Seif kutumbua nyongo kesho

Basi tuiombee sana Zanzabar ili isiingie kwenye machafuko.

Uhai wa watu ni wa muhimu sana kuliko hata siasa.
 
Baada ya mwezi hizi hekaya zitaisha kama ilivyotokea huku bara na hazitakaa zibadilishe kitu.
 
Anajisumbua huyo bora akae andelee kuishi na familia yake kwa amani maana hata umri nao umeenda.
 
Yeye kila mwezi akaunti inasoma some millions kama pension awaonee huruma walala hoi wakatafute PESA ya kupika japo urojo, kila siku porojo kazi watafanya lini ?Watanzania tujifunze kuwapuuza wanasiasa wanao cheza na saikolojia zetu, ikiwemo kutupotezea muda.

Kikinuka zenji Malimu atapaa na ndege kwenda Uarabuni au abapoza Dar huku watumbatu na Wapemba wakitoana makoromeo
 
Safari hii atazungumza toka Serena au Kempisky?
 
Wakuu msichoke , haya mambo ya Zanzibar kiukweli hayajaisha , ndio kwanza yanaanza .

Taarifa mpya zilizonakiliwa kwenye gazeti la Mwananchi zinaeleza kwamba Shujaa Maalim Seif atazungumza na dunia kesho tarehe 10 / 4 ambapo atapata nafasi ya kuweka wazi mustakabali wake kisiasa .

Mwamba huyo wa siasa za nchi hii ambaye sasa dunia nzima inamtambua na kumkubali ataelezea mikakati , mipango na mwelekeo wa chama chake cha CUF katika siasa za Zanzibar .

Kila la heri Maalim Mungu akulinde .

====================

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.

CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.

“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.

“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Chanzo: Mwananchi.
It is too late,the train has already gained momentum and he is out of the platform.
Ningepata nafasi ya kumshauri ningemshauri kwamba kucheza na wajukuu nyumbani is better than kutumbua nyongo.
 
Hana impact yoyote huyo mgombea wa kudumu wa nationalist party aka cuf.
 
ANATAKA KULAGHAI UMMA KUWAMBIA KUWA ATAGOMBANIA TENA 2020 NA KWA SASA AMEKUBALI MATOKEO. DUH kumbe yote yale yalikuwa nguvu za soda na kuwafanya CUF mabwege
 
Hivi CUF bado ipo? Ataongea kama Katibu Mkuu wa CUF ama Katibu Mwenza wa UKAWA?
Unavyopangilia hoja ni kitu kingine na maudhui ya hoja zako. Kalaga Baho na ufurahi maana CUF haipo, sasa anayezungumzia CUF anazungumzia CUF ipi kama haipo?
 
UKAWA imekuwa ukiwa. Ndo maana wanabaki na moja tu la kutoa matamko
Hoja za wasio na udhu shombo tupu. Kama UKIWA unakuhusu nini? Kuna mtu anatoa matamko, maigizo na maagizo kama mtumbua majipu wenu?
 
Unavyopangilia hoja ni kitu kingine na maudhui ya hoja zako. Kalaga Baho na ufurahi maana CUF haipo, sasa anayezungumzia CUF anazungumzia CUF ipi kama haipo?
Mkuu hivi Mwenyekiti wa CUF ni nani? Nauliza tu nifahamu
 
Ni vizuri humjui maana hujui na hutajua kwa sababu hutaki kujua. Mwenyekiti wa CCM anajulikana ni malaika na atamwachia malaika mwingine mwezi wa sita.

Hawa wenyeviti wa CCM wana kazi moja tu nayo ni kuizika CUF kwa nguvu za dola. Lakini wanasahau wanashindani na hiari ya mioyo ya wapiga kura. HAZIKWI MTU ANAYEPENDWA TOKA MIYONI. DOLA ZINAPALILIA KUATAMIA VYANGU VYAKO NA VYAKO VYAKO SI VYANGU
 
Wakuu msichoke , haya mambo ya Zanzibar kiukweli hayajaisha , ndio kwanza yanaanza .

Taarifa mpya zilizonakiliwa kwenye gazeti la Mwananchi zinaeleza kwamba Shujaa Maalim Seif atazungumza na dunia kesho tarehe 10 / 4 ambapo atapata nafasi ya kuweka wazi mustakabali wake kisiasa .

Mwamba huyo wa siasa za nchi hii ambaye sasa dunia nzima inamtambua na kumkubali ataelezea mikakati , mipango na mwelekeo wa chama chake cha CUF katika siasa za Zanzibar .

Kila la heri Maalim Mungu akulinde .

====================

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.

CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.

“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.

“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Chanzo: Mwananchi.
Binafsi Napata shida kujuwa aina ya nyongo atatema maana kila upande wamezungukwa, kwangu kama mtanzania ni bora angeachana na siasa total maana hana pakupita huo ndio ukweli. Hakuna dunian double agent alie wahi kushinda vita ya moyo wake ni lazima afike mahali anyooshe mikono na kushindwa, siri ya zenj ni kubwa na kila anaye ijuwa mara nyingi harudi kusimulia ameona nini. MAALIM SEMA SIASA BASI MAANA TANGU UMEANZA KUULA MFUPA HUU MAGEGO YAONGEZEKA NA MFUPA HAUJA UVUNJA HATA KIPANDE...... MFUPA ULIO MSHINDA FISI WEWE HUUWEZI
 
Back
Top Bottom