Maalim Seif kutumbua nyongo kesho

Maalim Seif kutumbua nyongo kesho

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,611
Reaction score
272,362
Wakuu msichoke , haya mambo ya Zanzibar kiukweli hayajaisha , ndio kwanza yanaanza .

Taarifa mpya zilizonakiliwa kwenye gazeti la Mwananchi zinaeleza kwamba Shujaa Maalim Seif atazungumza na dunia kesho tarehe 10 / 4 ambapo atapata nafasi ya kuweka wazi mustakabali wake kisiasa .

Mwamba huyo wa siasa za nchi hii ambaye sasa dunia nzima inamtambua na kumkubali ataelezea mikakati , mipango na mwelekeo wa chama chake cha CUF katika siasa za Zanzibar .

Kila la heri Maalim Mungu akulinde .

====================

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.

CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.

“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.

“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Chanzo: Mwananchi.
 
Wakuu msichoke , haya mambo ya Zanzibar kiukweli hayajaisha , ndio kwanza yanaanza .

Taarifa mpya zilizonakiliwa kwenye gazeti la Mwananchi zinaeleza kwamba Shujaa Maalim Seif atazungumza na dunia kesho tarehe 10 / 4 ambapo atapata nafasi ya kuweka wazi mustakabali wake kisiasa .

Mwamba huyo wa siasa za nchi hii ambaye sasa dunia nzima inamtambua na kumkubali ataelezea mikakati , mipango na mwelekeo wa chama chake cha CUF katika siasa za Zanzibar .

Kila la heri Maalim Mungu akulinde .
Hivi CUF bado ipo? Ataongea kama Katibu Mkuu wa CUF ama Katibu Mwenza wa UKAWA?
 
Atutajie tu hatua za kuchukua,hatutaki figisufigisu
 
Si juzi tu walitoa maazimio? Au wameyafanyia amendment?
kesho sasa anakuja mzee mwenyewe Maalim Seif ambaye utafiti unaonyesha kwamba anakubalika kwa 95% na wazanzibar , usikose tukio hili la kihistoria tangu kuumbwa kwa nchi hii .
 
Ataongea na dunia? Dunia inamjua?? Kwa cheo gani alichonacho hasa...huyu mtu kaifanyia nini dunia sorry Zanzibar mpaka ajulikane kiivyo?
Tusiende na upepo huyu mtu ni king'ang'anizi asiye na lolote jipya lakustua mtu. Hatutaki u extremist wala kuiarabisha Zenji. Mabadiliko ni jambo zuri lakini yanatakiwa yawe mabadiliko chanya.
 
kesho sasa anakuja mzee mwenyewe Maalim Seif ambaye utafiti unaonyesha kwamba anakubalika kwa 95% na wazanzibar , usikose tukio hili la kihistoria tangu kuumbwa kwa nchi hii .
Mkuu nasubiria kwa hamu tamko lake mzee wa KAMAHURU
 
Hahahahahaaaaaa. Kwani yale waliyoongea hivi majuzi hayajaeleweka? Au kwa vile Dunia imewapuuza?
utajua tu hiyo kesho ikifika , nchi ambayo matundu ya vyoo vya shule yanajengwa na wazungu , kupuuza hela za MCC ni kujitafutia matatizo makubwa sana .
 
Ataongea na dunia? Dunia inamjua?? Kwa cheo gani alichonacho hasa...huyu mtu kaifanyia nini dunia sorry Zanzibar mpaka ajulikane kiivyo?
Tusiende na upepo huyu mtu ni king'ang'anizi asiye na lolote jipya lakustua mtu. Hatutaki u extremist wala kuiarabisha Zenji. Mabadiliko ni jambo zuri lakini yanatakiwa yawe mabadiliko chanya.
Huu ndio ukweli mchungu ambao UKAWA hawataki kuusikia
 
Hahahahahaaaaa. Huku sasa ni kuchanganyikiwa
utajua tu hiyo kesho ikifika , nchi ambayo matundu ya vyoo vya shule yanajengwa na wazungu , kupuuza hela za MCC ni kujitafutia matatizo makubwa sana .
 
utajua tu hiyo kesho ikifika , nchi ambayo matundu ya vyoo vya shule yanajengwa na wazungu , kupuuza hela za MCC ni kujitafutia matatizo makubwa sana .
Naona umekasirika sana, punguza jaziba Maalimu Seif ndio basi tena, alidhani atakuwepo kwenye cabinet,
 
Back
Top Bottom