Maalim Seif & Hussein Ali Mwinyi

Maalim Seif & Hussein Ali Mwinyi

GeoMex

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
5,430
Reaction score
20,063
Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.(Zaburi 133:1)
Screenshot_20210101-184818.jpg
 
Zaburi na hao maustaadh vipi tena?
Huo mstari hauna ubaya wowote kwa maustadh, ndugu wakae pamoja kweli, mstari haujadanganya kabisa.

Japokuwa damu imemwagika, tofauti na serikali za awamu zilizopita, awamu hii imeonesha nia ya dhati kutaka kuwaunganisha Wazanzibar wawe kitu kimoja katika kujenga taifa lao na kuacha kutumia siasa kuwagawa. Mfano wakati wa awamu iliopita, ilijaa vijembe na kueneza chuki na ubaguzi. Walau hivi sasa tunaona kuwa Rais anataka tuheshimiane regardless of which party you support. Na ameonesha kwa dhati kabisa na hamu ya kutaka kushirikiana na Wapinzani katika kusonga mbele. Akina sheni walishukuru Maalim kususia uchaguzi ili wajifarague.
 
Ccm huwajui vizuri wewe, subiri ufike uchaguzi hao act watashangazwa nakwambia, na baada ya uchaguzi ccm watataka wakae pamoja tena
 
Haiwezi kupendeza hata siku moja

Iwapo wao wanafaidika kwa gharama za walala hoi, maskini waliokiona chamtemakuni.

Halafu wao kwenye mapicha, majumba ya kifahari ulinzi na kula vinono

Sio sawa na udhalili wa hali ya juu kwa waliohujumiwa haki zao za msingi kikatiba.
 
Mbona umeandika za watu sasa?

~Infinity
Unajua kusoma mkuu??

Nimekwambia dini zetu hazikuandikwa sasa ntaquote kifungu kutoka hewani mkuu??

Ndo maana nimetumia za watu mkuu
 
Hawa jamaa naona kama wote wanajua jinsi ya kuitoa Zanzibar kwenye umaskini kunuka.
 
Maridhiano ni kitu kizuri sana,mfano uhuru kinyata asingeweka maridhiano na raila,,watu wangeumia sana,,wapinzani nao ni watu kama sisi buku 7..
 
Ccm huwajui vizuri wewe, subiri ufike uchaguzi hao act watashangazwa nakwambia, na baada ya uchaguzi ccm watataka wakae pamoja tena
Hahaha Ccm ninachowakubali hawaachi kiti cha urais hata kwa dawa,halafu uchaguzi ukiisha wanakuja na ngonjera za tusameheane muda huo tayari wako ikulu.

Hio ndio CCM ninayoijua mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Maalim astaafu vizuri kwa ving'ora,maisha yanataka nini tena
 
a9e2d76efb217f77c9631a4185543045.jpg

Ndugu waliwahi kuwa pamoja ila baadae ikawa hivi
585a3105fa566f9c1491c4d0d6711203.jpg
 
Back
Top Bottom