Maalim Seif Hamad kwanini asipewe tuzo ya amani?

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
Mwaka 1988 Maalim Seif alifukuzwa CCM kutokana na mgogoro ndani ya chama.
  • Kwa kipindi cha miaka 26 Maalim Seif Hamadi amepambana bila kuchoka, amechochea mageuzi makubwa ndani ya Tanzania.
  • Maalim amepambana na vigogo wakubwa kwenye chaguzi za kisiasa tangu mwaka 1995 na kuwatoa jasho kweli kweli (Salmin Amour), mwaka 2000 na 2005 (Amani Karume, mtoto wa rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume), mwaka 2010 na 2015 (Dk. Ali Mohammed Shein).
  • Amesababisha ushawishi wa chama cha ACT-Wazalendo kupanuka na kukua bara na Visiwani.
  • Mafanikio makubwa ni matokeo ya jitihada zake katika siasa ni pamoja na kuleta umoja wa kitaifa, mpaka kufanikiwa kubairishwa kwa katiba ya Zanzibar kuwa na nafasi za makamu wawili wa rais wa Zanzibar.
 
Zitto na Maalim usiwaamini hata dak moja ni matapeli wa kisiasa
Wale sio matapeli na ndiomaana hawaja shtakiwa.
Mimi huwa nawaita wafanya biashara ya siasa, yaani siasa ndio kazi yao na inawalipa. Hivyo ukiona wanahamasisha wanachama, basi faham kwamba hapo ndipo wanapo tengenezea kula yao pamoja na familia zao...
 
Sidhani kama anastahili, apate tuzo kwa kushirikiana na waliomwibia kura, je, hao wezi wamemwahidi hamwibii tena? Mnatengeneza tatizo mnataka pongezi kulitatua, crazy!
 
Wanatia aibu sn asee
 
Yani watu hawataki kumwacha huyu mzee apumue tangia alipo tangazwa tu .. yan daah😁😁😂
 
Sidhani kama anastahili, apate tuzo kwa kushirikiana na waliomwibia kura, je, hao wezi wamemwahidi hamwibii tena? Mnatengeneza tatizo mnataka pongezi kulitatua, crazy!
km huwezi kuwashinda ungana nao, umri umeenda acha apumzike. km ni mapamambano amejitahidi, maana nasikia kuna nadhalia kuwa ameshawahi kushinda urais.
 
Sidhani kama anastahili, apate tuzo kwa kushirikiana na waliomwibia kura, je, hao wezi wamemwahidi hamwibii tena? Mnatengeneza tatizo mnataka pongezi kulitatua, crazy!
Kasaidia sana mageuzi ya kisiasa, kapambana jamani sasa wengine wachukue kijiti wajaribu. kwa umri wake stress siyo salama tena.
 
Naunga mkono hoja, ila sio pekee yake, hata Dr. Mwinyi anastahili hiyo tuzo!
P
Dr Mwinyi ni mapema sana, ngoja tumpe muda kwanza tuone matokeo ya hii mipango anayofanya. Maalim miaka 28 siyo mchezo, kachangia kuleta mageuzi ya kisiasa lkn pia maridhiano katka jamii ya watanzania hasa wa Zanzibar. amewafundisha wana siasa siyo ugomvi ni siyo harakati.
 
Magufuli ndiye anastahili tuzo ya amani. Amejenga utulivu na amani nchi hii haijapata kutokea. Kila mtu anaunga mkono jitihada zake. Kila mtanzania wakati huu anafurahia nchi yake kuliko wakati mwingine wowote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom