Maalim Seif: CHADEMA waroho wa madaraka

Mzee wa uliberali anadhani Elerai ni Zenji?Asubiri June 16, 2013 ataisikilizia kwenye bomba chadema itakavyowaunguza cuf na wenza wao,ccm.
 
Mleta thread,Maalim angetaja fujo 3 zilizofanywa na CHADEMA bungeni na aweke sababu za fujo hizo ili tupime.
 
Hivi kuna mroho wa madaraka kama Maalimu Seif?

Hamad Rashid alipoonesha kugombea ukatibu wmkuu wa CUF Maalim Seif akamuundia zengwe na kumfukuza uanachama kabla ya kurudishiwa na Mahakama.

Maalim Seif na Lipumba WAMEJIFANYA wagombea wa kudumu wa U-Rais wa SMZ na JMT respectively tangu mfumo wa vyama vingi uanze 1995.

CDM chama makini kilishawahi kuwaunga MKONO CUF kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 kwenye nafasi za URAIS wa JMT na SMZ. Kama CUF sio WAROHO wa madaraka basi nao waiunge mkono CDM 2015! thubutu yako Maalim.

CUF na CDM walishirikiana bungeni kuunda kambi rasimu ya UPINZANI kwasababu lilikuwa hitaji la kikanuni. CUF ilikuwa haina wabunge wa kutosha kuunda kambi ya UPINZANI peke yao.
 
Tangu walivyotangaza wao ni walibarali, sisiem ikafunganao ndoa ya mkeka wakawa wapole kama wananyolewa. Wakawasaliti wazanzibari mchana kweupe! Hivi sasa anawashambulia CDM kwa vile chama chake kimekosa umaarufu Bara na visiwani.

Hamad Rashid nayeye alikuwa anatamani madaraka ya kuwa kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, alipoukosa pamoja na kusaidiwa na sisiem, akaugeukia u-Seif Sharifu Hamadi (Ukatibu Mkuu wa Kafu) ndipo alipokutana na teke lililo mpeleka ADC!

Hiyo yote ni uroho wa madaraka, sasa hivi maalimu ana kula keki ya Taifa taratibu bila kelele kwani alichokuwa anakitafuta (madaraka) keshayapata!
 

Mkuu usiangaike na huyo mliberali mzoefu
 

Una kumbu kumbu ya Prof Safari & uchaguzi CUF?
 

Hakuna sababu ya kuhangaika kumjibu huyu mliberali; hajui maana ya maneno aliyosema; ni mchecheto kutokana na hali alivyoikuta mbaya kwa mgombea wake, Msaliti John Bayo
 
Shibuda alipotaka kugombea urais kupitia CCM nini kilitokea Sheikh Yahaya alisemaje, acha unafiki pimbi weweCUFtumeshawaunga mkono mara ngapi? tulichotofautiana naCUF nikuigamakubaliano na CCM ya kumuunga mkono Kikwete kwa kuwa ni mwislamu na Lipumba ni mwislamu mwenzake wakaacha utaifa wakatanguliza dini zao sasa ulitaka tuendelee kushirikiana kwa lipi watu wameshajiweka wazi au hata video hujaziona na uliwekewa humu JF kama hujalizika na hizo muombe bi kiroboto maana alishapewa na Lema.
 
Kuna ukweli ndani yake ukiwa neutral! Ila ukiwa CHADEMA ni ukweli mchungu.
CUF wanajiitaje wapinzani wakati wanaongoza Serikali ya Zanzibar pamoja na CCM?Ukiwa muelewa ukweli si mchungu.
 
Adui yako ni Mw. JK Nyerere? unataka wamseme Marehemu, hivi usivyo na akili hata ya kupengea kamasi unaweza kufananisha CCM ya Nyerere na uozo wa CCM ya sasa iliyojaa ufisadi ubinafsi wa kupindukia..Nyerere sisemi kuwa hakuwa na mapungufu lakini ukimlinganisha na nani hapa Tanzania
 
Seif akae kimya!watapewaje nafasi ya kambi ya Upinzani Bungeni wakati wameungana na CCM bungeni na Serikalini?Maalim anahoji uroho wa madaraka?...mbona yeye amehongwa umakamu wa Rais usio na nguvu sie tupo kimya?kawa kama Ceremonial,hana nguvu wala madaraka..raha yake kula marupurupu..amewauza CUF ktk ndoa ya CCM...Yupo kama Joka la Kibisa..haling'ati wala kutema mate..unaweza kuliweka hata ndani ya suruali na lising'ate...kama unataka ujue tabia ya Joka la kibisa,basi Ijumaa nenda Break Point pale Posta uone WANNE STAR anavocheza na joka na kisha kulifungia ktk box...SEIF umewauza CUF kwa ndoa ya CCM
 
Mleta mada ni gamba anamsaidia promotion mliberali wao kafu a.k.a mwanandoa wa gamba!!!
 
Alisema wakati CUF, ilipofanikiwa kuongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi wa Hammad Rashid Mohamed, kulikuwa na busara za hali ya juu katika uendeshaji wa vikao vyao.

Leo anamtambua Hamad Rashidi!... Mhhh hiki kituko.
 
Mleta mada ni gamba anamsaidia promotion mliberali wao kafu a.k.a mwanandoa wa gamba!!!

Humjui!!... Ni mliberali.. Yuko pamoja na magamba mpaka JK akiondoka madarakani. Akigombea Lowasa anarudi kuendeleza mambo ya mombasa.
 

Hee Zitto ni mwakilishi wa ccm, Cuf, kabila lako au dini yako?
 
Mliberali Maalim Seif hana uhalali uhalali wa kusimama na kuongea mbele ya raiya wenye akili timamu.


NB:

CCM na CUF hapa Arusha mnachezea pesa zenu bure kuhonga.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hana adabu kabisa Seif kwanza ujinga wake huo apeleke huko huko Zanzibar anakosema anataka mamlaka kamili anatafuta nini Arusha,Mgombea wa maisha CUF-Zanzibar huo sio uroho wa madaraka,fujo na matusi ya nguoni wanayotoa wabunge wake wa CUF na wa mumewe CCM hajaona hizo propaganda apeleke kwa mkewe vinginevyo anapoteza muda kutmia fedha za serikali kuja kumnadi mgombea mwizi wa fedha za ujenzi wa clinic ya olimpiki
 
Mume na mke huwa hawapishani matamko,kwa sababu mambo yote huwa wanayapanga wakiwa chumbani,
hakuna jipya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…