Wakati maandalizi ya kupokezana kijiti cha Mwenyekiti wa CCM kutoka kwa JKT kwenda JPM yakizidi kupamba moto huko Dodoma, mwanasiasa machachari na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sherif Hamad amepata mualiko wa kuhudhuria Mkutano ambao umeratibiwa na shirika la National Democratic Institute (NDI) utaofanyika Philadelphia, Pennsylvania, kuanzia Julai 25-28 2016.
Mualiko huo ni kwa hisani ya Shirikisho la Kimataifa la International Leaders Forum.
Maalim Seif anatarajiwa kuwasili Philadephia tarehe 23 Julai huku akitia gia angani akiunganisha ziara yake refu ilioanzia USA, UK na EU na sasa kurejea tena USA
Kuzidi kuendelea kutambuliwa kwa kiongozi huyu na taasisi za kimataifa zinazidi kupaisha joto la tumbo la mahasimu wake wa kisiasa na kuzidi kujenga hoja yake ya kupokonywa ushindi wa uchaguzi wa Oktoba 25 uliotambuliwa na waangalizi wa mataifa na wa ndani kuwa ulikuwa huru na wa haki.