Maalim Seif anena baada ya Jecha Kudai alikuwa sahihi kufuta Uchaguzi ZNZ

WinVista

Senior Member
Nov 11, 2014
134
87
MALIM.jpg

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema ameshamalizana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha na haoni umuhimu wa kuzungumzia wala kumjibu, kwa sababu atampa sifa asizostahili.

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha kituo cha televisheni cha Azam TV juzi, Jecha alisema hakumshirikisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 visiwani humo.

Jecha alifuta matokeo hayo Oktoba 28, 2015, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa uchaguzi wa rais, huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.

Alitangaza uchaguzi mpya Machi 20, 2016 ambao ulisusiwa na CUF na Dk Shein kuibuka mshindi.
 
Huyu Seif kwa kweli ataendelea kupasua vichwa vya watu.
Asipoangaliwa atatusababishia watanzania maisha magumu kutokana na vikwazo vya kiuchumi.
 
Jecha alishasema Yeye Kama Nahodha wa Meli akiwa katikati ya dhoruba baharini hatosubiri Ruhusa wala kupoteza Muda wa kuwasiliana na mwny Chombo badala ya kunusuru Chombo chenyewe!
 
View attachment 463268

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema ameshamalizana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha na haoni umuhimu wa kuzungumzia wala kumjibu, kwa sababu atampa sifa asizostahili.

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha kituo cha televisheni cha Azam TV juzi, Jecha alisema hakumshirikisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 visiwani humo.

Jecha alifuta matokeo hayo Oktoba 28, 2015, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa uchaguzi wa rais, huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.

Alitangaza uchaguzi mpya Machi 20, 2016 ambao ulisusiwa na CUF na Dk Shein kuibuka mshindi.

cc @
Pohamba

TUNDU LISU AMEMALIZA KILA KITU HAPA

Jecha anatumika!! Siku atasema ya moyoni subiri ni suala la muda tu! Sio mbali sana kitambo kidogo tu
 
Huyu Seif kwa kweli ataendelea kupasua vichwa vya watu.
Asipoangaliwa atatusababishia watanzania maisha magumu kutokana na vikwazo vya kiuchumi.
Umeongea point sana,angalia hata nchi zinazokuja bongo Lusaka urafiki,huko Zanzibar ni kama wametengwa hawana nchi ndugu wala rafiki,zaidi ya Magufuli ambaye naye so mtu was kumtilia maanani sana
 
Back
Top Bottom