Maalim Seif amuinua Lowassa Z’bar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225

Wananchi wa Zanzibar waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Urais wa chama cha CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad katika uwanja wa Kibandamaiti mjini Zanzibar​

Posted by: Jabir Idrissa 23 hours ag


KAMPENI ya Maalim Seif Shariff Hamad ya kushika madaraka ya Zanzibar imeanza kwa nguvu kwa kupata ugeni mzito wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano, Edward Lowassa na mgombea mwenza wake, Juma Duni Haji. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).

Maalim Seif, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye katika serikali inayomaliza muda mwezi ujao ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais, alizindua kampeni yake jioni hii kwenye uwanja wa Kibandamaiti, mjini Zanzibar.


Mkutano huo, ulishuhudiwa na Lowassa, kada aliyehama CCM mwezi uliopita, na kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuteuliwa kuwania urais kwa mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).Lowassa alitumia dakika chache kuwahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa wapige kura kwa amani na utulivu na “hakuna atakayeziiba kura zao.”“Hawawezi kutuibia, msiogope kitu… tuna uwezo wa kulinda kura zetu. Huo uwezo tunao, au mnadhani hatuna,” amesema na kuambiwa “tunao.” Alijibu vilio vya hofu ya kutokea wizi wa kura kama ambavyo Zanzibar imekuwa ikishuhudiwa kila uchaguzi.Lowassa ametoa wasiwasi umma na vitisho kuwa chama cha upinzani kikishinda, kutakuwa na vurugu, akisema hakutakuwa na vurugu yoyote. “Vurugu zitoke wapi, kwani hapa kuna vurugu iko wapi na tumekutana hapa kwa wingi,” amesema Lowassa huku wananchi wakimshangilia.Ameahidi kuwa baada ya ushindi katika uchaguzi wa Oktoba 25, ataomba sehemu ya sherehe ifanyike mjini Zanzibar, kwa kuwa pia “itakuwa ni sherehe kwa ushindi wa Maalim Seif.” Aliomba wananchi wampigie kura nyingi yeye pamoja na Maalima Seif ili waunde serikali makini pande zote mbili.Lowassa amelaumu kitendo cha wapinzani wake kuchukua mabango ya picha zake na kuyaharibu. “Wanachukua mabango yetu wameyaangusha. Tumewaambia tutafanya kampeni za kistaarabu lakini angalia wanavyofanya,” amesema.Akihutubia umma uliohudhuria mkutano huo baada ya uteuzi wa wagombea urais kufanywa jana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Maalim Seif alisema akishika madaraka, atawarudisha masheikh Zanzibar.“Nikiwa rais masheikh wetu watarudi Zanzibar, kama wana makosa watashitakiwa katika mahakama zetu ambazo ziko sawa na Mahakama ya Tanzania Bara,” amesema.Awali alisema inashangaza kuambiwa Zannzibar ina rais, ina Baraza la Wawakilishi na ina Mahkama, ambayo mamlaka yake sawa na mahkama ya Bara, lakini “waliamua masheikh wetu kuwapeleka Bara, nasema watarudi haraka mara tu nikiwa rais.”Maalim Seif ambaye anagombea mara ya tano ndani ya malalamiko ya kuporwa ushindi wake, amesema amejiandaa kuibadilisha Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika Mashariki kwa kiwango cha maendeleo.


  • Nia yangu ipo palepale ya kuibadilisha Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika Mashariki kwa maendeleo makubwa. Tutaijenga Bandari ya Zanzibar kwa vitendo sio maneno, tutafungua uwanja wetu mpya wa ndege na kuhakikisha unakuwa na eneo la mizigo mikubwa ili Burundi, Rwanda, Zambia waje kununua bidhaa hapa.
  • Tutaungua Benki ya Uwekezaji ya Zanzibar ya kutoa mikopo kwa wanawake na vijana wenye shida ya mitaji ya kufanyia biashara zikiwemo za Jua Kali.


Maalim Seif amesema serikali atakayoongoza itakuwa na utii kwa utawala wa sheria na haki za binadamu na kamwe haitaruhusu watu kudhalilishwa na askari wa vikosi kama inavyofanyika askari wanaojifunika nyuso na kutesa wananchi.


 

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
4,582
2,000
Walijitahidi kujenga hoja na kushusha munkari munkari huwapa ccm na polisi nafasi
 

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
14,949
2,000
Akishinda Maalim tumeshinda sote , halikadhilika ushindi wa Lowassa ushindi wetu tanganyika na zanzibar.
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,133
2,000
Ila kiukweli Zanzibar ilipaswa iwe mbali sana kimaendeleo kuizidi hata Tanzania bara...

Sijui ni nini kimeikumba...
 

Johne

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
328
170
CCM irudi kuzim kwanza kenda ku-update majini yake yaendane na mfumo wa digital
 

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
1,956
2,000
Ila kiukweli Zanzibar ilipaswa iwe mbali sana kimaendeleo kuizidi hata Tanzania bara...

Sijui ni nini kimeikumba...
Hakuna asiyejua kwamba maendeleo ya Zanzibar yanadunishwa na serikali ya muungano kwa kudhibiti mapato na misaada yake inayopokea toka nje.
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
6,069
2,000
Mzee wa "sawa sawa".Wazanzibari msifanye makosa ya kuirudisha ccm,mabadiliko yata wabadili kuondokana na hali inayowakabili
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,652
2,000
Hakuna asiyejua kwamba maendeleo ya Zanzibar yanadunishwa na serikali ya muungano kwa kudhibiti mapato na misaada yake inayopokea toka nje.
Ya ukweli haya? Je umeshafikiria soko la Zanzibar litakuw lipi kama muungano haupo? Hata hao aliowasema Maalimu kuyoka Congo, Burundi n.k. hawafiki huko pasipo kupita Tanganyika!
 

Kobe

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
1,792
2,000
Ya ukweli haya? Je umeshafikiria soko la Zanzibar litakuw lipi kama muungano haupo? Hata hao aliowasema Maalimu kuyoka Congo, Burundi n.k. hawafiki huko pasipo kupita Tanganyika!

Labda kama umepata ufahamu kipindi cha uongozi wa mkwere, tunaojua vizuri kuhusu biashara haswa bidhaa kupitia bandari ya Zanzibar tumeshaelewa maana yake.
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,652
2,000
Labda kama umepata ufahamu kipindi cha uongozi wa mkwere, tunaojua vizuri kuhusu biashara haswa bidhaa kupitia bandari ya Zanzibar tumeshaelewa maana yake.
Kama umeelewa unawamegea na wengine ili nao waelimike
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom