Maajabu ya ziwa Natron

Maajabu ya ziwa Natron

Aisee kama Ziwa Natron nalo lipo mnadani sijui tunaelekea wapi watz
 
Ziwa Natron, lililoko kaskazini mwa Tanzania, ni mojawapo ya mazingira magumu zaidi duniani. Maji yake yana pH ya juu hadi 10.5 na yanaweza kufikia joto zaidi ya 60 ° C. Ukali wa ziwa hilo unatokana na kabonati ya sodiamu na madini mengine, ambayo hupenya kutoka kwa miamba ya volkeno inayozunguka.

Wakati ndege au wanyama wanapokufa katika ziwa, madini hukausha miili yao, na kuwahifadhi katika hali ya mawe. Mpiga picha Nick Brandt alinasa picha za kuogofya za viumbe hawa walionyamazishwa.

View attachment 3352619Ni bustani ya asili ya sanamu, nzuri na ya kutisha - inayoonyesha jinsi mazingira ya hali ya juu yanaweza kutoa matokeo ya ajabu na yasiyotarajiwa
Mshana Jr, huwa nahusudu maandiko yako lakini hili andiko lako naona kama umepigwa!
Nimepita mara nyingi pale Ziwa Natron kuelekea Waso (Loliondo) lakini hiki ulicholeta hapa si sahihi.
Ni kweli yapo magadi ya kutosha yanayotiririka toka Mlima wa Mungu (Oldonyo Lengai) ulio jirani na Ziwa Natron lakini haya uliyoleta hapa si sahihi kabisa.
 
Halina samaki?
Wapo pale samaki wachache wanoweza kustahimili viwango vikubwa vya maji chumvi.
Pia wapo Flamingo wa kutosha hasa kutegemea na msimu.
Pia kuja joto kali sana hadi kufikia 41 C. Mazingira ya eneo lile kwa kweli ni magumu sana lakini hata hivyo utawaona vijana wa Kimasaai wakichunga makundi ya mbuzi na pale waonapo gari likipita husimama katikati ya barabara na kuomba maji ya chupa.

Katikati na Mlima Odonyo Lengai na Ziwa Natron kuna kijiji kinaitwa Ngare Sero; Kutokana na joto kali sana la eneo lile, kama upo safarini ni lazima usimame pale kidogo angalau upate pause - utapata . maji baridi na nyama choma (mbuzi) kisha uendelee na safari kuelekea Mto wa Mbu kupitia Engaruka (historical Site) au Longido (kama unaelekea Arusha).
 
Back
Top Bottom