Wakuu,
Mimi huwa nashangazwa sana na wauza kahawa wa Tanzania .Huwa wanaweka kahawa kwenye birika la aluminium halafu chini wanaweka mkaa ili kahawa isipoe, sasa ninachojiuliza ni kwa nini wasitumie "Thermoses " ili kuepuka kutembea na mkaa? Au mkaa unasaidia kuifanya kahawa kukolea zaidi?