Maajabu ya wauza kahawa

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,188
7,490
Wakuu,

Mimi huwa nashangazwa sana na wauza kahawa wa Tanzania .Huwa wanaweka kahawa kwenye birika la aluminium halafu chini wanaweka mkaa ili kahawa isipoe, sasa ninachojiuliza ni kwa nini wasitumie "Thermoses " ili kuepuka kutembea na mkaa? Au mkaa unasaidia kuifanya kahawa kukolea zaidi?
 
Birika na jiko la mkaa linalobebeka lina kazi mbili
1.kutunza joto kwa kahawa
2.kuendeleza uzalishaji wa kinywaji kahawa kadiri inavyohitajika.

Ukitia kahawa kwenye thermos hupati wateja.
Ni sawa na kumuuzia mtu kahawa kwenye kikombe cha chai (tea mug)

Kahawa ni zaidi ya kinywaji ndani yake kuna utamaduni na staha za pwani.
Huwezi kunywa kahawa ukiwa na haraka na papara.
Mara nyingi vijiwe vya kahawa vilitumika kama "meeting points" kwa watu wengi hasa mitaa ya Msimbazi na Uhuru , kumbuka wakati huo magari yote yalikuwa yanaishia Kkoo,hakukuwa na hizi route ndefu i.e Ubungo Mbagala, gmboto makumbusho.....Kariakoo ndio ilikuwa mahali pa kubadilishia na kuunganisha magari.
Huwezi kunywa kahawa huku umekaa kwenye kiti cha plastic lazima iwe bench la mbao.
Pia kikombe cha kahawa na kashata ina ushikaji wake. Haushiki kama unashika andazi.
Hata hizo kashata zilikuwa na ukataji wake sio siku hizi wanakata vyovyote tu.
Kwa wale wanaofahamu vijiwe maarufu vya kahawa pale "round about " ya mtaa wa Uhuru na Msimbazi wataelewa. Kwenye kijiwe cha kahawa watu huwa hawabishani bali wanajadiliana wakitumia lugha ya staha na kuzungumza Kiswahili fasaha.Hii ilifanya kuvuta wasikilizaji wengi maana hata kama watu wanajadili dini kamwe hakutokei ugomvi.
Hata unywaji wa kahawa una taratibu zake haunywi kama unakunywa chai.

Kwa wale waliokuja mjini siku nyingi wataelewa
 
Wakuu,

Mimi huwa nashangazwa sana na wauza kahawa wa Tanzania .Huwa wanaweka kahawa kwenye birika la aluminium halafu chini wanaweka mkaa ili kahawa isipoe, sasa ninachojiuliza ni kwa nini wasitumie "Thermoses " ili kuepuka kutembea na mkaa? Au mkaa unasaidia kuifanya kahawa kukolea zaidi?

Wanapokuwa wanatembea wanakuwa na kahawa waliyoisaga kwenye mifuko yao, ile iliyokuwa kwenye Birika ikiisha basi anajaza maji tena na kuweka kahawa mpya, anaweza kuuza hata lita 50 kwa siku
 
Birika...kwanza mimi toka nakuwa namuona babu yangu anatumia birika yeye chupa atakuambia zinamagonjwa sana bora utumie birika
 
Jamani naomba kuwaulizen hawa wanaume dar huwa wakoje mana akitokea mtu mmoja na panga wao hungia ndani ni kwamba hawana nguvu
 
Sometime uwa wanaongeza maji kahawa ivyo moto ulee uifanya iendelee kuchemka vema.
 
Back
Top Bottom