Maajabu ya wauza kahawa

Hii ni kali nimecheka balaa ... Kutembea na mkaa bongo yetu raha tupu hakuna cha thermos hapo mkuu kahawa mvuke bwana..!
 
Ila na wao wanatakiwa kukata leseni kwani wanatembea na vyombo vya moto,Ivi jamani hapa Dar hakuna chama cha wauza kahawa kweli ama
 
2017 Tanzania kumbe wenye ubongo wa size ya memory card ya 225mb bado mpo? Hilo swali nenda kawaulize watoto wa primary kati ya watoto kumi sita au saba watakupa majibu sahihi kabisa. Amini hivyo
 
Achana na habari za kahawa, mwambieni ndugu yenu aeke vyet
 
Mkuu umenifurahisha sana! Unajua kuna vitu vingine ukifikiria unaweza ukacheka including that! Umetufurahisha sana
 
Mkuu kwanza ningependa ufahamu Kua kahawa INA nguzo 5
1)Iwe ya moto
2)iwe changu
3)inywewe ktk kikombe chake maalum
4)iwe na takadumu.takadumu maana yake unakunywa kahawa na kashata au tende au halua au matunda
5)maneno ya kwenye genge la kahawa yaache papo hapo endapo umeshamaliza kunywa kahawa na ukaondoka
 
ikipungua wanaongeza maji wenzio, hivyo kwenye thermos itaendelea kupoa pia kwa pilika zao lazima zitapasuka aisee

 
Mkuu lile birika huwa wanaongeza maji njiani wanaendelea na safari yani kwa siku anaweza uza kahawa hata lita 30 sasa ukiwa na thermosi huwezi
Lita 30 huwa anabeba ndoo ya maji au
 
Birika ni kama tangazo au sign kuwa ni muuza kahawa kwahyo mtu akiona lile birika tu anamuita
 
acha imani potofu sio kila anaejua kusoma alienda shule, unapokosea ni lazima uambiwe ni kwa faida yako stay safe
Kwetu ni Kolomije Mimi na Daudi Bashite tumesoma shule moja nivumilie mkuu
 
hapo kwenye red bila shaka ulitaka kuandika chungu,
 
Acha kua na mawazo ya kijinga,unaporekebishwa kubali kistaarabu,hiyo ni kwa faida yako pia.
Mkuu nishamjibu sisi watu wa Kolomije Walimu walikuwa wachache.Mimi na Daudi Bashite tumesoma na kukaa dawati moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…