Maajabu ya serikali ya tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maajabu ya serikali ya tanzania.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wikiliki, Jan 19, 2011.

 1. Wikiliki

  Wikiliki JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 529
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana Jf wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania uliopita vyuo vikuu vilichelewa kufunguliwa kisa fedha ya kuwalipa wanafunzi hakuna eti hivyo wakasogeza mbele ili wapate fedha cha kushangaza hata baada ya kusogeza mbele muda na kuwanyima wanafunzi haki yao ya kupiga kura hadi leo hii migomo ya wanafunzi kila kona kisa hakuna fedha. Je kulikuwa na ulazima wa kusogeza muda wa kufungua vyuo.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mkuu, hii migomo ingetokea kipindi cha uchaguzi nini kingetokea..CCM waliliona hilo ndiyo maana walikataa
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama pesa ya kuwalipa wanafunzi imekosekana, sasa zile ahadi zetu sijui zilifika ngapi vile, nadhani 100 + zitatekelezeka?
  Mie binafsi nilikuwa na matarajio makubwa sana na ahadi mbili tu; 1.Ujenzi wa barabara ya musoma - arusha ili niwe napanda basi la zakaria express pale ubungo ninapokwenda nyumbani na 2.Ununuzi wa meli ziwa victoria ili niweze kusafiri kwa uhakika ninapokwenda kuwasalimia wajukuu zangu kule Kamachumu!!
  Sasa kwa hali kama hii na kuna tetesi kwamba mishahara ya mwezi ujao kwa watumishi wa serikali iko hatihati sijui itakuwaje.
   
 4. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe wanafunzi kurudishwa nyumbani kambla ya uchaguzi 2010 kujificha jambo???
   
 5. CPU

  CPU JF Gold Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kipato cha Siri kali kimeshuka kaka, tangu CHADEMA wanyakue majimbo na halmashauri kadhaa nchi nzima kipato kinahama. Ona sasa posho tu za Makatibu wa SISIEMU zinawapiga chenga, Makamba-le anaulizwa KULIKONI anaanza kumwaga matusi ya kambale. Sasa wanataka kufidia kwa kupandisha bei za huduma za jamii kama maji, umeme, vyakula, nauli n.k. ili kodi iwe kubwa
   
 6. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuondoe huu mzigo wa misumari ya moto mgongoni.

  CCM tukailaze mahala pabaya jehanam kwa haraka sana kabla hatujatumbukia sote kwa pamoja shimoni.
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu huo mzigo wa misumari mgongoni mwetu umegandishwa kwa Super Glue ya Kijerumani miaka 50 sasa. Na mbaya zaidi kuna washikaji (vyombo vya dola) vinaulinda huo mzigo usishuke. Sasa option iliyobaki ni kukata sehemu ya mgongo ili itoke na mzigo (kumwaga damu) ndo pengine tunaweza kuwa huru. Sio mapenzi yetu kukata nyama ya mgongo lakin sioni option mbadala
   
Loading...