Maajabu ya Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma

Maajabu ya Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,781
Mkuu wa Mkoa wa Dodma mama Rehema Nchimbi amewaomba waendesha vymbo vya moto vya aina zote mjini Dodma kuwa wakarimu, wapole na wenye utu katika kipindi cha siku 3 za mkutano wa ccm mjini hapo...!

Binafsi nimemwona wa ajabu kwasababu yeye kama Mtumishi wa serikali ni wajibu wake kusisitiza hilo muda wote, siyo kipindi cha Mkutano wa ccm.

Ana maana baada ya mkutano kuisha madereva hao warudie kwenye enzi zao za vurugu utapeli na usumbufu kwa abiria!

Dawa ya hawa wakuu wa mikoa ni kuwafuta kazi kwenye Katiba mpya hawa.
 
Hivi vyeo ni vya kuvifutilia mbali.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Uccm unamsumbua huyu mama. Mbona kwenye kampeni za m4c hajasema lolote?
 
Uccm unamsumbua huyu mama. Mbona kwenye kampeni za m4c hajasema lolote?
Kama utakumbuka vema ni kwamba mwezi March Mama huyuhuyu alipiga marufuku mikutano yote ya siasa mjini Dodoma baada ya kuona M4C iko pale na huku Bunge linaendelea.
 
Huyu mchumba ake na Philipo Mangula siku hizi bure kabisa,nimeamini kweli siasa inaharibu wasomi wetu kwani alipokuwa pale UDSM alikuwa ni asset nzuri sana!
 
Mungu wangu mwalimu wangu masters ya history mliman huyo.. Ubongo wake ndio umekuwa hivyo
 
Hivi huyu Nchimbi ni daktari wa nini? Maana naona anaongea kama mganga wa kienyeji ashakum! Kwake mkutano wa CCM ni mwanzo na mwisho wa kila kitu lazima uheshimike ili asipoteze ulaji wake.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodma mama Rehema Nchimbi amewaomba waendesha vymbo vya moto vya aina zote mjini Dodma kuwa wakarimu, wapole na wenye utu katika kipindi cha siku 3 za mkutano wa ccm mjini hapo...!

Binafsi nimemwona wa ajabu kwasababu yeye kama Mtumishi wa serikali ni wajibu wake kusisitiza hilo muda wote, siyo kipindi cha Mkutano wa ccm.

Ana maana baada ya mkutano kuisha madereva hao warudie kwenye enzi zao za vurugu utapeli na usumbufu kwa abiria!

Dawa ya hawa wakuu wa mikoa ni kuwafuta kazi kwenye Katiba mpya hawa.

Kabla ya kuwa RC alikuwa DC pengine anataka kuwa katibu Mkuu maana maamuzi yake siku zote ni utata mtupu
 
Anatekeleza maagizo ya Pinda, Pinda akijibu swali bungeni alihalalisha wakuu wa mikoa na wilaya kukutumikia chama cha mapinduzi sasa huyu mama hawezi kupingana na boss wake wa kulaumiwa kwenye hili ni Pinda na jk!hawa wakuu wa wilaya na mikoa wanapokea maelekezo toka juu!
 
hao wapo kwa masirahi ya walio waweka ndio maana hana jipya. Lakini kila kitu kina mwisho
 
Mwalimu mjinga,uzalisha wanafunzi wajinga.Hii nayo ni vipi?

Siyo lazima. Mchango wa Mwl ni kama asilimia 40% au 50% ktk uelewa wa mwanafunzi wake. Mazingira yanayo mzunguka mwanafunzi; wazazi; mwanafunzi mwenyewe uchangia asilimia zilizobaki.
 
Wasomi wote walioko ccm akili zao zimeshikiliwa na mtu mwingine. Wanayoyafanya hayaendani wala kulingana na visomo vyao.
 
()*() .Wapi Mrisho Gambo bingwa wa kugundua elimu ya mtu kaipataje?
 
Wakuu wa mikoa ni makada wa chama cha mapinduzi............................. hivyo ni haki yake kuimarisha mazingira kwa kipindi chote ccm wanafanya vikao vyao
 
good reasoning.

"Binafsi nimemwona wa ajabu kwasababu yeye kama Mtumishi wa serikali ni wajibu wake kusisitiza hilo muda wote, siyo kipindi cha Mkutano wa ccm.

Ana maana baada ya mkutano kuisha madereva hao warudie kwenye enzi zao za vurugu utapeli na usumbufu kwa abiria!"
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodma mama Rehema Nchimbi amewaomba waendesha vymbo vya moto vya aina zote mjini Dodma kuwa wakarimu, wapole na wenye utu katika kipindi cha siku 3 za mkutano wa ccm mjini hapo...!

Binafsi nimemwona wa ajabu kwasababu yeye kama Mtumishi wa serikali ni wajibu wake kusisitiza hilo muda wote, siyo kipindi cha Mkutano wa ccm.

Ana maana baada ya mkutano kuisha madereva hao warudie kwenye enzi zao za vurugu utapeli na usumbufu kwa abiria!

Dawa ya hawa wakuu wa mikoa ni kuwafuta kazi kwenye Katiba mpya hawa.

Nadhani umetoroka Mirembe hosipitali. Mkutano huo Ni ujio wa watu wengi Dodoma hivyo lazima RC Kama Kiongozi wa mkoa aandae Wananchi wake ili waweze kuendesha maisha yao sambamba na umati wa wajumbe wa Mkutano huo wa ccm
 
Back
Top Bottom