Serikali: Kupanda kwa bei ya Nyama kunatokana na upungufu wa Ng'ombe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.

Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.

Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000.
 
Jibu la kipumbavu sana kutoka kwa huyo waziri. Suala la idadi ya mifugo katika nchi ni sera ambayo inapaswa kusimamiwa na serikali ili kuregulate bei ya nyama pamoja na mifugo hiyo katika nchi.

Huyu waziri ni sawa na anawaambia wananchi kuwa kazi imemshinda, halafu sad enough hana hata habari kuwa anadeliver message kama hiyo.

Wafanya biashara katika habari hii wanaonekana kutoa sababu ambazo ni za kiuchumi na ambazo ni genuine kuliko waziri mwenye dhamana.
 
Nyama kuuzwa 8,000 bei iliyochangamka asee atleast iwe 5000 hadi 6000

Lakn kusin ndio bei hiyo tangu 2013 nimeikuta hiyo bei ya 8000 had sasa
 
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.

Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.

Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000.
Wapromote ufugaji wa Ngrooohhhh? Miezi sita tu anaingia sokoni, wakati Ng'ombe anahitaji miaka miwili na uzao wao ni wa 1\1\ na mimba ya miezi 9. Wakati Ngrooohhh mimba moja watoto 12 na mimba ni miezi mitatu tu.
 
Halafu quality ya nyama inashuka kipindi hiki kwa mifugo kukondeana kutokana na upungufu wa malisho na maji, hivi haiwezekani hivyo viwanda vya kuchakata nyama vikavuna hawa mifugo wakiwa kwenye hali nzuri kiafya na kuhifadhi kwenye majokofu kwa ajili ya kuendelea kusambaza nyama bora sokoni? au soko la hivi viwanda ni kupeleka nje ya nchi tu hasa arabuni. Ni bora wizara ithibiti hivi viwanda kusafirisha nyama nje ya nchi ili kunusuru lishe za watanzania, kwenye samaki tunapigwa na huku kwenye nyama tupigwe? tutakuwa wageni wa nani.......
 
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.

Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.

Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000.
Kwanini Afrika ina mawaziri wapumbavu ?
 
Back
Top Bottom