ahahahhaaaha nimecheka sana sana ni kweli nilifika Chato nikitokea Bukoba kuelekea Mwanza. Nilipita pale Chato saa kumi jioni, kwenye zile taa ilikua gari yetu, Baskeli upande wa pili na sijui ng'ombe au Punda wale. Dah nilishangaa sana sana sana.
Tulionywa pia na mwenyeji wetu mmoja kuwa kule lazima kwenye zebra usimame hata kama uko peke yako maana hata Mwenyekiti wa Kiyongoji anaweza kukukamata, atakusimamisha ukijua anaomba Lift kumbe anakukamata.
Niliona pia ujenzi mkubwa sana sijui ilikua ni kitu gani kile au ndio lile Jengo la TRA???