Tangantika
JF-Expert Member
- Aug 12, 2018
- 4,941
- 6,199
Mbona makbora hujataka au sio muhimu kwa Korea kusini.Korea kaskazini, ndo nchi pekee Duniani ambayo raia wake hawaruhusiwi kuwa na Dini yaani hakuna waislamu wala wakristo marufuku!
Korea kaskazini, ndo nchi pekee Duniani ambayo vitabu vitakatifu vya Dini haviruhusiwi kuingia nchini humo.
Korea kaskazini Rais anaheshimika kama Mungu.
Korea kaskazini, kuvaa vimini marufuku.
Korea kaskazini, rais akiongea ukisinzia unapigwa risasi. Mwaka juzi waziri wa ulinzi alipigwa risasi hadharani kwa kosa la kusinzia kwenye kikao wakati rais akiongea.
Korea kaskazini, ndo nchi pekee Duniani iliyowahi kuiteka nyambizi ya Marekani.
Korea kaskazini, adhabu ya kifo ni adhabu ya kawaida mno.
Korea Kaskazini, ni familia moja tu ndio inaongoza nchi.
Korea kaskazini, hakuna vyama vingi.
Korea kaskazini, hakuna uchaguzi wa rais hurithishana.
Korea kaskazini, kuna style 18 tu za kunyoa nywele na kila raia anatakiwa kunyoa style hizo. Style ya kiduku ni style anayotakiwa kunyoa rais tu.
Korea kaskazini, ndo nchi inayoongoza kwa kuwa na mabalozi wachache Duniani.
Korea kaskazini, ndo nchi inayoongoza kwa raia wake kutoroka nchi.
Korea kaskazini, haina ubalozi Tanzania.
Korea kaskazini, raia hawaruhusiwi kuangalia Movies za nje ya nchi.
Korea kaskazini, raia hawaruhusiwi kuangalia taarifa za habari za nje.
Korea kaskazini, ndo nchi pekee Duniani ambayo rais wake hajawahi kufanya ziara Africa.
Korea kaskazini, ndo nchi pekee Duniani ambayo hairuhusu mtu kuomba uraia.
Korea kaskazini, ndo nchi pekee Duniani ambayo raia wake hawaruhusiwi kutoka nje ya nchi isipokuwa kwa kazi maalum ya kiserikali.
Korea kaskazini, hutumia kalenda ya peke yao yaani kwao kwa sasa ni mwaka 105 huanza kuhesabu mwaka aliozaliwa babu yake rais wa sasa Kim John Un.
.
Korea kaskazini, kuvaa jeans marufuku.
Korea kaskazini, bange ruksa kuvuta, kulima na kuuza.
Korea kaskazini, ni marufuku kuongea kingereza. Ukigundulika unaongea unanyongwa.
Korea kaskazini, ndio nchi inayoongoza kwa mabalozi wake wakistaafu kutorudi nchini humo yaani hutorokea huko huko.
Korea kaskazini, raia wa Korea kusini haruhusiwi kabisa kuingia Korea kaskazini, ila raia wa Korea kaskazini anaruhusiwa kuingia Korea kusini bila viza.
Korea kaskazini, ndo nchi yenye rais mdogo zaidi Duniani.
Korea kaskazini, rafiki yake mkubwa ni China.
Korea kaskazini, hakuna mitandao ya kijamii yaani hakuna Facebook, Twitter, Whatsup, Instagram nk,
Hiyo ndio Korea kaskazini.
View attachment 1431853
Sent using Jamii Forums mobile app