Msuele
Member
- Dec 5, 2016
- 65
- 35
Miaka 15 nyuma iliyopita nilikuwa nikiishi na babu yangu, ambaye alikuwa ni matibabu wa matatizo ya kiswahili, alifanya kazi hiyo kwa muda mrefu sana na alikuwa akinishirikisha katika tiba zake, mimi bila kuelewa alikuwa akimaanisha nini kunikaribisha katika shughuli zake na hali ya kuwa mimi na mdogo sana kiumri.
Kuna siku babu aliniita kwenye ofisi yake na wakati natoka ili kuelekea katika kibanda kilichopo nje ya nyumba yetu nilikuta gari kubwa ambalo sikuwahi kumuona nalo mtu yeyote katika maeneo haya ambayo tulikuwa tukiishi na babu.
Nikashangaa sana lakin bila ya kupoteza muda nikaelekea kwenye ofisi ya babu na nikamkuta mtu mkubwa mwenye tumbo kubwa na ananukia kiasi ambacho sikupenda atoke tena maana sikuwahi kusikia harufu nzuri kiasi kile kwani kila siku nikiingia huwa naisikia harufu kali ya udi na ubani.
Babu akaniambia kaa hapo mjukuu wangu, bila ya kusita nikakaa, Babu akaanza kumuambia yule jamaa haya sema shida yako nini? Yule jamaa akaanza kusema, mtaalam mimi ninashida kubwa sana sijui utanisaidiaje.
Mmh!Nikaguna na kushangaa kimoyo moyo huyo baba ana shida gani kwasababu na babu mbona anaonekana kama hana pesa za kumzidi yeye, nilijisemesha moyoni bila ya kupata jibu nikaamua kutulia na kumsikiliza babu nini atamjibu.
Babu akamuambia wewe sema una tatizo gani usifiche kitu, yule baba akasema mimi ni mfanyakazi katka ofisi za serekali, bila ya kuhitaja jina ni ofisi gani ila aliendelea na maelezo yake ila shida yangu ni sihitaji bosi wa ile ofisi anisikilize kwa kila nitakacho muambia na pia nahitaji kugombea Udiwani wa kata pia nahitaji wananchi wanichague bila kipingamizi. Yule baba aliishia hapo katika maelezo ambyo alikuwa akimueleza babu.
Babu akamuambia sawa kijana nimekuelewa nitajie jina lako na jina la mama yako nikupe kitu ambacho kitakusaidia katika mambo yako unayoyahitaji. Jamaa bila kushangaa alitaja jina lake na jina la mama yake, babu alichukuwa karatasi nyeupe na rangi nyekundu ambayo nilimsikia akiita kwa jina la Zafarani, na akachukuwa kitabu kikubwa ambacho sikuelewa ndani mmeandikwa nini.
Lakini babu alianza kufunua kurasa za kile kitabu na akaanza kuchovya ile rangi kwa kutumia kijiti na kuanza kuchora michoro ambayo sikuielewa inamaanisha nini,
ila baada ya kukitazama vizuri kile kitabu niliona kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu ambayo sikuwa ni mwenye kuielewa daaah.! Nilichoka sana kuona kile kitabu maana haikuwa mara ya kwanza wala ya pili kumuona babu na kitabu kile. Nilitamani kujua kukisoma mule ndani kwasababu nilikuwa nikimuona babu akiwasaidia wengi sana wenye matatizo haswa wenye majini ya kupewa. Basi mimi nilibaki tu kutamani kujua kuwa nitaweza vipi kukisoma na hali ya kuwa kina lugha nisiyoijua.
Haya babu akaendelea na kazi yake alipo maliza kuandika akaanza kutengeneza kitu mithili ya hirizi, na akaisokotea kwa uzi mweupe baada ya kuimaliza nikagundua kuwa ile ni hirizi na akaanza kuifukiza kwa ubani na huku akiwa anasema maneno ambayo sikuyaelewa na akamkabidh yule jamaa. Baada ya kumkabidhi akamuambia kila utakapoenda usisahau kuwa nayo.
Yule baba akasema nimekuelewa babu. Eehee babu kazi yako unafanya kwa bei gani.? Aliuliza yule baba kumuuliza babu. Babu akamjibu huwa ANZIMA kama hizo huwa nafanya kwa laki 5 ila wewe utanipa uliyokuwa nayo, babu alisema na kuishia hapo. Mmh mimi nikashangaa sana kuwa kidude kile kinauwezo kiasi gani mpaka akakiuza kwa pesa hile mmh! Nilijiuliza sana ila sikupata jibu kamili.
Bs yule baba akampa babu kiasi cha laki tano kama alivyotaka mwanzo na akamuahidi kuwa akifanikiwa atampa zawadi nono kuliko hiyo. Basi akatuaga na kuondoka zake mimi nikabki na babu mule ndani, nikaanza kumuuliza babu ilikutaka kujua kuhusu kile kitabu, Babu hivi hiki kitabu kinaitwaje? Babu bila kunificha akanijibu mjukuu wang hiki kinaitwa AUFAKIL AZZAL hiyo ni kwa lugha ya Kiarabu ila Kiswahili ni upanga wa zamani, Mmh babu kwanini kiitwe hivyo? Babu alicheka na kunishika kichwa na kusema usijali mjukuu wangu utayajua yote hayo ila nahitaji usome sana madrasa mjukuu wangu tena sana.
ITAENDELEA ...