Maajabu ya Kisiwa cha Jibondo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
000000000000amanibahari.jpg
JIBONDO ni kisiwa kidogo katika eneo la Kisiwa cha Mafia kilichobeba jina la wilaya ndani ya Mkoa wa Pwani.
Kisiwa hicho ni moja kati ya visiwa vidogo takriban vitano ndani ya Kisiwa Kikuu cha Mafia kilichopo karibu na mlango wa Mto Rufiji kuingia Bahari ya Hindi eneo la Kusini mwa Tanzania.


Mbali ya Jibondo, visiwa vingine wilayani Mafia ni Chole, Juani na Bwejuu.

Wakati Wilaya ya Mafia inatajwa kuwa miongoni mwa maeneo yaliyoachwa nyuma katika maendeleo hapa Tanzania, Kisiwa cha Jibondo ambacho pia ni kijiji kimeachwa nyuma zaidi katika maendeleo mbali na fursa zilizopo.

Kwa mujibu wa wakazi wa Jibondo maana na jina hilo ni jiwe kubwa na ndivyo kilivyo kisiwa hicho, kwani kipo juu ya mwamba.

Kijiji hicho ni cha asili na kimekuwepo kwa zaidi ya karne tatu huku wenyeji wake wakiwa ni Wamatumbi na Washirazi.
Hata hivyo, kwa sasa Jibondo kuna makabila mengine ikiwamo Wamakonde, Wandengereko na makabila mengine yenye asili ya Pwani.

Hali ya miundombinu kisiwani Jibondo siyo ya kuzungumzia kwa kuwa hakuna umeme zaidi ya umeme wa jua unaoonekana katika jengo la Zahanati ya Jibondo, hakuna barabara, pikipiki wala gari ingawa hali hiyo pengine inachangiwa na eneo kilipo kisiwa hicho, ukubwa wake au uhalisia.

Baiskeli zipo na wananchi wa Jibondo wanasema: "Hatujui ni karne gani tutakuwa na ndoto ya kupata umeme wa Tanesco."

Ili uweze kufika Jibondo kama umetokea Dar es Salaam, lazima utumie boti isiyo ya uhakika wala usalama kutoka Nyamisati Wilaya ya Rufijivau ndege ndogo hadi Kilindoni mjini Mafia, ndipo upate usafiri wa gari hadi Utende hapo tena upande boti au mashua hadi katika kisiwa hicho.

Safari za mashua kwa kawaida huchukua muda mrefu, zikiwa pia na hatari na misukosuko, lakini ukweli unabaki kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kufika Jibondo.

Zaidi ya hapo kwa wakazi wa Jibondo mawasiliano pekee rahisi kwao ni simu za mkononi ambazo wakazi wake wengi hasa vijana wanazimiliki.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Fakhi Ali Hassan(CUF) na Diwani wa Kata ya Jibondo, Sadick Bakari Sadick (CCM), walinipokea katika eneo la Kilindoni kwenda Utende na kuvuka pamoja nami kwa boti hadi Kisiwa cha Jibondo umbali unaokadiriwa kuwa kilometa nane hadi tisa, ambapo nilishuhudia na kuelezwa mengi niliyoanza kueleza kuhusu kisiwa hicho.
Kabla kuanza safari kuelekea Jibondo, ufukweni mwa bahari nilishuhudia boti na mashua za uvuvi nne zilizoegeshwa zikiwa zimejaza madumu ya kuhifadhia maji.

Niliuliza wenyeji wangu: "Kulikoni hali hiyo?" Nao walijibu: "Haya ndiyo maisha ya Jibondo miaka nenda rudi."
Nilipotaka ufafanuzi zaidi, Diwani Sadick aliyeeleza kuwa ni mzaliwa wa kijiji hicho kutoka kabila la Wamatumbi alinieleza kuwa kwa kiasi kikubwa hiyo ni sehemu ya maisha ya watu wa Jibondo pamoja na visiwa vya Juani na Chole.
Alieleza kuwa kila siku asubuhi, mchana hata jioni wakazi hao hulazimika kusafiri baharini kwa umbali huo kwa kupisha ili kufuata maji kijiji cha Utende.


Niliposogea karibu nilishuhudia baadhi ya wananchi na wamiliki wa mashua na boti hizo wakizaja maji kwenye madumu tayari kupeleka Jibondo.

Katika mazungumzo yetu baada ya kufika Jibondo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Fakhi Ali Hassan anasema:
"Kila boti inabeba madumu 150, kila siku asubuhi boti 10 zinakwenda kusomba maji na jioni boti 10. Kila dumu la lita 20 huchotwa na kusafirishwa kuja kijijini ambapo huuzwa kati ya Sh500 hadi Sh700 kutegemea upatikanaji wa mafuta kuendeshea boti ambayo ni ghali."

Anasema kuwa kutokana na hali halisi na ukubwa wa gharama siyo jambo la ajabu mkazi wa Jibondo kulala siku tatu bila kuoga.

"Hapa Jibondo kukaa siku tatu bila kuoga siyo jambo la ajabu,"anasema akihoji: "Leo miaka 50 ya uhuru hatuna maji, kikwazo nini au hatustahili kutumia kodi tunayopeleka serikalini?"

Kuhusu tatizo hilo la maji Diwani Sadick anaongeza: "Kwa namna yoyote ili kuokoa watu wa Jibondo na wakazi wengine wa kata hii lazima miradi ya maji itekelezwe ikiwa kwa kujengwa malambo ya maji au yawekwe mabomba."
"Mbona imewezekana kutoa maji Mwanza hadi Shinyanga, vipi sisi hapa Jibondo maji yapo ng'ambo tu.?"


Anasema kuwa eneo hilo lipo lililojengwa mwishoni mwa miaka ya 1960, hata hivyo, limechakaa na kukosa ukarabati kwa muda miaka zaidi ya 16, mbali ya kutokidhi mahitaji kutokana na kuwa dogo ikilinganishwa na idadi ya watu waliopo sasa Jibondo.

Kuhusu idadi ya watu Mwenyekiti wa kijiji hicho, Fakhi Ali Hassan anaeleza kuwa idadi ya watu waliopo katika kijiji hicho ni zaidi ya 3000, huku asilimia 98

wakitegemea uvuvi na kazi nyingine za baharini ikiwemo kilimo cha zao la mwani.

Hiyo inatokana na hali halisi na ukweli kwamba Kisiwa cha Jibondo kuwa ni mwamba ambao hata hivyo unaovutia ukiwa na maajabu ya maisha ya watu juu yake kwa zaidi ya karne tatu sasa.

"Jibondo ni kijiji cha asili kipo kwa zaidi ya miaka 300 na wakazi wake hata wahamiaji ni wavuvi," anaeleza Hassan.
Ardhi ya kisiwa hiki imefunikwa kwa jiwe zaidi ya asilimia 98 huku minazi ikizunguka maeneo ya ufukweni tu pamoja na nyasi fupi kwa uchache kwenye maeneo machache, ambazo hutumika kulisha ng'ombe na mbuzi wachache waliopo Jibondo.


Nilitaka pia kujua iwapo wakazi wa Jibondo wana redio na televisheni au kwa namna nyingine wanapataje habari au taarifa za kila siku kuhusu hali ya nchi inavyokwenda na je kuna tawi la benki yoyote au kituo cha polisi?
Swali hili lilijibiwa kwa pamoja na mwenyekiti wa kijiji hicho na diwani.

"Redio ipo pale zahanati, Tv hakuna,"alisema mmoja wa viongozi hao.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Fakhi Hassan alisema: "Lakini wapo baadhi ya watu ingawa wachache wana Tv, hutumia kama kitega uchumi kwa kuonyesha video kutumia umeme wa jua au jenereta."

Kuhusu Kituo cha Polisi Diwani, Sadick alisema: "Hapa kijijini hakuna kituo cha polisi wala polisi, lakini kama Kata ya Jibondo tumepewa askari kata wawili, tunasubiri ujenzi wa nyumba mbili kwa ajili yao ukikamilika watakuja kuishi huku."

Ni nadra kukuta mti wa matunda au chakula kama vile mpapai au mihogo katika Kisiwa cha Jibondo hivyo kukifanya kijiji hicho kutegemea kupata chakula chake nje ya kijiji hicho, iwe Kilindoni au kutoka jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa imani mwenyekiti wa Kijiji cha Jibondo anasema kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu huku eneo hilo likiwa na misikiti mitatu na madrasa mbili.

Hata hivyo, umaarufu wa Jibondo unatajwa na walio wengi wilayani Mafia kuwa ni kutokana na watu wake kwa kiasi kikubwa kuwa wavuvi huku wakiwa na vuguvugu la kisiasa lililo na sura mbili.

Upande mmoja ni chama tawala CCM na upande wa pili ni Chama cha Wananchi (CUF).

Anaeleza kuwa kijiji chake kina zaidi ya nyumba 600 huku kila kaya ikikadiriwa kuwa na watu kati ya wanne na watano.

Anafafanua kuwa Wakristo wachache wanaoweza kuwepo katika kijiji hicho ni watumishi wa umma wanaokwenda kufanya kazi Jibondo.
Kisiwa cha Jibondo kina shule moja ya msingi iliyo na wastani wa wanafunzi 325 na walimu watatu ambapo hata hivyo Mwalimu Mkuu, Mrisho Mkungu,

amepewa kazi ya uofisa mtendaji wa kijiji hivyo, kutokuwepo shuleni muda mwingi na shule hiyo kubaki na walimu wawili.

Pia kuna viwanja vinne vya michezo kimoja kikiwa eneo la Shule ya Msingi Jibondo iliyojengwa miaka ya 1950.
Jibondo ina zahanati moja iliyo na watumishi watatu, mmoja kwa sasa akiwa masomoni.


"Katika zahanati hii tunahitaji daktari kamili, pia zahanati ndogo. Wajawazito wengi hulazimika kupelekwa nje ya kijiji, kwa kiasi kikubwa kwenda Kilindoni," alisema Diwani Sadick akiungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji:

"Ukipata mgonjwa hapa, ni wewe mwenyewe ujue utapata wapi boti na mafuta ya kumpeleka hospitali ni lazima uwe na Sh100,000 au zaidi."

Kuhusu tiba za asili mwenyekiti wa Kijiji cha Jibondo anasema kuwa katika eneo lake hakuna mganga wa tiba asilia, ingawa anaamini wapo wanaotumia tiba hizo na kwamba hilo ni suala la uamuzi wa mtu binafsi.

Anasema kuwa Jibondo pia hakuna soko, lakini yapo maduka madogo machache ya watu binafsi hali aliyosema inasababisha wananchi kutegemea zaidi kununua bidhaa kutoka Kilindoni au Dar es Salaam.


Kuhusu ujenzi wa nyumba, Fakhi anabainisha kuwa kwa asili hujenga nyumba za kutumia mawe ya baharini ambayo hata hivyo sasa wanazuiwa kuvuna na Mamlaka ya Hifadhi za Bahari (Marine Park)

"Hawa Marine Park siyo tu wametuzuia kuchukua mawe ya kujenga nyumba wakisema tuchukue mawe yaliyokufa bali hata kufanya uvuvi. Sasa mwananchi wa kawaida anajuaje jiwe lililokufa? Hapo inahitajika elimu," anasema.

Baadhi ya wananchi wanaunga mkono hoja hiyo wakieleza kuwa kuanzishwa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (Mafia Island Marine Park – MIMP) ingawa kulielezwa kuwa ni kwa nia njema, lakini sasa ni sawa na kiama kwao.
"Tunakwamishwa na Marine Park kupata matumizi binafsi, hatuwezi hata kulipa karo.


Wanatukamata hata kutubambikiza kesi. Hali hii imevuruga uchumi wote wa kijiji kwani kwa ardhi ya Jibondo huwezi kulima, awali tulipata walau Sh5000 kwa siku, sasa hata Sh3000 ni bahati kuzipata," alisema mkazi wa Jibondo Haji Ahmad Amri.


Naye Fakhi Shujaye alisema: "Kwa hali ilivyo hapa Jibondo tunashindwa hata kuwaamini viongozi wetu, hatuoni kinachoendelea, tunazuiwa kuvua kila mahali hata maeneo ambayo awali hao Marine Park waliruhusu kuvua. Familia zinachanganyikiwa kwa kukosa kipato."

Mwingine anasema kuwa: "Kwa hali ilivyo sasa kwetu ni hatari, unakata leseni ya uvuvi, lakini unazuiwa kuvua. Sasa tumechoka liwalo na liwe, ama zao ama zetu."

Hata hivyo, mwenyekiti na diwani wa Jibondo wanaona kuwa upo umuhimu kwa taasisi ya Marine Park kurejea makubaliano ya awali na wanakijiji hata kukutana nao ili kuwaelimisha upya kuhusu uhifadhi wa bahari ili wananchi wa Jibondo waweze kuendeleza maisha yao.

Kuhusu siasa wananchi hao wanasema kuwa hali mbaya ya Jibondo inaweza kuwa imechangiwa na tofauti ya kisiasa baina ya uongosi wa Serikali ya kijiji chao na Wilaya ya Mafia.

"Hapa naona siasa ni changamoto nyingine, sisi hapa Jibondo ni CUF wilayani ni CCM, hivyo viongozi hawafiki. Tukikataa mradi wanalazimisha tuukubali, tukiukubali wao wanakataa. Hilo linatugombanisha na viongozi wetu hapa kijijini hata wa kata. Lakini mbaya zaidi hatujamwona Mbunge tangu tulipomchagua, wala Mkuu wa Wilaya," alisema Bakili Yusuph Bakili.

Akizungumzia siasa mwenyekiti wa kijiji hicho alisema: Kihalisia sisi bado tunaishi kijamaa kwani sote ni ndugu hapa kijijini, siasa zisitumike kuwatenga watu bali kuwaleta karibu. Sijui hilo lilitokea wapi, lakini sasa msimamo wetu ni mmoja tunataka maji na maendeleo mengine."

Hata hivyo, wananchi hao walipotakiwa kueleza iwapo wanakumbuka kuwa ni lini mara ya mwisho walipotembelewa na kiongozi wa kitaifa walisema kuwa tangu walipopata akili timamu hawajawahi kuona kiongozi wa kitaifa kutembelea Jibondo.

Diwani wa Kata ya Jibondo Sadick Bakari Sadick alisema kuwa anachokumbuka ni kwamba kati ya mwaka 2000 na 2005 walitembelewa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji wakati huo, Antony Diallo pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, marehemu Ditopile Mzuzuri.Maajabu ya Kisiwa cha Jibondo
 
Asante Mzizimkavu kwa habari hii inayoonyesha hali halisi vijijini.

Kwa nini mtu asioge kwa siku tatu kwa kisingizio cha kukosa maji katika kisiwa kidogo kilichozungukwa na maji ya bahari?

Naweza kuelewa watu kukosa maji ya kunywa kwa sababu maji ya bahari ni ya chumvi, lakini ya kuoga?
 
Asante Mzizimkavu kwa habari hii inayoonyesha hali halisi vijijini.

Kwa nini mtu asioge kwa siku tatu kwa kisingizio cha kukosa maji katika kisiwa kidogo kilichozungukwa na maji ya bahari?

Naweza kuelewa watu kukosa maji ya kunywa kwa sababu maji ya bahari ni ya chumvi, lakini ya kuoga?

Kiranga
Unawashauri waogelee au waoge?

Baada ya kuogelea/ kuoga maji chumvi mwili unakuwaje?

Umeshawahi kuoga maji chumvi? Na baadae ukajitupa kitandani?

Hata watu wanaoogelea baharini wanapomaliza hutaka maji ya kawaida ili kuondosha chumvi.
 
Kiranga
Unawashauri waogelee au waoge?

Baada ya kuogelea/ kuoga maji chumvi mwili unakuwaje?

Umeshawahi kuoga maji chumvi? Na baadae ukajitupa kitandani?

Hata watu wanaoogelea baharini wanapomaliza hutaka maji ya kawaida ili kuondosha chumvi.

Maji chumvi ya wapi?

Maana kuna maji chumvi na maji "chumvi".

Mi nishaoga maji chumvi ya Oysterbay Beach na sikuhitaji kuoga zaidi kwa usiku huo, tena ukioga zaidi unaondoa madini muhimu kutoka chumvi za bahari.
 
asante sana kwa habari hii MziziMkavu
Kweli Tanzania kuna watu wana shida
cha kushangaza waandishi wetu wa habari wanafocus kwenye habari za siasa na mijini
hivi ndio vitu wanatakiwa waandike, vinaelimisha sana jamii. Imagine mimi hata sikujua kama kuna visiwa kadhaa ndani ya mafia.
asante sana
 
Hizo ni shida kama zilivyo sehemu nyingi nchini mwetu, wala si maajabu!
 
ummh! interesting ... shukran MziziMkavu

mkuu Kiranga ukishaoga maji ya bahari mwili unakuwa unapauka .. yaani hujisikii comfortable kabisa .. aim talking through experience mimi nimekulia tanga kijiji chetu kipo ufukweni mwa bahari njia ya kwenda mombasa barabara ya horohoro .. nakumbuka nilipokuwa mtoto mara nyingi baada ya kuoga chumvi au tukitoka kupokea wavuvi ilikuwa huwa tunakwenda kisimani kujimwagia maji ya kawaida
 
Asante Mzizimkavu kwa habari hii inayoonyesha hali halisi vijijini.

Kwa nini mtu asioge kwa siku tatu kwa kisingizio cha kukosa maji katika kisiwa kidogo kilichozungukwa na maji ya bahari?

Naweza kuelewa watu kukosa maji ya kunywa kwa sababu maji ya bahari ni ya chumvi, lakini ya kuoga?[/QUOTE]

UCHAFU NI TABIA jamani...
 
Asante Mzizimkavu kwa habari hii inayoonyesha hali halisi vijijini.

Kwa nini mtu asioge kwa siku tatu kwa kisingizio cha kukosa maji katika kisiwa kidogo kilichozungukwa na maji ya bahari?

Naweza kuelewa watu kukosa maji ya kunywa kwa sababu maji ya bahari ni ya chumvi, lakini ya kuoga?[/QUOTE]

UCHAFU NI TABIA jamani...

Hapana sio wachafu watu wa Jibondo,vijana wengi ni wavuvi wa pweza ambao ni wazamiaji hivyo kama kuoga baharini basi ni kila siku!! Lakini kama walivyochangia wengine, ukitoka kuoga maji ya chumvi (bahari) mwili hupauka hivyo ni lazima upate maji baridi kuondoa yale ya chumvi, angalia hata nywele zao (na wavuvi wengi) huwa nyekundu sababu ya maji ya chumvi na jua.. Fika Jibondo uone mkuu, jamaa hata kuzikana ni tabu maana chini mwamba so kaburi halifiki hata futi 3!!
 
Maji chumvi ya wapi?

Maana kuna maji chumvi na maji "chumvi".

Mi nishaoga maji chumvi ya Oysterbay Beach na sikuhitaji kuoga zaidi kwa usiku huo, tena ukioga zaidi unaondoa madini muhimu kutoka chumvi za bahari.

Mkuu, maji ya baharini baada ya kuoga/kuogelea hayavumiliki kwenye ngozi. Mara moja moja kama ulivyofanya, may be. Na fukwe zetu zilivyokuwa chafu siku hizi, ndo' kabisaa huchelewi kupatwa na magonjwa mengine ya ngozi!!
 
Sasa maajabu ni yepi?

When your head is well up the stinker don't expect to smell a thing! Diwani wa CCM, miaka 35 ya CCM, umeme zero, ndoo ya maji shs. 700/=, etc. etc.... maajabu ni yepi!!
 
When your head is well up the stinker don't expect to smell a thing! Diwani wa CCM, miaka 35 ya CCM, umeme zero, ndoo ya maji shs. 700/=, etc. etc.... maajabu ni yepi!!

Cha ajabu nini hapo?
 
When your head is well up the stinker don't expect to smell a thing! Diwani wa CCM, miaka 35 ya CCM, umeme zero, ndoo ya maji shs. 700/=, etc. etc.... maajabu ni yepi!!

Cha ajabu nini hapo? Hata US kuna visiwa havina umeme na wao ni matajiri na wanajitawala kwa zaidi ya miaka 200.

Wewe umeme wa nini, bibiyo na babuyo walikuwa wanaujuwa umeme?
 
Asante kwa haya maajabu. Kwani kisiwa kuwa juu ya jiwe ni ajabu watu hawawezi lima au kuchimba visima. Nimeongeza uelewa wa Jiografia ya TANZANIA
 
Kwa maelezo yako na maelezo ya wenyeji,hicho kisiwa ni sehemu isiyofaa kwa maisha ya binadamu, kama si ujuha ni nini ? wanatafuta nini maisha yote kwenye eneo ambalo halina miundombinu na ni vigumu kupata hiyo miundombinu,kwa nini wasirudi kwenye maeneo yafaayo kuishi binadamu kama ni shughuli za uvuvi wazifanye kutokea huko ? Wanajua kisiwa chao kiko juu ya jiwe,kuonesha kuwa hata maji si rahisi kupatikana,bado wanajisifu kuwa wameishi hapo kwa miaka zaidi ya 200, kama huo ndiyo ukweli hawana shida labda ni wewe mwandishi uliyekwenda na mfumo wako wa maisha kwa binadamu wenye mfumo tofauti then starehe zao ukatafsiri kama ndiyo shida.
Kuna vitu vingine havingii akilini,unaanzisha kijiji jangwani wakati maeneo mazuri yamejaa tele ili upate nafasi ya kulalamika,tuache kushabikia ujinga
 
Kwa maelezo yako na maelezo ya wenyeji,hicho kisiwa ni sehemu isiyofaa kwa maisha ya binadamu, kama si ujuha ni nini ? wanatafuta nini maisha yote kwenye eneo ambalo halina miundombinu na ni vigumu kupata hiyo miundombinu,kwa nini wasirudi kwenye maeneo yafaayo kuishi binadamu kama ni shughuli za uvuvi wazifanye kutokea huko ? Wanajua kisiwa chao kiko juu ya jiwe,kuonesha kuwa hata maji si rahisi kupatikana,bado wanajisifu kuwa wameishi hapo kwa miaka zaidi ya 200, kama huo ndiyo ukweli hawana shida labda ni wewe mwandishi uliyekwenda na mfumo wako wa maisha kwa binadamu wenye mfumo tofauti then starehe zao ukatafsiri kama ndiyo shida.
Kuna vitu vingine havingii akilini,unaanzisha kijiji jangwani wakati maeneo mazuri yamejaa tele ili upate nafasi ya kulalamika,tuache kushabikia ujinga
Unashangaa hapo maji dumu 500? Sogea mpaka kisiwa cha Nyuni huko dumu moja la maji ni sh 2000
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom