Euphransia
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 937
- 778
Leo kupitia Redio BBC idhaa ya kiswahili kuna mahojiano yamefanywa Na mtanzania kabila la mkurya huko Mara akisema kuwa mila ya kabila hilo ni kwamba ikitokea umekufa bila kuoa ni lazima ndugu yako aende kuchumbia binti Na kumweleza ukweli kuwa anamchumbia Kwa niaba ya marehemu binti akikubali basi taratibu za mahari zinafanyika kamabni ng'ombe 10 zinalipwa.Yule aliyeenda kuchumbia ndio anamzalisha yule mwanamke Na majina k.m Mtoto wa kwanza no mwanaume basi atapewa jina la marehemu.Na watoto wote watakaozaliwa watahesabika in wa marehemu.Pia huyo aliyeoa Kwa niaba ya marehemu ana hiari ya kumwacha yule Mke wa marehemu ili yule Mke aolewe Na MTU anayempenda.Na akiolewa Na MTU atakayemuoa watoto watakao zaliwa hawatakuwa wa yule marehemu.Tunaomba wakurya mchangie zaidi.
Chanzo:BBC redio
Chanzo:BBC redio