Sawa, lakini na ubora wake je, unakidhi? Ubora = maudhui, sanaa iliyotumika, mantiki, mvuto, burudani, nk.
hapo kwenye bilioni 12 naomba ufafanuzi, halafu nadhani tatizo hapa ni kubwa, kwa sababu hata nigeria ambayo iko mbele sana bado movie zake nyingi hazionyeshwi kwenye cines.
Tatizo wateja wa bongo movie ni house girls ambao wao wanapenda kuona mwanamke mrembo kama wema na mkaka handsome aliyejipaka easy black kichwana na kavaa suti ya kuwakawaka,wakiwa wanaishi kwenye ghorofa na kuendesha Range rover.Hivyo target yao ni kuonyesha mapenzi na maisha bora ambayo intended audience inayatamani,hawafikirii utunzi mzuri wa stori na script na kujenga uhalisia kwa kuumiza vichwa na kuwekeza kwenye teknolojia.
hizo takwimu za Bil. 12 umezipata wapi?
hakuna mtu mwenye akili timamu ataenda kuangalia Bongo Movie after all watazamaji wakubwa ni ma house girl