Maajabu ya awamu ya 5

Maajabu ya awamu ya 5

Kulikoni kufanya alichokifanya JPM,alipaswa at least kufanya jambo hili kwa manufaa ya wasomi wa taaluma ya ujenzi na wakandarasi wetu kwa ujumla.

Angekaa na bodi ya manunuzi, wapange wao price list ya hardware materials according to market price kwa wakati uliopo. Then wakae pamoja na construction consultant kutoka Ardhi University waandae kitu inaitwa "rates" ya kila construction item in which itawasaidia kuandaa bill inayoendana na uhalisia, profit margin ktk ujenzi za kumpa Mkandarasi zinaeleweka.

Then waendelee na mfumo ule ule wa kutangaza tender kwa wakandarasi, cha msingi Mkandarasi atakaezidi kiwango kilichopangwa na wataalamu wa bodi asipewe tender, na atakaeangukia kwenye budget stahiki apewe kazi. Its very simple.
 
Namba 1.
Consultant -TBA
Contractor- TBA

Namba 2
Consultant- NHC
Contractor- NHC
Client -NHC

Namba 3
Consultant -Tanroads
Client- Tanroads

Na mengine mtaongezea, Ila ukweli tunaibiwa.
sheria ya manunuzi tupa kule
 
Safi sana mh magu, hatutaki tendering za kutuibia mchana kweupe kwa visingizio vya kufuata utaratibu.
 
Wewe kama ulifika hata form four Basi ulichezea ada ya mzazi wako. Akili yako imejaa tope
Wasomi siku zote wanajibu kwa hoja. Ila wewe ni mmoja wa wendawazimu wanaojibu kwa matusi na kejeli za elimu. My friend elimu yangu na darasa la saba huko form four mbali sana.
 
kumbuka pia ndani ya hizi kuna vitengo tofauti na kila kitengo kina kazi yake maalum.
inaweza kuwa TBA imesimama lakini kuna idara tofauti mtoa uzi usishangae
 
Je value for money ikoje!? hakuna ujanja unjanja safari hii...
 
Thaman ya pesa na mirad iendane Mkuu... lazima Wazalendo wasimamie ilo kwa vitendo na si maneno🙂
 
Mbona kama unajikuna mwenyewe kaka. Hayo ndio maajabu. Kazi IPO. Unatetea wapiga dili nini. Ghorofa la floor NNE mnapiga being ya 5-10 billion sasa mtajenga mawili ama matatu. Majengo yote ya zamani yaliyodumu miaka 50 hadi 100 consultancy na contractor alikuwa nani. Mliua taasisi za umma muingize ubinafsi wenu kupitia kampuni zenu. Mtaelewa tu.
Yote ni kazi ya CCM ......................!!
 
Mimi nadhani Magu anafanya vizuri katika hili. Zaidi, anatakiwa kukaa na mashirika yote yenye miradi ya kitaifa. Apige mahesabu ya kila miradi, huku akishirikisha wataalamu wachache ambao hawana sifa ya kupiga dili. Baada ya hapo atangaze tender ili baadaye apatikane mzabuni anayeendana na gharama zilizopatikana kwa kila mradi.
 
Baba Consultant tokea zamani walikuwepo. Hivi unafatilia vizuri haya mambo au unaropokwa tu.
ni sawa na kuweka internal auditor na external auditor kampuni moja.
 
Namba 1.
Consultant -TBA
Contractor- TBA

Namba 2
Consultant- NHC
Contractor- NHC
Client -NHC

Namba 3
Consultant -Tanroads
Client- Tanroads

Na mengine mtaongezea, Ila ukweli tunaibiwa.

Kweli hii ni mpya yaani consultant ambaye ni mshauri ,ndiye mjenzi na ndiye mteja. NHC wanamshauri NHC juu ya NHC kujenga gorofa linalomilikiwa na NHC. Kwenye public procurement act No.7 ya mwaka 2011 na ragulations zake za mwaka 2015 kuna kipengele kilikuwa kinakataza jambo kama hili. Lakini huenda kwenye yale marekebisho hili wameliona sawa huenda kwasababu NHC na TBA ni mashirika ya umma hii ni hatari sana kwa ubora wa majengo yenyewe lakini pia kwa usalama wa raia watakaotumia hayo majengo lakini mbaya zaidi iko kwa CONSULTANTS NJE YA MASHIRIKA YA UMMA YENYE JUKUMU LA UJENZI NCHINI. Waombe Mungu TANROADS nao wasifuate huu mkubo itakuwa kilio kwao.
 
Kulikoni kufanya alichokifanya JPM,alipaswa at least kufanya jambo hili kwa manufaa ya wasomi wa taaluma ya ujenzi na wakandarasi wetu kwa ujumla.

Angekaa na bodi ya manunuzi, wapange wao price list ya hardware materials according to market price kwa wakati uliopo. Then wakae pamoja na construction consultant kutoka Ardhi University waandae kitu inaitwa "rates" ya kila construction item in which itawasaidia kuandaa bill inayoendana na uhalisia, profit margin ktk ujenzi za kumpa Mkandarasi zinaeleweka.

Then waendelee na mfumo ule ule wa kutangaza tender kwa wakandarasi, cha msingi Mkandarasi atakaezidi kiwango kilichopangwa na wataalamu wa bodi asipewe tender, na atakaeangukia kwenye budget stahiki apewe kazi. Its very simple.
Wataalamu walioajiriwa serikalini waendelee kuwa watazamaji.

Au waendelee kusaini daftari la mahudhurio na kuondika kusubiri mdhahara.

Wote ni wasomi wa tanzania hii hii.
 
Bahati mbaya watakaofia ndani ni ndugu zetu wao wakipeta na kupongezana kwa walichovuna
Hii hoja ya majengo kuanguka ikoje. Kwamba hao wajenzi toka taasisi za serikali hawana uelewa wa kazi husika au?

Acheni upotoshaji. Tumeshuhudia makampuni binafsi yakilipua kazi za ujenzi kila mahala hatuwashangai mbapotetea kitumbua.
 
Back
Top Bottom