Maajabu ya Airtel wana maitainance charges kwa ajili ya airtel money

chrissmeck

Senior Member
Nov 14, 2013
110
105
Jana nimepokea ujumbe kutoka Airtel wakiniambia wanitoza sh. 180 kama maitainance charges kwa kuwa sijatumia Airtel money. Hii imekaaje wakuu? Kwa uelewa wangu bank ndo zinatoza hii ada. Sijajua kama mitandao mingine wanafanya hivi. Kama nao wapo huu ni wizi mkubwa sana ikitegemea sijawahi kukubalia nao kama watanitoza hela kwa kutotumia account. Au kw vile imeitwa account so lazima iwe na sifa za Bank account!

My take:
Airtel wajaribu namna ya kushawishi watu kutumia airtel money ila sio kwa mtindo huu

6902544439a2a38c08825354f3fe004d.jpg
 
Mkuu benki hawatozi ada ya maintenance kwa sababu "hujatumia akaunti".. Maintenance charges zipo muda wote utumie usitumie.Na benki wanakulekeza yote hayo unapofungua akaunti hawakushtukizi kwa makato usiyoyajua. Benki usipodeposit hela kwa muda mrefu akaunti inafungwa. Hili la airtel limekaakaa kama penalty na sio maintemance.
Waambie kuwa huhitaji tena hiyo akaunti kwa sababu hizo gharama za maintenance hazipo kwenye mkataba wenu kwa hiyo waisitishe. Mitandao ya simu inatoza gharama kubwa mno za.miamala. Kwa nini waanze kudai na maintemance charges? Huo ni upuuzi kabisa.
 
Doh hii mpya,ase sidhani ka ishawahi kutokea kwa mtandao mwingne wowote tz.
 
Duh me mbona airtel money yangu inafika hadi miezi 4 bila kutumika na hamna hayo makato
 
Dawa ni kubaki na salio la sifuri kwenye airtel money tuone wataitoa wapi hiyo pesa ya maintenance.

Wanasahau siku hizi kuhama mtandao wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba yako ni jambo dogo sana, tena inakua rahisi zaidi unapokua na salio la sifuri.
 
ila nawe umezidi,180 unaanzishia uzi..hapana
 
Hata mimi walinitumia alafu Kwa bahati mbaya nimesahau password ya Airtel money kila ninapojaribu hata kupiga 100 sipati msaada
 
Hii kampuni ni wezi kbs. Nina ushahidi kuna siku waliniibia 1200. Kupita kuna lidada limoja utadhani linakunya keki likanijibu ndivyo sivyo nilichukia sana. Huyo juha moja anasema eti "hata 180 unadai?" Alitaka ziwe ngapi ndio adai? Je watu 100 wakiibiwa hivyo kwa saa 1 tu ni kiasi gani? Watanzania wengi tuna mtindio wa ubongo nadhani. Sio lazima kutoa comment just because u hv an account.
 
Ila kuna siku nilipiga customer care nikasaidiwa na kijana mmoja jamani huyu kweli anajua kazi yake na anaipenda. Lugha tamu yenye afya (palatable) anajua maana ya customet care kwa kweli. Naomba hao wadada wa customer care services eajifunze toka kwa huyu Hassan Nkinda ni mfano wa kuigwa. Naomba hii kampuni impe nafasi ya kuwapa somo wenzake.
 
sahihisho: mtoa mada airtel wamekutoza tsh 300 sio 180. hiyo 180 ni idadi ya siku ambazo hukuwa unatumia huduma yao ya airtel money
 
Hii mitandao sasa imechanganyikiwa,
km una mtu unataka umpe 100,000/ ni bora uitoe na umpelekee
wao wakifanya hivyo wanakukata sh 3,500
 
  • Thanks
Reactions: OTG
Mimi pia wamenitumia et watanikata sh300,huu ni uboya uliotukuka ujambazi fraud,tcra wako kumlinda nani ivi au Wana mgao wao kwa kila ujambazi tunaofanyiwa watanzania
 
Ukipiga simu huduma kwa wateja. ..hauunganishwi kuongea na mtu wa Airtel.

Inasikitisha sana.
 
hii mitandao inasikitisha sana, mm wiki iliyopita nilikua nazunguka vijijini, nikakosa vocha za halotel ikabidi ni kope 1000, ili nipate bundle niperuzi jf, kwa hiyo nikaunga 500 ya kwanza, nilipotaka kuunga mia tano ya pili nashangaa sms inakuja eti huna salio lakutosha, nilipoangalia salio wameshakata mia mbili, jioni nikakuta wamekata mia themanini, siku iliyofuata salio sifuri. na hapo ujue nilikua sijafungua data mchana wote, kwa sababu nilikua nasubiri usiku nitakapokua nimemaliza shughuli zangu ndipo niingie jf. costumer care hawapokei simu, ni shida hii mitandao...
 
Back
Top Bottom