Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Kama kawaida yetu Tanzania tumebadili gia angani kwa mara nyingine.
Lengo la Serikali yetu tangu 2013 ni kuuza umeme nje ya nchi. Tena tulijipa mwaka tu hadi kutimiza lengo hili. Yaani tuliambiwa na Muhongo kuwa tutakuwa na Megawati 500 za ziada za kuwauzia majirani zetu wenye shida ifikapo 2014.
Rejea>> Tanzania kuuza umeme nje ya nchi kuanzia mwakani
Muhongo aliyasema hayo kitaalam kabisa akigusia mradi wa Kinyerezi na pia gesi ya Mtwara.
2014, Injinia Felchesmi Mramba alipeleka 'deadline' hadi 2016 na kusema tena kuwa tutauza umeme nje katika Mkutano Mkuu Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la TANESCO na kuongeza matumaini kuwa TANESCO imeshasaini mikataba ya kujenga njia za kusambaza umeme kwa nchi tatu za Afrika Mashariki.
Rejea>>Matumaini: Tanzania kuuza umeme nje ya nchi mwaka 2016
Sasa Mkuu wa nchi anaposema tutanunua umeme kutoka nje, anakuwa anatuchanganya.
Sawa bila umeme hatuwezi kuendesha viwanda vizuri lakini sisi sio wa kununua umeme toka nje, tunatakiwa kuwa na umeme extra.
Je, Megawati 500 za ziada zilizoahidiwa tangu 2013 ziko wapi hadi tunataka kununua Megawati 400 kutoka Ethiopia?? Gesi si tunayo au imeisha? Au tunanunua tu kwa sababu ni wa bei rahisi?
Inashangaza sana.