Maajabu nane ya Reli mpya ya Dar - Moro

Maajabu nane ya Reli mpya ya Dar - Moro

Hutawaona majizi chadema wakipongeza kwenye uzi huu, lakini ikikamilika ndio wa kwanza kupanda!

Sasa hivi wako bize kupongeza maendeleo ya nchi zingine ,kenya rwanda, ethiopia marekani etc.
Kwani Chadema wakipanda hiyo treni kuna shida gani? Kwani imejengwa na michango ya chama cha Mapinduzi? Kama imejengwa kwa fedha za umma basi hiyo ni ya watanzania wote bila kujali chama, dini au kabila. Acha chuki za kisiasa. Eti Chadema ndio utawaona wa kwanza kupanda, lazima wapande maana ni treni yao pia kama ilivyo treni ya watanzania wote. Kuumia utaumia sana lakini watapanda tu. Sasa sijui utakunywa sumu siku utakapowaona wamepanda hali wakiwa na magwanda yao!
 
RELI ya Kisasa (SGR) inayojengwa hapa nchini imeelezwa kuwa ni reli bora kuliko zote Afrika. Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), ilianza awamu ya kwanza ya ujenzi Mei, 2017 na inajengwa na Kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi kwa ubia na Kampuni ya Mota-Engil Africa ya Ureno.

Awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ina urefu wa Kilomita 205 zikiwemo Kilomita 95 za njia za kupishania treni na kufanya reli kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kuwa na urefu wa Kilomita 300. Akizungumza na gazeti hili, Meneja wa Mradi huo kutoka Rahco, Maizo Mgedzi alisema ubora wa reli ya kisasa inayojengwa Tanzania uko juu ikilinganishwa na ubora wa reli zilizojengwa kwenye baadhi ya nchi Barani Afrika.

Mgedzi, alizitaja baadhi ya nchi Barani Afrika ambazo zimejenga reli ya SGR kuwa ni pamoja na Ethiopia, Afrika Kusini, Kenya na Morocco. Alisema, reli zilizojengwa kwenye nchi hizo zina uwezo wa kupitisha treni zenye uwezo wa mwendokasi wa kilomita 120 tu kwa saa tofauti na reli inayojengwa nchini ya kupitisha treni za uwezo wa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

“Lakini pia reli tunayoijenga itatumia treni za umeme tofauti na nchi nyingine nyingi ambazo treni zao zinatumia mafuta ya dizeli. Ethiopia wanajenga reli ya kutumia umeme na kipande kidogo cha reli ya abiria Johannesburg, Afrika Kusini nacho kinatumia umeme,” alisema. “Pia sisi tunajenga reli yenye uwezo wa kupishanisha treni zenye urefu wa kilomita mbili tofauti na nchi nyingine ambazo treni zao hazizidi kilomita moja; Viwango vya ubora wa reli tunayojenga Tanzania viko juu kuliko nchi nyingine,”alieleza Meneja wa Mradi, Mgedzi.

MATALUMA NA UPANA WA RELI Kwa kuzingatia ubora na uimara wa reli hiyo, serikali imeamua kujenga reli hiyo kwa kutumia mataluma ya zege na si ya chuma kama kwenye reli ya zamani ambayo inatumika mpaka sasa. Imeelezwa kuwa, reli inayojengwa kwa mataluma ya chuma ina uwezo mdogo zaidi ikilinganishwa na reli inayojengwa kwa mataluma ya zege.

Akifafanua faida ya kutumia mataluma ya zege kwenye ujenzi wa reli ya kisasa unaoendelea, Mgedzi alisema, mataluma ya zegeyataiwezesha reli inayojengwa kubeba mzigo wenye uzito mkubwa zaidi wa hadi tani 35 kwa ekseli tofauti na reli iliyopo sasa iliyojengwa kwa mataluma ya chuma ambayo haiwezi kuchukua mzigo mzito zaidi unaozidi tani 14 kwa ekseli.

Mgedzi alisema, mataluma ya zege yana uwezo wa kuhimili mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa kwa treni ya abiria na mwendokasi wa kilomita 120 kwa saa kwa treni za mizigo tofauti na treni ya sasa inayotumia mataluma ya chuma na mwendokasi wa kilomita 70 kwa saa. Kuhusu upana wa reli hiyo ya kisasa, mtaalamu huyo alisema itakuwa na upana wa milimita 1,435 ambao ni sawa na upana wa mita 1.435 tofauti na reli ya sasa yenye upana wa milimita 1,000 ambao ni sawa na upana wa mita moja.

“Upana mkubwa wa reli tunayoijenga sasa utaiwezesha treni inayotembea juu ya reli kuwa imara, kwenda kwa kasi na kuwa salama zaidi. Kwa hiyo reli tunayojenga ina upana wa milimita 435 zaidi ya reli inayotumika sasa.” “Na tunaposema ‘gauge’ maana yake ni upana wa reli.

Reli ina miguu miwili, yaani kulia na kushoto ambayo imeshikwa na mataluma, kwa hiyo upana kati ya reli moja na nyingine unaitwa ‘gauge,’” alifafanua Meneja Mgedzi. UWEZO WA KUBEBA MIZIGO NA ABIRIA Kwa kuzingatia viwango vya ubora, reli inayojengwa nchini, itakuwa na uwezo wa kupitisha mzigo wa tani kati ya milioni 17 hadi 25 kwa mwaka ikilinganishwa na reli ya sasa inayopitisha tani milioni tano kwa mwaka.

Kuhusu abiria, Mgedzi alisema, kutokana na urefu wa njia za kupishanisha treni, reli hiyo itaweza kusafirisha kiwango kikubwa cha abiria lakini kwa kuanzia itakuwa ikisafirisha abiria wasiopungua milioni 1.2 kwa mwaka. IDADI YA SAFARI DAR-MORO Kwa kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya usafiri, kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kuwepo kwa treni tatu za abiria kama hatua ya mwanzo zitakazokuwa zikienda na kurudi Dar es Salaam na Morogoro kila siku.

Kwa mujibu wa Mgedzi, treni moja ya abiria inaweza kufanya safari zaidi ya 3 au 4 kwa siku kati ya Dar es Salaam na Morogoro, na hivyo kwa siku kunaweza kuwa na safari kati ya tisa hadi kumi na mbili, lakini idadi ya safari itaongezeka kulingana na abiria walivyo wengi. “Unapoanza na kitu kipya, una hatua ya awali ya kuvutia wateja na ili wateja waweze kuvutika unahitaji kutoa huduma ya uhakika, usafiri wa kasi na pasipo kupoteza muda kwa kusimama simama njiani, mambo hayo yatavutia tu wateja,” alieleza Meneja Mradi, Mgedzi.

IDADI YA STESHENI Reli hiyo ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ina stesheni sita, Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro. UHAI WA RELI Imeelezwa kuwa, uhai wa reli baada ya kukamilika na kabla ya kuanza kufanyiwa ukarabati wowote mkubwa, unategemea mifumo yake ilivyo kama madaraja, vyuma vya reli, mifumo ya umeme, pamoja na mifumo ya ishara na mawasiliano.

Akielezea uhai wa reli hiyo ya kisasa, Mgedzi alisema, madaraja ya reli hiyo yana uwezo wa kudumu kwa miaka 100, wakati reli yenyewe ambacho ni chuma kinachokanyagwa na kusuguliwa na tairi la chuma la treni, lina uwezo wa kudumu kwa miaka 40 kabla ya ukarabati. Kuhusu mifumo ya umeme na mawasiliano, alisema inategemea na aina ya mtambo na nyaya zitakazotumika, hivyo reli hiyo ya SGR alisema usanifu wa vitu hivyo bado unaendelea na taarifa za uhai wake zitatolewa baadaye.



Habari leo

We have heard too much of this. We now want to see its reality! Aslo, we want the controvesy about the project financing clearly elaborated. Furthermore, what arrangements are being put in place currently to ensure that this expensive investiment is guaranted of commercial viability.
 
..reli itakapokamilika ndiyo utaweza kuzungumzia maajabu yake.

..kwa sasa hivi mradi upo ktk hatua ya maandalizi ya eneo la ujenzi, pamoja na ku-design miundombinu itakayojengwa.

..mradi utakapokamilika ndipo tutakapoweza kutamka kwa uhakika kama kuna "maajabu" au la.

..
Mradi unajengwa.
 
Tunasifia kipande cha Dar- Moro wakati vipande vingine kuanzia Morogoro na kuendelea HELA hakuna..

Kutwa kutapatapa.. mara Barclays, mara South Africa.. kila mahali Nchi imekuwa kama MATONYA kwa kuomba omba..


Hakuna anayepinga maendeleo, ila kama Nchi lazima ifanye mambo yenye uwezo nayo..

Wenzetu kwenye mpaka infrastructure wanafanya kwa PPP.. sisi kila kitu tunataka kifanyike kwa KODI na MIKOPO, tena mikopo kutoka Commercial Banks yenye riba kubwa..!!

Serikali ifanye yale yenye uwezo nayo na itapata sifa tu.

Kwenye Elimu kumeoza, kwenye Afya hakufai, miradi ya Maji karibu yote imesimama kisa hela zote ni kwenye Reli na ma Flyover.

Unajenga flyover Ubungo, wakati Shekilango, Magomeni na Faya hakuna Flyover au Interchange unakuwa umetatua foleni kivipi??

Kazi ipo.
My friend Kupanga ni kuchagua,co wanachofanya wenzio na wewe ufanye.sisi co wazee wa kudesa.
 
Train ya umeme na umeme hatuna, hilo ni ajabu la tisa.

Mkuu:
Uzoefu unaonyesha kuwa Train za mwendo kasi hutumia umeme kati ya 4800-9000 KW (max. power output) na hii ni kwa wastani wa 19-33 kWh/km.

Aidha kwa engines za wenzetu wa India zenye uwezo wa 3600HP hutumia takriban 2685 kWh.

Hivyo kwa ujumla hiki ni kiasi kidogo sana kutoka kwenye gridi yetu ya taifa ambayo ni zaidi ya 1300 MW.

Hata hivyo Engine za train hizo zitakuwa na back-up diesel/gas turbine engine power generation support.

Usihofu mkuu ondoa shaka mafanikio ni kuthubutu. TANZANIA imeng'oa nanga sasa ni mbele tu.
 
Labda hilo la 120 na 160 km/h
Iyo kweli maajab 120km/h mbwembwe nyingiii wakati speed ya enzi za Soviet Union...
Japan sasa hivi wako kwenye mchakato wa kujenga yenye up to 500km/h na huskii mwembwe ama kweli maskini akipata makalio hulia mbwata mbwata!
 
Muwe macho wenye MABUS wanaotoa huduma Moro - Dar. Baada ya kuanza kazi treni za mwendo kasi itabidi muyaegeshe MABUS yenu. Wafanyakazi watakuwa wanafanya kazi Dar na kuishi Morogoro. Kweli maendeleo ni kitu kingine.
Ndo mnavodanganywa ivo...kabla ya mwendokasi kuanza si mliambiwa kua mtakua mnaenda mjini kutoka mbezi kwa nusu saa tu sasa hivi naona mnatumia robo saa eti?
 
Yah kwa level yetu Africa lazma tujisifu ukilinganisha na nchi zingine.
Yani we una chongo inamuangalia mwenye kengeza unajisifu??
Pumbavu kweli ..waangalie wenye macho mawili ujione how unlucky you are!
 
Kwanini Tazara haifanyi kazi na njia inayopitia kuna malori mengi sana.
Sio Tazara tu mpaka reli ya Kaskazini haifanyi kazi mpaka miti inaota katikati ya reli!
Yani kama izi reli zilizopo tumeshindwa kuzitumia........sasa hiyo mpya ya kazi gani??
 
Iyo kweli maajab 120km/h mbwembwe nyingiii wakati speed ya enzi za Soviet Union...
Japan sasa hivi wako kwenye mchakato wa kujenga yenye up to 500km/h na huskii mwembwe ama kweli maskini akipata makalio hulia mbwata mbwata!

wee achana na Japan, sisi tuangalie tuko wapi kwa sasa na kunakwenda wapi. Kwa sasa hivi engine za reli ya kati zinazotumia diesel maximum speed yake sijui kama inafika 70km/h.... kama tutapata hiyo ya 120 ni ongezeko la asilimia 71....inatosha!
 
hivi vile vichwa vya train vilivyookotwa bandarini wenyewe washavichukua...???
 
Hutawaona majizi chadema wakipongeza kwenye uzi huu, lakini ikikamilika ndio wa kwanza kupanda!

Sasa hivi wako bize kupongeza maendeleo ya nchi zingine ,kenya rwanda, ethiopia marekani etc.
akili yako mbovu, kila kitu kwako kiko kisiasa! uzi mzuri sana uko informative na ni swala la maendeleo ila kakosea kichwa cha uzi wenyewe labda kama nia yake ilikuwa ni kuteka hadhira pana zaidi, maana siku hizi kuna mbinu nyingi. Ila wewe acha upimbi walioupenda uzi na kubonya kitufe ni watanzania wa mielekeo tofauti ya kisiasa nikiwemo mimi.
 
Tunasifia kipande cha Dar- Moro wakati vipande vingine kuanzia Morogoro na kuendelea HELA hakuna..

Kutwa kutapatapa.. mara Barclays, mara South Africa.. kila mahali Nchi imekuwa kama MATONYA kwa kuomba omba..


Hakuna anayepinga maendeleo, ila kama Nchi lazima ifanye mambo yenye uwezo nayo..

Wenzetu kwenye mpaka infrastructure wanafanya kwa PPP.. sisi kila kitu tunataka kifanyike kwa KODI na MIKOPO, tena mikopo kutoka Commercial Banks yenye riba kubwa..!!

Serikali ifanye yale yenye uwezo nayo na itapata sifa tu.

Kwenye Elimu kumeoza, kwenye Afya hakufai, miradi ya Maji karibu yote imesimama kisa hela zote ni kwenye Reli na ma Flyover.

Unajenga flyover Ubungo, wakati Shekilango, Magomeni na Faya hakuna Flyover au Interchange unakuwa umetatua foleni kivipi??

Kazi ipo.
Eti na wewe ni great thinker!!!
 
Hutawaona majizi chadema wakipongeza kwenye uzi huu, lakini ikikamilika ndio wa kwanza kupanda!

Sasa hivi wako bize kupongeza maendeleo ya nchi zingine ,kenya rwanda, ethiopia marekani etc.

Kwani wewe unapowalipia watoto wako ada za shule unahitaji jirani wakupongeze?Kutimiza wajibu hakuhitaji pongezi. Na hao Chadema wamekuibia mkeo? Umesahau kuweka mawasiliano.
 
Iyo kweli maajab 120km/h mbwembwe nyingiii wakati speed ya enzi za Soviet Union...
Japan sasa hivi wako kwenye mchakato wa kujenga yenye up to 500km/h na huskii mwembwe ama kweli maskini akipata makalio hulia mbwata mbwata!
Mimi katika hili bado nasubiri mkuu,
 
Mkuu:
Sidhani kama itakuwa sahihi kama unavyo andika. Mfano hai ni reli ya jirani zetu Kenya, (Mombasa-Nairobi)
Wasafirishaji wa mabasi wamepata pigo sana kufikia baadhi yao kufunga biashara ktk njia hiyo.
Kiuhalisia siku zote gharama za treni ni ndogo ikilinganishwa na mabasi na si hivyo tu treni yetu sisi itakuwa ya umeme hivyo tutegemee gharama kuwa chini zaidi ya hayo mabasi yanayo tumia mafuta ya diesel.
Hata hivyo ni rahisi kuanzisha treni maalumu kwa huduma za wasafiri wa vituo vya njiani (loops) ili kukidhi mahitaji ya soko la usafirishaji.

..hoja yangu ni kwamba mabasi yatahudumia maeneo/miji ambayo treni haifiki.

..vilevile mabasi yatahudumu wakati / muda ambao treni hazitoi huduma.

..Lakini pia nakubaliana na wewe kuwa biashara ya mabasi kwa yale maeneo ambayo treni inayafikia itaathirika kwa kiwango kikubwa.
 
Wasiwasi wangu ni kwamba hyo phase one itachukua miaka zaidi ya saba kukamilika,muda utaongea
 
Yaani unasema reli ya km 200 ni maajabu! Kweli tembea uone! Hii akili ya kimaskini sijui inatokea wapi, ! Why nchi za kimaskini zikifanya jambo zinaona ni big deals? Kujenga km 200 au hata 2000 siyo jambo la kujipongeza kihivyo! Ni kama ww una marafiki zako watano wote mko broke sasa ukipata laki unaona maajabu! Wakati anaother group they just made a billion dollar wala hawaoni maajabu, haya mambo ya kusifiana utafikiri tumekuwa developed country tuache tunasifia ujinga
 
Back
Top Bottom