Maajabu nane ya Reli mpya ya Dar - Moro

Maajabu nane ya Reli mpya ya Dar - Moro

Tunasifia kipande cha Dar- Moro wakati vipande vingine kuanzia Morogoro na kuendelea HELA hakuna..

Kutwa kutapatapa.. mara Barclays, mara South Africa.. kila mahali Nchi imekuwa kama MATONYA kwa kuomba omba..


Hakuna anayepinga maendeleo, ila kama Nchi lazima ifanye mambo yenye uwezo nayo..

Wenzetu kwenye mpaka infrastructure wanafanya kwa PPP.. sisi kila kitu tunataka kifanyike kwa KODI na MIKOPO, tena mikopo kutoka Commercial Banks yenye riba kubwa..!!

Serikali ifanye yale yenye uwezo nayo na itapata sifa tu.

Kwenye Elimu kumeoza, kwenye Afya hakufai, miradi ya Maji karibu yote imesimama kisa hela zote ni kwenye Reli na ma Flyover.

Unajenga flyover Ubungo, wakati Shekilango, Magomeni na Faya hakuna Flyover au Interchange unakuwa umetatua foleni kivipi??

Kazi ipo.
Serekari yetu haitaki wakosoaji kama wewe jihadhari na white Nissan itakufuatilia
 
Siyo sehemu ni karibu kote. Ukiondoa kwenye madaraja na kwenye station ambapo ndipo TAZARA imetumia mataaluma ya magogo, sehemu nuingine zote imetumia zege. Hadi nguzo za kupitishia nyaya za simu kutoka Dar hadi New Kapir ni zege
Kuna mataaluma ya zege au mbao yanapitisha treni ninauliza nieleweshwe
 
Ukienda Uchina na nchi nyingine, train zake zina mwendo kasi wa 300kph na rail zake ziko mbili sambamba hakuna sehemu maalum ya kupishana. Kwa kuwa ni mwanzo speed ya 160kph inafaa, kakini kwa reli tutakazojenga mbeleni tulione hilo la improvement japo hela ndio kikwazo kikubwa
 
Tunaweka mambo sawa kwa ajiri ya wanyonyaji huku sisi tukiambulia vijineno tu vya hovyo, sitasahau mbwembwe zilizokuwepo wakati wa ujio wa digital. Na sitakaa nisahau tulivyohadaiwa sana na mambo ya gas, tuliaminishwa mengi sana as i f Tanzania ingegeuka kuwa kama paradiso. Yanayoendelea sahivi sote tunayaona, gesi ilishuka kwa si zaidi ya sh2000 lakini ukirejea zile tambo utabaki unajiuliza yako wapi yale yote tuliyokuwa tukihadithiwa
 
Hutawaona majizi chadema wakipongeza kwenye uzi huu, lakini ikikamilika ndio wa kwanza kupanda!

Sasa hivi wako bize kupongeza maendeleo ya nchi zingine ,kenya rwanda, ethiopia marekani etc.
Kwani wanaojengewa hiyo reli ni wanacdm hadi wapongeze? Nyakati nyingine tumia kichwa kufikiri badala ya makalio muda wote! Jiulize 50+ years mlikuwa busy na kujenga himaya ya ccm tu?
 
Muwe macho wenye MABUS wanaotoa huduma Moro - Dar. Baada ya kuanza kazi treni za mwendo kasi itabidi muyaegeshe MABUS yenu. Wafanyakazi watakuwa wanafanya kazi Dar na kuishi Morogoro. Kweli maendeleo ni kitu kingine.
Sasa wale wakazi wa mlandizi chalinze bwawani ubena zomoni mikese nk hiyo sgr yako itawahusu vipi? Saa ingine hata kama huna ubongo wa kufikiria unaweza kuazima kwa kuku au bata
 
Taruma za zege zipo kwenye reli ya TAZARA kwa hiyo hilo siyo ajabu, ila habari imekolezwa

Tuna kawaida ya kudharau matengenezo na marekebisho ya mara kwa mara kwa kisingizio cha "mbona inafanya kazi" je tumejipanga vipi kuhakikisha usalama wa watakao tumia njia hiyo, na je litokeapo jamba tumejipanga namna gani kuhakikisha huduma zinaenedelea kuwepo badala ya kukimbilia kusema "kila jambo lina changamoto"
 
Siyo sehemu ni karibu kote. Ukiondoa kwenye madaraja na kwenye station ambapo ndipo TAZARA imetumia mataaluma ya magogo, sehemu nuingine zote imetumia zege. Hadi nguzo za kupitishia nyaya za simu kutoka Dar hadi New Kapir ni zege


Mwandishi hajawahiona hiyo kitu, kwake imekuwa ni ajabu, sijui akienda akatazama yale mahandaki na madaraja ya nguzo moja, treni inaishia kwenye handaki inaibukia kwenye daraja sijui atasemaje
 
Hutawaona majizi chadema wakipongeza kwenye uzi huu, lakini ikikamilika ndio wa kwanza kupanda!

Sasa hivi wako bize kupongeza maendeleo ya nchi zingine ,kenya rwanda, ethiopia marekani etc.
Majizi ya CDM yakiongozwa na Bwana Mkubwa ... Chenge na wenzao kibao.
 
RELI ya Kisasa (SGR) inayojengwa hapa nchini imeelezwa kuwa ni reli bora kuliko zote Afrika. Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), ilianza awamu ya kwanza ya ujenzi Mei, 2017 na inajengwa na Kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi kwa ubia na Kampuni ya Mota-Engil Africa ya Ureno.

Awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ina urefu wa Kilomita 205 zikiwemo Kilomita 95 za njia za kupishania treni na kufanya reli kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kuwa na urefu wa Kilomita 300. Akizungumza na gazeti hili, Meneja wa Mradi huo kutoka Rahco, Maizo Mgedzi alisema ubora wa reli ya kisasa inayojengwa Tanzania uko juu ikilinganishwa na ubora wa reli zilizojengwa kwenye baadhi ya nchi Barani Afrika.

Mgedzi, alizitaja baadhi ya nchi Barani Afrika ambazo zimejenga reli ya SGR kuwa ni pamoja na Ethiopia, Afrika Kusini, Kenya na Morocco. Alisema, reli zilizojengwa kwenye nchi hizo zina uwezo wa kupitisha treni zenye uwezo wa mwendokasi wa kilomita 120 tu kwa saa tofauti na reli inayojengwa nchini ya kupitisha treni za uwezo wa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

“Lakini pia reli tunayoijenga itatumia treni za umeme tofauti na nchi nyingine nyingi ambazo treni zao zinatumia mafuta ya dizeli. Ethiopia wanajenga reli ya kutumia umeme na kipande kidogo cha reli ya abiria Johannesburg, Afrika Kusini nacho kinatumia umeme,” alisema. “Pia sisi tunajenga reli yenye uwezo wa kupishanisha treni zenye urefu wa kilomita mbili tofauti na nchi nyingine ambazo treni zao hazizidi kilomita moja; Viwango vya ubora wa reli tunayojenga Tanzania viko juu kuliko nchi nyingine,”alieleza Meneja wa Mradi, Mgedzi.

MATALUMA NA UPANA WA RELI Kwa kuzingatia ubora na uimara wa reli hiyo, serikali imeamua kujenga reli hiyo kwa kutumia mataluma ya zege na si ya chuma kama kwenye reli ya zamani ambayo inatumika mpaka sasa. Imeelezwa kuwa, reli inayojengwa kwa mataluma ya chuma ina uwezo mdogo zaidi ikilinganishwa na reli inayojengwa kwa mataluma ya zege.

Akifafanua faida ya kutumia mataluma ya zege kwenye ujenzi wa reli ya kisasa unaoendelea, Mgedzi alisema, mataluma ya zegeyataiwezesha reli inayojengwa kubeba mzigo wenye uzito mkubwa zaidi wa hadi tani 35 kwa ekseli tofauti na reli iliyopo sasa iliyojengwa kwa mataluma ya chuma ambayo haiwezi kuchukua mzigo mzito zaidi unaozidi tani 14 kwa ekseli.

Mgedzi alisema, mataluma ya zege yana uwezo wa kuhimili mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa kwa treni ya abiria na mwendokasi wa kilomita 120 kwa saa kwa treni za mizigo tofauti na treni ya sasa inayotumia mataluma ya chuma na mwendokasi wa kilomita 70 kwa saa. Kuhusu upana wa reli hiyo ya kisasa, mtaalamu huyo alisema itakuwa na upana wa milimita 1,435 ambao ni sawa na upana wa mita 1.435 tofauti na reli ya sasa yenye upana wa milimita 1,000 ambao ni sawa na upana wa mita moja.

“Upana mkubwa wa reli tunayoijenga sasa utaiwezesha treni inayotembea juu ya reli kuwa imara, kwenda kwa kasi na kuwa salama zaidi. Kwa hiyo reli tunayojenga ina upana wa milimita 435 zaidi ya reli inayotumika sasa.” “Na tunaposema ‘gauge’ maana yake ni upana wa reli.

Reli ina miguu miwili, yaani kulia na kushoto ambayo imeshikwa na mataluma, kwa hiyo upana kati ya reli moja na nyingine unaitwa ‘gauge,’” alifafanua Meneja Mgedzi. UWEZO WA KUBEBA MIZIGO NA ABIRIA Kwa kuzingatia viwango vya ubora, reli inayojengwa nchini, itakuwa na uwezo wa kupitisha mzigo wa tani kati ya milioni 17 hadi 25 kwa mwaka ikilinganishwa na reli ya sasa inayopitisha tani milioni tano kwa mwaka.

Kuhusu abiria, Mgedzi alisema, kutokana na urefu wa njia za kupishanisha treni, reli hiyo itaweza kusafirisha kiwango kikubwa cha abiria lakini kwa kuanzia itakuwa ikisafirisha abiria wasiopungua milioni 1.2 kwa mwaka. IDADI YA SAFARI DAR-MORO Kwa kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya usafiri, kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kuwepo kwa treni tatu za abiria kama hatua ya mwanzo zitakazokuwa zikienda na kurudi Dar es Salaam na Morogoro kila siku.

Kwa mujibu wa Mgedzi, treni moja ya abiria inaweza kufanya safari zaidi ya 3 au 4 kwa siku kati ya Dar es Salaam na Morogoro, na hivyo kwa siku kunaweza kuwa na safari kati ya tisa hadi kumi na mbili, lakini idadi ya safari itaongezeka kulingana na abiria walivyo wengi. “Unapoanza na kitu kipya, una hatua ya awali ya kuvutia wateja na ili wateja waweze kuvutika unahitaji kutoa huduma ya uhakika, usafiri wa kasi na pasipo kupoteza muda kwa kusimama simama njiani, mambo hayo yatavutia tu wateja,” alieleza Meneja Mradi, Mgedzi.

IDADI YA STESHENI Reli hiyo ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ina stesheni sita, Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro. UHAI WA RELI Imeelezwa kuwa, uhai wa reli baada ya kukamilika na kabla ya kuanza kufanyiwa ukarabati wowote mkubwa, unategemea mifumo yake ilivyo kama madaraja, vyuma vya reli, mifumo ya umeme, pamoja na mifumo ya ishara na mawasiliano.

Akielezea uhai wa reli hiyo ya kisasa, Mgedzi alisema, madaraja ya reli hiyo yana uwezo wa kudumu kwa miaka 100, wakati reli yenyewe ambacho ni chuma kinachokanyagwa na kusuguliwa na tairi la chuma la treni, lina uwezo wa kudumu kwa miaka 40 kabla ya ukarabati. Kuhusu mifumo ya umeme na mawasiliano, alisema inategemea na aina ya mtambo na nyaya zitakazotumika, hivyo reli hiyo ya SGR alisema usanifu wa vitu hivyo bado unaendelea na taarifa za uhai wake zitatolewa baadaye.

Habari leo
Mkuu hichi kichwa cha habari sijakifahamu..., wewe mtanzania mwenye asili ya kihindi au umekusudia kuandika "Maajabu MANANE reli mpya ya Dar -Moro"
 
Hutawaona majizi chadema wakipongeza kwenye uzi huu, lakini ikikamilika ndio wa kwanza kupanda!

Sasa hivi wako bize kupongeza maendeleo ya nchi zingine ,kenya rwanda, ethiopia marekani etc.
kwani yule mzee alienda ikulu bado ni fisadi?
 
Ulisikia kutoka kwa nani?Kama ulisikia kupitia taarifa ya serikali weka source sio kuleta habari za kusikia.
Una undugu na mtulia nini mkuu!?
Mimi sielewi na najua hili ni jukwaa la wajuzi wa mambo na daima wanatoaga majibu, kama huna jibu basi subiri wajuzi wa mambo waje.
 
Tunasifia kipande cha Dar- Moro wakati vipande vingine kuanzia Morogoro na kuendelea HELA hakuna..

Kutwa kutapatapa.. mara Barclays, mara South Africa.. kila mahali Nchi imekuwa kama MATONYA kwa kuomba omba..


Hakuna anayepinga maendeleo, ila kama Nchi lazima ifanye mambo yenye uwezo nayo..

Wenzetu kwenye mpaka infrastructure wanafanya kwa PPP.. sisi kila kitu tunataka kifanyike kwa KODI na MIKOPO, tena mikopo kutoka Commercial Banks yenye riba kubwa..!!

Serikali ifanye yale yenye uwezo nayo na itapata sifa tu.

Kwenye Elimu kumeoza, kwenye Afya hakufai, miradi ya Maji karibu yote imesimama kisa hela zote ni kwenye Reli na ma Flyover.

Unajenga flyover Ubungo, wakati Shekilango, Magomeni na Faya hakuna Flyover au Interchange unakuwa umetatua foleni kivipi??

Kazi ipo.
Jinyonge au hamia kwenu burundi
 
Vipi, nasikia na flyover ya Ubungo michoro imebadilika baada ya kugundua kuwa designers wa mwanzo wali overestimate kiasi cha magari yatakayopita. Ni kweli!?
Muulize Mange sijui ndiyo karibu wenu mpya? Akili hakuna kabisa.
 
Hutawaona majizi chadema wakipongeza kwenye uzi huu, lakini ikikamilika ndio wa kwanza kupanda!

Sasa hivi wako bize kupongeza maendeleo ya nchi zingine ,kenya rwanda, ethiopia marekani etc.
Wasukuma ni washamba sana.hasa kwa wanawake weupee.kariukiii
 
Back
Top Bottom