Maajabu nane ya Reli mpya ya Dar - Moro

Maajabu nane ya Reli mpya ya Dar - Moro

Tunasifia kipande cha Dar- Moro wakati vipande vingine kuanzia Morogoro na kuendelea HELA hakuna..

Kutwa kutapatapa.. mara Barclays, mara South Africa.. kila mahali Nchi imekuwa kama MATONYA kwa kuomba omba..


Hakuna anayepinga maendeleo, ila kama Nchi lazima ifanye mambo yenye uwezo nayo..

Wenzetu kwenye mpaka infrastructure wanafanya kwa PPP.. sisi kila kitu tunataka kifanyike kwa KODI na MIKOPO, tena mikopo kutoka Commercial Banks yenye riba kubwa..!!

Serikali ifanye yale yenye uwezo nayo na itapata sifa tu.

Kwenye Elimu kumeoza, kwenye Afya hakufai, miradi ya Maji karibu yote imesimama kisa hela zote ni kwenye Reli na ma Flyover.

Unajenga flyover Ubungo, wakati Shekilango, Magomeni na Faya hakuna Flyover au Interchange unakuwa umetatua foleni kivipi??

Kazi ipo.
Ungeuliza nini kinaendelea badala ya kulalamika.
FYI kipande cha kutoka Moro hadi Makutopora (Dodoma) tayari mkatabata umeshasainiwa na mkandarasi ameshalipwa malipo ya awali ili aanze kazi mara moja.
 
Miaka 7? una uhakika? Sasa hivi ujenzi umefikia kiwango gani?

..sasa hivi wanaandaa eneo la ujenzi.

..pia wanaandaa michoro ya miundombinu ya reli.

..hizi ni hatua za mwanzo, ujenzi bado haujaanza.
 
. Mgedzi, alizitaja baadhi ya nchi Barani Afrika ambazo zimejenga reli ya SGR kuwa ni pamoja na Ethiopia, Afrika Kusini, Kenya na Morocco. “Lakini pia reli tunayoijenga itatumia treni za umeme tofauti na nchi nyingine nyingi ambazo treni zao zinatumia mafuta ya dizeli.

Uongo mkubwa! Umeshatoa mifano ya SGR ya thiopia, Afrika Kusini, Kenya na Morocco, halafu unasema sie ni tofauti tutatumia umeme. SGR Kenya Mombasa- Nairobi sio ya umeme? SGR South Africa sio umeme? SGR Ethiopia - Djibout sio umeme? SGR Morrocoo sio umeme?

Sasa ni nani kati ya uliotaja kuwa na SGR lakini hawatumii umeme kama sisi tutakavyofanya? Watu wengine wanaongea mbofu mbofu sana.
 
Mkuu:
Uzoefu unaonyesha kuwa Train za mwendo kasi hutumia umeme kati ya 4800-9000 KW (max. power output) na hii ni kwa wastani wa 19-33 kWh/km.

Aidha kwa engines za wenzetu wa India zenye uwezo wa 3600HP hutumia takriban 2685 kWh.

Hivyo kwa ujumla hiki ni kiasi kidogo sana kutoka kwenye gridi yetu ya taifa ambayo ni zaidi ya 1300 MW.

Hata hivyo Engine za train hizo zitakuwa na back-up diesel/gas turbine engine power generation support.

Usihofu mkuu ondoa shaka mafanikio ni kuthubutu. TANZANIA imeng'oa nanga sasa ni mbele tu.
Basi sawa.
 
..sasa hivi wanaandaa eneo la ujenzi.

..pia wanaandaa michoro ya miundombinu ya reli.

..hizi ni hatua za mwanzo, ujenzi bado haujaanza.
Taarifa yako siyo ya kweli ndugu, tafuta ukweli kwa watu wakweli ili ujue ukweli.
 
Taarifa yako siyo ya kweli ndugu, tafuta ukweli kwa watu wakweli ili ujue ukweli.

..mkandarasi ndiyo huyohuyo unayesanifu mradi.

..kama reli imeanza kujengwa tueleze basi wamefika wapi sasa hivi.

..Kilomita ngapi za mradi zimeshakamilishwa?Stesheni[vituo] ngapi zimeshajengwa?
 
..mkandarasi ndiyo huyohuyo unayesanifu mradi.

..kama reli imeanza kujengwa tueleze basi wamefika wapi sasa hivi.

..Kilomita ngapi za mradi zimeshakamilishwa. Vituo vingapi vimeshajengwa.
Haya bhana, hatubishani!
But elewa kabla ya kuona hivyo vituo na reli yenyewe kuna several stages ambazo ni lazima zifanyike kwanza, otherwise huwezi jenga reli hewani kama zilivyo mbingu!
Acheni watu wafanye kazi yao.
 
wee achana na Japan, sisi tuangalie tuko wapi kwa sasa na kunakwenda wapi. Kwa sasa hivi engine za reli ya kati zinazotumia diesel maximum speed yake sijui kama inafika 70km/h.... kama tutapata hiyo ya 120 ni ongezeko la asilimia 71....inatosha!
Tuachane na Japan tuangalie Rwanda sio? Ndo akili yako inavyokutuma
 
Haya bhana, hatubishani!
But elewa kabla ya kuona hivyo vituo na reli yenyewe kuna several stages ambazo ni lazima zifanyike kwanza, otherwise huwezi jenga reli hewani kama zilivyo mbingu!
Acheni watu wafanye kazi yao.

..kama ni hivyo basi tunazungumza kitu kimoja.

..mimi hoja yangu ni kwamba mradi uko ktk hatua za awali sana, tuwe na subira mpaka mradi huu utakapofikia hatua za matokeo ambapo tunaona mataruma yametandazwa, stesheni zimekamilika, engine za treni zinafanyiwa majaribio, then tunaweza kuzungumzia " maajabu " ya reli yetu.
 
Aliye juu mngoje chini....Utangoja sana Mkuu na utakufa bila kelele kama walivokufa wafuasi wa kibwetere sio maneno yangu ayo ni maneno ya Prof Jay kwnye Chemsha Bongo
Unajua nasubiri nini?
Na kwanini nasubiri?
Hata kama usipo subiri nini kitabadilika?
Kwa maneno yako naona wewe utakua umempandia huko huko juu, utakua unyota ya bashite.
 
RELI ya Kisasa (SGR) inayojengwa hapa nchini imeelezwa kuwa ni reli bora kuliko zote Afrika. Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), ilianza awamu ya kwanza ya ujenzi Mei, 2017 na inajengwa na Kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi kwa ubia na Kampuni ya Mota-Engil Africa ya Ureno.

Awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ina urefu wa Kilomita 205 zikiwemo Kilomita 95 za njia za kupishania treni na kufanya reli kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kuwa na urefu wa Kilomita 300. Akizungumza na gazeti hili, Meneja wa Mradi huo kutoka Rahco, Maizo Mgedzi alisema ubora wa reli ya kisasa inayojengwa Tanzania uko juu ikilinganishwa na ubora wa reli zilizojengwa kwenye baadhi ya nchi Barani Afrika.

Mgedzi, alizitaja baadhi ya nchi Barani Afrika ambazo zimejenga reli ya SGR kuwa ni pamoja na Ethiopia, Afrika Kusini, Kenya na Morocco. Alisema, reli zilizojengwa kwenye nchi hizo zina uwezo wa kupitisha treni zenye uwezo wa mwendokasi wa kilomita 120 tu kwa saa tofauti na reli inayojengwa nchini ya kupitisha treni za uwezo wa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

“Lakini pia reli tunayoijenga itatumia treni za umeme tofauti na nchi nyingine nyingi ambazo treni zao zinatumia mafuta ya dizeli. Ethiopia wanajenga reli ya kutumia umeme na kipande kidogo cha reli ya abiria Johannesburg, Afrika Kusini nacho kinatumia umeme,” alisema. “Pia sisi tunajenga reli yenye uwezo wa kupishanisha treni zenye urefu wa kilomita mbili tofauti na nchi nyingine ambazo treni zao hazizidi kilomita moja; Viwango vya ubora wa reli tunayojenga Tanzania viko juu kuliko nchi nyingine,”alieleza Meneja wa Mradi, Mgedzi.

MATALUMA NA UPANA WA RELI Kwa kuzingatia ubora na uimara wa reli hiyo, serikali imeamua kujenga reli hiyo kwa kutumia mataluma ya zege na si ya chuma kama kwenye reli ya zamani ambayo inatumika mpaka sasa. Imeelezwa kuwa, reli inayojengwa kwa mataluma ya chuma ina uwezo mdogo zaidi ikilinganishwa na reli inayojengwa kwa mataluma ya zege.

Akifafanua faida ya kutumia mataluma ya zege kwenye ujenzi wa reli ya kisasa unaoendelea, Mgedzi alisema, mataluma ya zegeyataiwezesha reli inayojengwa kubeba mzigo wenye uzito mkubwa zaidi wa hadi tani 35 kwa ekseli tofauti na reli iliyopo sasa iliyojengwa kwa mataluma ya chuma ambayo haiwezi kuchukua mzigo mzito zaidi unaozidi tani 14 kwa ekseli.

Mgedzi alisema, mataluma ya zege yana uwezo wa kuhimili mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa kwa treni ya abiria na mwendokasi wa kilomita 120 kwa saa kwa treni za mizigo tofauti na treni ya sasa inayotumia mataluma ya chuma na mwendokasi wa kilomita 70 kwa saa. Kuhusu upana wa reli hiyo ya kisasa, mtaalamu huyo alisema itakuwa na upana wa milimita 1,435 ambao ni sawa na upana wa mita 1.435 tofauti na reli ya sasa yenye upana wa milimita 1,000 ambao ni sawa na upana wa mita moja.

“Upana mkubwa wa reli tunayoijenga sasa utaiwezesha treni inayotembea juu ya reli kuwa imara, kwenda kwa kasi na kuwa salama zaidi. Kwa hiyo reli tunayojenga ina upana wa milimita 435 zaidi ya reli inayotumika sasa.” “Na tunaposema ‘gauge’ maana yake ni upana wa reli.

Reli ina miguu miwili, yaani kulia na kushoto ambayo imeshikwa na mataluma, kwa hiyo upana kati ya reli moja na nyingine unaitwa ‘gauge,’” alifafanua Meneja Mgedzi. UWEZO WA KUBEBA MIZIGO NA ABIRIA Kwa kuzingatia viwango vya ubora, reli inayojengwa nchini, itakuwa na uwezo wa kupitisha mzigo wa tani kati ya milioni 17 hadi 25 kwa mwaka ikilinganishwa na reli ya sasa inayopitisha tani milioni tano kwa mwaka.

Kuhusu abiria, Mgedzi alisema, kutokana na urefu wa njia za kupishanisha treni, reli hiyo itaweza kusafirisha kiwango kikubwa cha abiria lakini kwa kuanzia itakuwa ikisafirisha abiria wasiopungua milioni 1.2 kwa mwaka. IDADI YA SAFARI DAR-MORO Kwa kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya usafiri, kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kuwepo kwa treni tatu za abiria kama hatua ya mwanzo zitakazokuwa zikienda na kurudi Dar es Salaam na Morogoro kila siku.

Kwa mujibu wa Mgedzi, treni moja ya abiria inaweza kufanya safari zaidi ya 3 au 4 kwa siku kati ya Dar es Salaam na Morogoro, na hivyo kwa siku kunaweza kuwa na safari kati ya tisa hadi kumi na mbili, lakini idadi ya safari itaongezeka kulingana na abiria walivyo wengi. “Unapoanza na kitu kipya, una hatua ya awali ya kuvutia wateja na ili wateja waweze kuvutika unahitaji kutoa huduma ya uhakika, usafiri wa kasi na pasipo kupoteza muda kwa kusimama simama njiani, mambo hayo yatavutia tu wateja,” alieleza Meneja Mradi, Mgedzi.

IDADI YA STESHENI Reli hiyo ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ina stesheni sita, Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro. UHAI WA RELI Imeelezwa kuwa, uhai wa reli baada ya kukamilika na kabla ya kuanza kufanyiwa ukarabati wowote mkubwa, unategemea mifumo yake ilivyo kama madaraja, vyuma vya reli, mifumo ya umeme, pamoja na mifumo ya ishara na mawasiliano.

Akielezea uhai wa reli hiyo ya kisasa, Mgedzi alisema, madaraja ya reli hiyo yana uwezo wa kudumu kwa miaka 100, wakati reli yenyewe ambacho ni chuma kinachokanyagwa na kusuguliwa na tairi la chuma la treni, lina uwezo wa kudumu kwa miaka 40 kabla ya ukarabati. Kuhusu mifumo ya umeme na mawasiliano, alisema inategemea na aina ya mtambo na nyaya zitakazotumika, hivyo reli hiyo ya SGR alisema usanifu wa vitu hivyo bado unaendelea na taarifa za uhai wake zitatolewa baadaye.

Habari leo
Kwahiyo injini na mabehewa vitakuwa maalum kwa Tanzania tu! Hii inamaana ni spesho oda kwa Tanzania!!!! Hatujaenda shule lakini pia si vizuri kutumia ujinga wetu kutudanganya. Urefu mkubwa wa kilomita hivi ndiyo unaothibitisha treni inayotumia umeme kuwa inatumia umeme kuliko ile ya kilomita mbili? Siasa hata tunapopika mrenda! Meneja wa kampuni ya reli amesema reli hivyo itafuta kovu la ukoloni, sijui kama ikulu ilijengwa baada ya uhuru, tukiacha hospitali ya Ocean Road na Muhimbili pamoja na MV Liemba, Victoria n.k. siasa siasa kutudangaya tusiosoma, Tazara ilijengea mataluma ya zege miaka ya1970, hivyo si jipya.
 
Back
Top Bottom