Maajabu na vituko vya mnyama fisi

Maajabu na vituko vya mnyama fisi

Hiyo namba vii (8) umesema anapenda kung'ang'ania madaraka au mie sijaelewa, alafu ile ya kuufukuza mkia wake kwa kuuzunguka kama chizi fulani hivi mbona hujaeleza.
Isome vizuri (viii) ...utaelewa, yaani anakula kiubabe sana, harembi kwa ufupi
 
Namba tisa imenifurahisha sana
Bila kupoteza dakika leo naomba nikuonjeshe sifa za mnyama fisi kwa kadri inavyowezekan:

(i)Ugomvi na mmoja wao umenunua ugomvi wa familia nzima.

View attachment 510169View attachment 510175
Wao wana sera kama ya marekani kuwa ukichokoza jimbo lao au taifa lao hasa kwenye maslahi yao basi wewe umetangaza vita na marekani nzima. Hivyo hivyo kwa fisi , akichokozwa mmoja au wawili na wababe wa mwituni kama nyati , simba, chui, basi fisi huyo hukimbia mbio za marathoni na kwenda kuita nyomi ya familia nzima na ndani ya dakika 3 utaona kuanzia babu, bibi, kaka dada, mama, baba ,shangazi wa ukoo, mjomba , mjukuu ,kilembwe na hivyo kupelekea kuwa mtiti wa familia nzima. Kwahiyo kama wako 180 kwa familia yao basi watakuja wote front line bila kujali kuna mgonjwa, mjamzito au mzee/kikongwe katika familia hiyo.


(ii) Hutenga cha kula cha watoto wao pembeni.

View attachment 510176
View attachment 510177
Fisi hata wawe na njaa kama ya mwana siasa , hata siku moja huwezi ona kala msosi wa mwanae, kwani wao wakipata kitoweo chao cha siku ni lazima watenge kwanza pembeni chakula kitachotumiwa na watoto wao.
Kwahiyo wakipiga pafu zao wakamaliza , watoto huwa na uhakika wa msosi wao kwani hauchanganywi na wa wakubwa wao. Mkubwa ukijichanganya kukidokoa kwa namna yoyote ile , basi sharia itafuata mkondo wake.
Hali hiyo hupelekea Watoto wa fisi kuwa mashavu dodo kila siku , na fisi mtoto kutamania aendelee kuwa mtoto kila siku (Kumbuka Lady Jdee aliimba…Natamani kuwa malaika…natamani kuwa kama mtoto…) fisi wakubwa hasa wale wazee huwa wakisikia wimbo huu hupata simanzi sana.

(iii)Hamna kushindwa kwenye mapambano (tifu).

Miongoni mwa sharia yao ni kama ya kina Mura kuwa panga au jambia likitolewa kiunoni basi hakuna kushuka chini bila kurudi na damu (usije kwenda kumbembeleza mura asamehe anaweza kukufyeka wewe mwenyewe uliyejipendekeza).

Hata kwa fisi ni hivyo , hivyo, hawana falasafa ya kushindwa vita au mapigano. Wao mtiti ukianza mtapigana mpaka ushindi upatikane ndo watakubali kusepa. Vinginevyo ligi itakuwa ndefu mpaka kuchee. kushindwa kwao ni kurudi nyuma kujipanga.

(iv)Fisi Wana uwezo mkubwa wa kunusa na kuhisi.

Miongoni mwa wanyama waliojaaliwa uwezo mkubwa wa kunusa an kuhisi kitu ni pamoja na fisi.
Fisi anaweza kuchezwa na machale kiasi cha kumjua mnyama mgonjwa au mweney afya mgogoro miongoni mwa wanyama wengi. Mfano wanaweza kujua simba mzee au mgonjwa yukoje katika kundi la simba , au Nyumbu boya boya kuliko wote katika kundi la Nyumbu. Na hivyo huwasaidia kufanya kazi yao ya kuwinda kuwa nyepesi kama kuokota dodo chini cha mchongoma.

(v) Harufu ya damu ndio mzuka wao hupanda mara dufu.

View attachment 510191

Kama ilivyo kwenye kikosi cha mizinga , milio makombora au mizinga yao ndiyo huwapandisha mizuka wazee wa kikosi cha mizinga au masai akipandishwa mori baada ya nyongo kutamalaki kichwani , basi ndipo nae huruka sama huku akiwa kachachamaa(weka mbali na watoto).

Basi na kwa fisi hali ni hiyo hiyo, ingawa wao hupandwa sana na mzuka wa kazi pale wanapoona damu imetapakaa kwa kiumbe husika. Yaani hapo afe beki afe kipa ushindi lazima upatikane. Hivyo ukiwaonesha damu tu ama zao ama zako.

(vi) Hutumia muda mfupi sana kulana mzigo (kula papuchi).
View attachment 510188View attachment 510189

Katika wanyama ambao huwa hawana cha kupoteza wakati wa kula papuchi basi ni fisi, wao fisi dume akibambia manzi basi ni ndani ya dk 5 mchezo umeisha na jamaa huendelea na mishe mishe zake kama kawa.
Huwezi kujua wamekulana saa ngapi, maana hawana kulemba mwandiko wakati wa imla (dictation) au wakati kalamu ni ya kuazima.
Baada ya muda mfupi utaona fisi demu amepigwa mwiba , na kungojea kwenda maternity block muda ukiwadia. Na Pia hulana mzigo kwa siri na kificho sana hasa palipo na watroto wao, siku zote hawataki watoto wao wajue kuwa mshua wao leo kala goma lake (Maza yao kaliwa na mshua).

(vii) Ni mwiko kujipakaza damu wakati na baada ya kula nyama/ kitoweo.

While eating
View attachment 510193

after eating
View attachment 510194

Ni marufuku kujipaka damu wakati wa kula, na atayepatikana na damu wenzie humtafuna.
Hivyo Sharia yao ya kuwa msafi wakati na baada ya kula inazingatiwa na kundi zima au ukoo mzima wa fisi husika. Ukijichanganya ukala nyama afu ukabaki na damu damu kizembe zembe lazima wenzako wakugeuze hasusa na kitoweo cha siku. Kwahiyo, sera ya jipende kabla ya kupendwa na mauti inazingatiwa katika maisha yao yote.

(viii) Ni wanyama wenye pirika pirika na mishe mishe nyingi muda wote.

View attachment 510198View attachment 510203View attachment 510199
Mnyama fisi kupumzika kwake yeye ni mpaka awe mgonjwa au kachoka sana, ila sehemu kubwa ya mai
 
Nitafurahi kuipata hiyo clip...
Shukrani sana mkuu.
Mkuu article Babkubwa, Hahahahahahahaaaaa niliona moja LinkedIn jamaa Anasema defence force yao sio ya Kitoto, mbele kabisaaaa unaambiwa wanatangulizwa Sijui Wazee wale na Watoto, Katikati kuna FFU na Wale Wajeshi wanakua Mwisho kabisaaaa. Ngoja nitafute ile picha kama nitaweza kuikopi niitupie humu
 
Dawa Yao ni Simba jike tu hawamsongelei wakati wa msosi anapokula, akikamata Fisi anaua
 
Ni katika masimulizi mbali mbali na shuhuda za watu.
Hata CCM wanalijua hili.Sina evidence wala fisi ila nasikia wenzetu wa sayansi za Giza wanatumia fisi kama wanavyotumia ungo.
Ungekuwa mahakamani jaji angefunga jalada na kesi inakuwa dismissed
 
Kingine hujamalizia mkuu..fisi hutembea na kusimama kwa miguu miwili kama. Binadamu kwa muda kadhaa..unaweza ukapishana nae kama MSHIKAJI FLAN HIVI kachill sehem..kasimama kumbe FISI
Kuna jamaa alinihadithia kwao Dodoma kuna mtu alimpiga roba fisi hadi kufa

Fisi alikuwa anatembea kwa miguu miwili anatembea pembezoni mwa ukuta ilikuwa usiku walivyokutana jamaa kwa panic akamuwahi roba

Sasa ile hadith yake ninai-confirm
 
Kuna jamaa alinihadithia kwao Dodoma kuna mtu alimpiga roba fisi hadi kufa

Fisi alikuwa anatembea kwa miguu miwili anatembea pembezoni mwa ukuta ilikuwa usiku walivyokutana jamaa kwa panic akamuwahi roba

Sasa ile hadith yake ninai-confirm
Duu.. Hyo kali mkuu..sasa kama jamaa kampiga roba fisi hadi kufa..huyo jamaa sio wa kuchezea..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom