Maajabu na vituko vya mnyama fisi

MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,094
7,225
Bila kupoteza dakika leo naomba nikuonjeshe sifa za mnyama fisi kwa kadri inavyowezekan:

(i)Ugomvi na mmoja wao umenunua ugomvi wa familia nzima.

upload_2017-5-16_17-25-1.jpeg
upload_2017-5-16_17-26-58.jpeg

Wao wana sera kama ya marekani kuwa ukichokoza jimbo lao au taifa lao hasa kwenye maslahi yao basi wewe umetangaza vita na marekani nzima. Hivyo hivyo kwa fisi , akichokozwa mmoja au wawili na wababe wa mwituni kama nyati , simba, chui, basi fisi huyo hukimbia mbio za marathoni na kwenda kuita nyomi ya familia nzima na ndani ya dakika 3 utaona kuanzia babu, bibi, kaka dada, mama, baba ,shangazi wa ukoo, mjomba , mjukuu ,kilembwe na hivyo kupelekea kuwa mtiti wa familia nzima. Kwahiyo kama wako 180 kwa familia yao basi watakuja wote front line bila kujali kuna mgonjwa, mjamzito au mzee/kikongwe katika familia hiyo.


(ii) Hutenga cha kula cha watoto wao pembeni.

upload_2017-5-16_17-28-33.jpeg

upload_2017-5-16_17-29-20.jpeg

Fisi hata wawe na njaa kama ya mwana siasa , hata siku moja huwezi ona kala msosi wa mwanae, kwani wao wakipata kitoweo chao cha siku ni lazima watenge kwanza pembeni chakula kitachotumiwa na watoto wao.
Kwahiyo wakipiga pafu zao wakamaliza , watoto huwa na uhakika wa msosi wao kwani hauchanganywi na wa wakubwa wao. Mkubwa ukijichanganya kukidokoa kwa namna yoyote ile , basi sharia itafuata mkondo wake.
Hali hiyo hupelekea Watoto wa fisi kuwa mashavu dodo kila siku , na fisi mtoto kutamania aendelee kuwa mtoto kila siku (Kumbuka Lady Jdee aliimba…Natamani kuwa malaika…natamani kuwa kama mtoto…) fisi wakubwa hasa wale wazee huwa wakisikia wimbo huu hupata simanzi sana.

(iii)Hamna kushindwa kwenye mapambano (tifu).

Miongoni mwa sharia yao ni kama ya kina Mura kuwa panga au jambia likitolewa kiunoni basi hakuna kushuka chini bila kurudi na damu (usije kwenda kumbembeleza mura asamehe anaweza kukufyeka wewe mwenyewe uliyejipendekeza).

Hata kwa fisi ni hivyo , hivyo, hawana falasafa ya kushindwa vita au mapigano. Wao mtiti ukianza mtapigana mpaka ushindi upatikane ndo watakubali kusepa. Vinginevyo ligi itakuwa ndefu mpaka kuchee. kushindwa kwao ni kurudi nyuma kujipanga.

(iv)Fisi Wana uwezo mkubwa wa kunusa na kuhisi.

Miongoni mwa wanyama waliojaaliwa uwezo mkubwa wa kunusa an kuhisi kitu ni pamoja na fisi.
Fisi anaweza kuchezwa na machale kiasi cha kumjua mnyama mgonjwa au mweney afya mgogoro miongoni mwa wanyama wengi. Mfano wanaweza kujua simba mzee au mgonjwa yukoje katika kundi la simba , au Nyumbu boya boya kuliko wote katika kundi la Nyumbu. Na hivyo huwasaidia kufanya kazi yao ya kuwinda kuwa nyepesi kama kuokota dodo chini cha mchongoma.

(v) Harufu ya damu ndio mzuka wao hupanda mara dufu.

upload_2017-5-16_17-31-35.jpeg


Kama ilivyo kwenye kikosi cha mizinga , milio makombora au mizinga yao ndiyo huwapandisha mizuka wazee wa kikosi cha mizinga au masai akipandishwa mori baada ya nyongo kutamalaki kichwani , basi ndipo nae huruka sama huku akiwa kachachamaa(weka mbali na watoto).

Basi na kwa fisi hali ni hiyo hiyo, ingawa wao hupandwa sana na mzuka wa kazi pale wanapoona damu imetapakaa kwa kiumbe husika. Yaani hapo afe beki afe kipa ushindi lazima upatikane. Hivyo ukiwaonesha damu tu ama zao ama zako.

(vi) Hutumia muda mfupi sana kulana mzigo (kula papuchi).
upload_2017-5-16_17-29-45.jpeg
upload_2017-5-16_17-30-35.jpeg


Katika wanyama ambao huwa hawana cha kupoteza wakati wa kula papuchi basi ni fisi, wao fisi dume akibambia manzi basi ni ndani ya dk 5 mchezo umeisha na jamaa huendelea na mishe mishe zake kama kawa.
Huwezi kujua wamekulana saa ngapi, maana hawana kulemba mwandiko wakati wa imla (dictation) au wakati kalamu ni ya kuazima.
Baada ya muda mfupi utaona fisi demu amepigwa mwiba , na kungojea kwenda maternity block muda ukiwadia. Na Pia hulana mzigo kwa siri na kificho sana hasa palipo na watroto wao, siku zote hawataki watoto wao wajue kuwa mshua wao leo kala goma lake (Maza yao kaliwa na mshua).

(vii) Ni mwiko kujipakaza damu wakati na baada ya kula nyama/ kitoweo.

While eating
upload_2017-5-16_17-32-50.jpeg


after eating
upload_2017-5-16_17-34-1.jpeg


Ni marufuku kujipaka damu wakati wa kula, na atayepatikana na damu wenzie humtafuna.
Hivyo Sharia yao ya kuwa msafi wakati na baada ya kula inazingatiwa na kundi zima au ukoo mzima wa fisi husika. Ukijichanganya ukala nyama afu ukabaki na damu damu kizembe zembe lazima wenzako wakugeuze hasusa na kitoweo cha siku. Kwahiyo, sera ya jipende kabla ya kupendwa na mauti inazingatiwa katika maisha yao yote.

(viii) Ni wanyama wenye pirika pirika na mishe mishe nyingi muda wote.

upload_2017-5-16_17-35-39.jpeg
upload_2017-5-16_17-38-16.jpeg
upload_2017-5-16_17-35-54.jpeg

Mnyama fisi kupumzika kwake yeye ni mpaka awe mgonjwa au kachoka sana, ila sehemu kubwa ya maisha yake ya kila siku ni mnyama mwenye mishe mishe na michakato mia kidogo. Pia ana haraka haraka na kimbele mbele sana katika ufanyaji wake wa mambo.

(ix) Ana wivu na mkono wa binadamu.
upload_2017-5-16_17-37-4.jpeg

Siku zote fisi akimuona mwanadamu anatembea yuko radhi akusindikize huku udenda na umate mate ukimtoka toka kinywani akidhani kuwa kuna muda mkono wako utadondoka na hivyo yeye kupata zari la mentali.

(x) Kanuni yao ya kula ni ya kunyofoa nyofoa nyama au kitoweo husika.
upload_2017-5-16_17-38-59.jpeg
upload_2017-5-16_17-39-13.jpeg
upload_2017-5-16_17-39-46.jpeg

Fisi huwaharembi rembi wakati wa kula, kama panya anavyokuwaga anafanya , kula huku anakupuliza, wao fisi huku sasambua kwa kukunyofoa nyofoa minofu na mifupa mpaka unakwisha. Kwa ufupi wanakula kama wanaume wa kazi au wendawazimu flani.

(xi) Hula huku akicheka cheka na kukenua meno mpaka amalize haja zake.
upload_2017-5-16_17-40-46.jpeg

Katika kitu ambacho huwashangaza hata masela wenzao wa porini ni ile hatua ya fisi kula huku akicheka cheka nakutoa vimilio vya ajabu ajabu kuanzia anaanza kula mpaka amalizapo.
Hiyo mbinu husaidia hata wanyama wengine kubaki wameduwaa pambeni wakishangaa jamaa wanavyogonga menyu kwani hushindwa kung’amua kirahisi kama wanawajadili wao wa pembeni au ndo utamu wenyewe wa msosi.

(xii) Cheza na vyote ila usicheze na watoto wao au kitoweo chao.
upload_2017-5-16_17-44-41.jpeg
upload_2017-5-16_17-45-17.jpeg

Katika kitu ambacho fisi hata kuacha salama ukijichanganya anga zake basi ni kitendo cha wewe kumzengua mwanae au kujifanya una taka kumpiga tukio katika kitoweo chake. Hapo hata kama ni fisi mzembe namna gani, mtapigana mpaka kucheee , akilinda maslahi yake nay a mwanae au kitoweo chake. Wanaweza funga mtaa (mbunga au msitu mzima ) kwa timbwili lake.
 

Attachments

  • upload_2017-5-16_17-34-16.jpeg
    upload_2017-5-16_17-34-16.jpeg
    6.7 KB · Views: 274
Fisi muoga??? Mnyama yeyote n muoga "Kwa maana ya kujilinda na si vinginevyo" akiumia kidogo tu mara nying hua ni n sawa na death sentence, ila sio kwenye njaa, akikosa mnyama wa kuwinda hua wanavamia hata vitoweo vya simba
Yuko Kama binadamu mwenye njaa....hachagui cha kula wala cha kunywa
 
umenifurahisha sana labda niongezee,
fisi jike ni kubwa kuliko dume inavyodhaniwa kwamba jike pia ana uume lakini ule si uume ni kinembe na hudinda kufikia urefu wa zaid ya inch 3.
2.fisi mtoto akizaliwa siku hiyohiyo anaanza kula nyama hii inachagizwa sana na wazani kula mifupa hivyo kuwa na calcium nyingi katika uzao wao!!
3.fisi ni anawinda kwa style inaitwa exhaustion yaani anamchosha mnyama hadi aanguke kisha kumkula!
4.ili fisi ajue sehemu kuna mzoga muda wote macho yake huwa juu juu hadi miguu ya nyuma imekuwa mifupi kwa kuangalia akitegemea kuona ndege Tai au vultures kwa kizungu.
5.katika wanyama wote duniani hakuna mwenye taya ngumu kama fisi kitu kinamfanya aweze kula hadi ngozi na kucha za wanyama,
 
Back
Top Bottom