Maajabu Makubwa - Kuzuia Kilimo cha Umwagiliaji

Acheni ujinga, yaani mna mtetea huyo mchina wenu anaye chota lita milioni 1 kwa saa na kusababisha ma milioni ya waTz kukosa maji, kwa nini asi chimbe kisima chake?? Huo ni uwekezaji au uhalibifu, Sometimes iachieni serikali ifanye yake,
Ebu acheni ujinga, huyo mchina alipaswa ashtakiwe kwa kuhujumu uchumi….,
Sio mchina tu, hata ng'0mbe zote zichinjwe zinakunywa maji mengi na kusababisha upungufu wa maji tanzania.
 
Dah! Hivi huyu jamaa aliishia wapi? Nakumbuka kulikuwa na kesi dhidi ya huu uharibifu, sijui iliishaje.
Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa mkoa wa mtwara baada ya kuharibu mashamba ya Mbowe, nchi ya ajabu sana hii katika sayari ya dunia
 
Siku zote, wananchi wamehamasishwa kufanya kilimo cha umwagiliaji. Ilani za uchaguzi za vyama vyote vya siasa za miaka yote, zinaeleza kama vyama hivyo vikipewa dola jinsi vitakavyoendeleza au vitakavyofanya ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinafanyika kwa ufanisi.

Makongamano, semina mbalimbali zimewahi kufanyika kuhamasisha kilimo cha unwagiliaji. Leo unawaambia wananchi wasifanye kilimo cha umwagiliaji. Hivi nchi hii inaongozwa na watu wa namna gani! Wakiacha kilimo cha umwagiliaji, baada ya miezi michache, tuanze tena kumwomba Mungu akete chakula?

Watanzania tuna laana gani, hadi kupata viongozi wasio na maono? Viongozi ambao, kunapotokea tatizo, badala ya kukaa, kutafakari kuhusisha think tanks, kuona namna bora ya kutatua tatizo bila ya kusababisha matatizo mengine, wanaibuka tu na kutoa kauli - kuanzia leo, hiki au kile marufuku. Very low thinking and leadership ability!

Tatizo la maji na umeme halijasababishwa na upungufu wa mvua wala maji bali kutokana na mipango mibovu ya Serikali. Na mipango mibovu ya Serikali inasababishwa na aina ya watu waliopo serikalini.

Nchi kama Mali, Niger, Guenea, Benin wanategemea mto Niger kama chanzo cha maji ya kutumia majumbani na kama chanzo cha cha uzalishaji umeme wa maji, na nimewahi kukaa mfululizo katika mataifa hayo miezi 6, umeme haukuwahi kukatika hata siku moja.

Kila nchi inayotumia maji ya mto Niger, imejenga mabwawa makubwa ya kutunzia maji, na mabwawa hayo yanajazwa kwa overflows za wakati wa kipindi cha mvua. Sisi wenye mito usiyo na hesabu, na maziwa makubwa, eti tunaongelea upungufu wa maji? Watasemaje Wamisri, watasemaje Walibya, Mali, Ghana, Burkina Faso na mataifa mengine yaliyo karibu na jangwa la Sahara?

Tusipepese macho, ukweli ni kuwa tuna shida ya umeme na maji kutokana na viongozi wasio na maono, mipango wala weledi. Tanzania siyo nchi ya kuzungumzia upungufu wa maji.

Kwa matatizo haya yanayotukumba sasa, na mengine ambayo hatukustahili kuwa nayo, yanatufanya tuzungumzie upungufu wa akili na tatizo la kushindwa kupata viongozi wenye weledi na maono.
Tatizo ni Wanasiasa na sio Wataalamu ndio wapangaji na wasimamizi wakuu wa Project zote za kitaalamu. Kwa hilo “Hatutoboi “ in Mbunge Bwege’s voice.
Halafu uhamasishaji wa watu kupanda miti umeishia wapi?!
 
Mimi kijijini kwetu nimechimba kisima na wala hata milioni mbili haikuisha. Maji ya kutosha miaka yote mpaka majirani wanachota, tena free. Solar siku hizi ni za kumwaga tuu
Basi hiyo ndo suluhisho la mtatizo ya maji na isiwe kijijini tu kama unaishi eneo lako sio la kupanga hata mjini chimba kisima, kwani kisima kinachukua eneo gani si nchi 6 au 8 kwa ku bore na mashine?
 
Sheria zipo zinazohusiana na Uchepusha maji kwaajili ya umwagiliaji.
Yule mchina kama anavyovibali hana kosa lolote japo sheria zimeongela ikitokea kumetokea upungufu wa maji je anapaswa kufanyaje.

Sio tuu umwagiliaji ila hata mto unaokatiza nchi tofauti unazo kanuni zake katika matumizi ya maji ndo mana mnaona kuna malumbano kati ya Misri na Ethiopia.

Japo si egemei mahali popote hebu fikiria pasiwe na sheria za umwagiliaji alafu kuweko na wakulima kama wale 20 ambao ndani ya saa wametumia maji lita milioni moja kila mmoja. Je huo mto unakuwa na kitu gani.

Mchina atawajibishwa kama vibali hana au amekengeuka makubaliano ya matumizi ya maji kwa kipindi vha upungufu wa maji
Kwahiyo yule mchina kasababisha upungufu wa maji dar ?
 
Mimi siongelei Mchina, naongelea zaidi ile kauli ya jumla kuwa wakuu wa Wilaya na Mikoa wawakamate waliochepusha maji. Wewe unajua jinsi viongozi na pilisi wetu walivyo, ikitoka kauli kama hiyo.
Hapo limetengenezwa chaka la kuonea watu na kuharibu Mali zao.

Polisi na wakuu wetu wa mikoa nao wanapata chaka la kujipatia chochote kutoka kwa wakulima na wafugaji.

Watendaji wa vijiji na maafisa wa serikali kuanza kupora Mali za watu kwa visingizio vya kuvamia vyanzo vya maji.

Nchi hii inaendeshwa na corrupt and uncivilized civil service.

Uhuni uliorasmishwa.
 
Very logical question. Ule ni uwongo. Serikali inashindwa kutimiza wajibu wake, wanatafuta mtu wa kumbebesha lawama. Na Watanzania baadhi walivyo wajinga wanaamini mkoa wa Pwani na Dar wanakosa maji kwa sababu ya mchina.

Ok, mchina amekamatwa, kuanzia jana maji yanatirirka kwenye mambomba yote ya mkoa wa Pwani na Dar?

Mchina yawezekana amekwenda kinyume cha kibali chake cha kutumia maji, au pengine hajakiuka chochote, lakini siyo kweli eti vile vimeshine vya HP 20 eti vinvuta maji milioni 1 kwa saa. Na uwongo mkubwa, wa ajabu, na lazima uwe una uwendawazimu kuuamini. Tangu lini engine 2 za 20 HP kika moja, zikavuta maji lita milioni 1 kwa saa? Hizo haziwezi kuvuta hata lita 50,000 kwa saa. Wenye uelewa kidogo wa machines, watanielewa.
Hivi kwanza lita million kwa saa zinamwagilia shamba la ukubwa gani ?

Hilo shamba au mafuriko.

Kuna mambo yanakera sana njia imetengenezwa ya kuonea watu.
 
Wazo zuri, ila naomba niku challenge kwa swali! Kwenye hili tatizo la maji na umeme wewe binafsi labda na familia yako umepiga hatua gani kujitegemea kwenye suala la umeme na maji au nawe ni kupepesa mdomo kulaumu wengine huku wewe mwenyewe ukiwa tegemezi!!
Lengo la hoja yako hasa ni nini ?
 
Siku zote, wananchi wamehamasishwa kufanya kilimo cha umwagiliaji. Ilani za uchaguzi za vyama vyote vya siasa za miaka yote, zinaeleza kama vyama hivyo vikipewa dola jinsi vitakavyoendeleza au vitakavyofanya ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinafanyika kwa ufanisi.

Makongamano, semina mbalimbali zimewahi kufanyika kuhamasisha kilimo cha unwagiliaji. Leo unawaambia wananchi wasifanye kilimo cha umwagiliaji. Hivi nchi hii inaongozwa na watu wa namna gani! Wakiacha kilimo cha umwagiliaji, baada ya miezi michache, tuanze tena kumwomba Mungu akete chakula?

Watanzania tuna laana gani, hadi kupata viongozi wasio na maono? Viongozi ambao, kunapotokea tatizo, badala ya kukaa, kutafakari kuhusisha think tanks, kuona namna bora ya kutatua tatizo bila ya kusababisha matatizo mengine, wanaibuka tu na kutoa kauli - kuanzia leo, hiki au kile marufuku. Very low thinking and leadership ability!

Tatizo la maji na umeme halijasababishwa na upungufu wa mvua wala maji bali kutokana na mipango mibovu ya Serikali. Na mipango mibovu ya Serikali inasababishwa na aina ya watu waliopo serikalini.

Nchi kama Mali, Niger, Guenea, Benin wanategemea mto Niger kama chanzo cha maji ya kutumia majumbani na kama chanzo cha cha uzalishaji umeme wa maji, na nimewahi kukaa mfululizo katika mataifa hayo miezi 6, umeme haukuwahi kukatika hata siku moja.

Kila nchi inayotumia maji ya mto Niger, imejenga mabwawa makubwa ya kutunzia maji, na mabwawa hayo yanajazwa kwa overflows za wakati wa kipindi cha mvua. Sisi wenye mito usiyo na hesabu, na maziwa makubwa, eti tunaongelea upungufu wa maji? Watasemaje Wamisri, watasemaje Walibya, Mali, Ghana, Burkina Faso na mataifa mengine yaliyo karibu na jangwa la Sahara?

Tusipepese macho, ukweli ni kuwa tuna shida ya umeme na maji kutokana na viongozi wasio na maono, mipango wala weledi. Tanzania siyo nchi ya kuzungumzia upungufu wa maji.

Kwa matatizo haya yanayotukumba sasa, na mengine ambayo hatukustahili kuwa nayo, yanatufanya tuzungumzie upungufu wa akili na tatizo la kushindwa kupata viongozi wenye weledi na maono.
Tulisema Jpm aliletwa na Mungu ili Watanzania tuamke usingizini. Mkaona wapinzani ninwehu. Ukweli sasa mnauon awenyewe. Kwamba Jpm aliruhusu walime hata kwenye vyanzo vya maji na wasibuguziwe. Mkampigia makofi. Leo hata mifupa yake haija oza mmeona matokeo.
Sasa jifunzeninkwa kuona.
 
Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa mkoa wa mtwara baada ya kuharibu mashamba ya Mbowe, nchi ya ajabu sana hii katika sayari ya dunia
Wakati wa marehemu, viongozi walikuwa wanashindana kufanya uovu dhidi ya wapinzani. Anayefanye ujambazi zaidi, marehemu Magufuli alimwona ndiye anayefaa zaidi. Tikuwa na kiongozi aliyefurahia zaidi uovu, uharamia na chuki kuliko wema.
 
Lengo la hoja yako hasa ni nini ?
Sio hoja hiyo ni changamoto ya kutaka majibu!!
Jibu lako:
Jitahidi kujitegemea kwa maji na nishati!

Wasiwasi wangu ni uelewa wa kichwa chako, ngoja nione utakavyojibu nikuelewe zaidi
 
Hapo limetengenezwa chaka la kuonea watu na kuharibu Mali zao.

Polisi na wakuu wetu wa mikoa nao wanapata chaka la kujipatia chochote kutoka kwa wakulima na wafugaji.

Watendaji wa vijiji na maafisa wa serikali kuanza kupora Mali za watu kwa visingizio vya kuvamia vyanzo vya maji.

Nchi hii inaendeshwa na corrupt and uncivilized civil service.

Uhuni uliorasmishwa.
Upo sahihi sana. Sijui tuna laana gani. Watu wenye uelewa mdogo wamebeba dhamana ya watu wote, pamoja na ya super intelligent people.
 
Sio hoja hiyo ni changamoto ya kutaka majibu!!
Jibu lako:
Jitahidi kujitegemea kwa maji na nishati!

Wasiwasi wangu ni uelewa wa kichwa chako, ngoja nione utakavyojibu nikuelewe zaidi
Kodi wanayolipa wananchi iwe inafanya kazi gani ili hali huduma kama hizo watakuwa wanajitegemea ?

Kwa hoja yako hii unataka kusema kila mwananchi wa Dar es Salaam awe na kisima chake cha maji nyumbani kwake ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom