Maajabu Makubwa - Kuzuia Kilimo cha Umwagiliaji

Sheria zipo zinazohusiana na Uchepusha maji kwaajili ya umwagiliaji.
Yule mchina kama anavyovibali hana kosa lolote japo sheria zimeongela ikitokea kumetokea upungufu wa maji je anapaswa kufanyaje.

Sio tuu umwagiliaji ila hata mto unaokatiza nchi tofauti unazo kanuni zake katika matumizi ya maji ndo mana mnaona kuna malumbano kati ya Misri na Ethiopia.

Japo si egemei mahali popote hebu fikiria pasiwe na sheria za umwagiliaji alafu kuweko na wakulima kama wale 20 ambao ndani ya saa wametumia maji lita milioni moja kila mmoja. Je huo mto unakuwa na kitu gani.

Mchina atawajibishwa kama vibali hana au amekengeuka makubaliano ya matumizi ya maji kwa kipindi vha upungufu wa maji
Tutajie hiyo sheria na kanuni husika ili tujue. Pili hivi Tanzania kuna miti mingapi ambayo mwisho wa siku maji huishia baharini? Unaweza kutuambia kwa saa moja mto Ruvu hupitisha na kumwaga baharini lita ngapi za maji ili tuone athari inayoweza kutokea ikiwa watu 100 watanyonya maji kwa pump kwa ajili ya kilimo? Hivi unajua ni kwa nini watanzania zaidi ya 80 % wanaotegemea kilimo ni masikini wa kutupwa?! Unaweza kunitajia tajiri angalau mmoja tuu aliyetajirika kwa kilimo cha kutegemea mvua??
 
Naangalia taarifa ya habari hapa...

Kuna bwana yupo Makongo Juu mwenye mabwawa ya samaki makubwa, DAWASA naona wamempiga chenga wanataka Wizara wasemelee....

Jamaa atapata hasara wqkifunga maji, ila atawapiga hela nyingi sana mahakamani
 
Ndugu ni kweli unaamini kuwa yule mkulima ana tumia lita milion 24 za maji kwa siku? Hayo maji anayapeleka wapi kwenye ardhi ya ukubwa gani anayolima yenye uwezo wa kunyonya hayo maji?
Mimi nina shamba la ekari nne na natumia pump niliyo nunua kwa laki saba hicho wanachosema ni uongo kabisa, unajua lita milioni moja ni pipa elfu 50, pipa laki tano kwa masaa 10?
 
Kwanini watu kila wakipata shida lawama kwa serikali mlidhani serikali ni kitu kizuri? Wenye akili walipojenga nyumba zao hata kama kuna maji ya system lakini wamechimba visima vyao ili kuondoa dependency na umeme pia kwa solar
Hili nalo ni tatizo, unakuta matajiri wakubwa lakini hawana back up plan ya visima vikubwa vya maji..
 
Wazo zuri, ila naomba niku challenge kwa swali! Kwenye hili tatizo la maji na umeme wewe binafsi labda na familia yako umepiga hatua gani kujitegemea kwenye suala la umeme na maji au nawe ni kupepesa mdomo kulaumu wengine huku wewe mwenyewe ukiwa tegemezi!!
Mimi kijijini kwetu nimechimba kisima na wala hata milioni mbili haikuisha. Maji ya kutosha miaka yote mpaka majirani wanachota, tena free. Solar siku hizi ni za kumwaga tuu
 
Hili nilishalisema, kuna watu wenye low IQ wapo mahala na ndo viongozi wanaofanya maamuzi kwa niaba ya wadanganyika.......
 
Tanzania haitakiwi kulalamika ukosefu wa maji maana tumezungukwa na maji kila kona. Ni aibu kubwa sana, tungekuwa na viongozi wenye maono wala tusinge jishughulisha na uchimbaji visima kwa sasa, tungeyaacha maji chini ya ardhi yabakie kama akiba.
 
Zipo taratibu za kufata ili ufanye kilimo cha umwagiliaji
Huwezi ukajionganishia mabomba na kuweka
Pump ya kuvuta maji kutoka mtoni ukafanya umwagiliaji,hizi sheria zipo nenda rudi
Ukimuachia mwanadam afanye anavyotaka kwenye vyanzo vya maji,mtaliaaaaa

Ova
Na pia ukiruhusu nchi iongozwe na watu ambao hawana ubunifu wala weledi, wananchi mtajuta.
 
Kama zile za kule HAI alizozibomoa na kuharibuharibu huyu hapa?
_MG_0071.JPG

Inasikitisha sana,yaani unaharibu maisha ya wafanyakazi zaidi ya 400 kisa siasa za maji taka! Laana itawatafuna na imeshaanza kuwatafuna aliyeagiza kashaenda,jambazi sabaya naye kawa kama Msouth Sudan.
 
Unajua gharama ya kuchimba kisima na kufanya irrigation? Bei ya mazao inapanga Selikari watu wakitumia mbinu rahisi za kulima mnawazuia mnataka wachimbe visima Selikari imeshindwa nini kuchimba visima na kujaza mabwawa?

Yes najua mkuu ,ukulima ni kazi minabidi uthamini kazi yako ,inahitaji uwekezaji mkuu,mcheck pinda amechimba visima ,wakulima ambao serious wanachimba visima mkuu.
 
Siku zote, wananchi wamehamasishwa kufanya kilimo cha umwagiliaji. Ilani za uchaguzi za vyama vyote vya siasa za miaka yote, zinaeleza kama vyama hivyo vikipewa dola jinsi vitakavyoendeleza au vitakavyofanya ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinafanyika kwa ufanisi.

Makongamano, semina mbalimbali zimewahi kufanyika kuhamasisha kilimo cha unwagiliaji. Leo unawaambia wananchi wasifanye kilimo cha umwagiliaji. Hivi nchi hii inaongozwa na watu wa namna gani! Wakiacha kilimo cha umwagiliaji, baada ya miezi michache, tuanze tena kumwomba Mungu akete chakula?

Watanzania tuna laana gani, hadi kupata viongozi wasio na maono? Viongozi ambao, kunapotokea tatizo, badala ya kukaa, kutafakari kuhusisha think tanks, kuona namna bora ya kutatua tatizo bila ya kusababisha matatizo mengine, wanaibuka tu na kutoa kauli - kuanzia leo, hiki au kile marufuku. Very low thinking and leadership ability!

Tatizo la maji na umeme halijasababishwa na upungufu wa mvua wala maji bali kutokana na mipango mibovu ya Serikali. Na mipango mibovu ya Serikali inasababishwa na aina ya watu waliopo serikalini.

Nchi kama Mali, Niger, Guenea, Benin wanategemea mto Niger kama chanzo cha maji ya kutumia majumbani na kama chanzo cha cha uzalishaji umeme wa maji, na nimewahi kukaa mfululizo katika mataifa hayo miezi 6, umeme haukuwahi kukatika hata siku moja.

Kila nchi inayotumia maji ya mto Niger, imejenga mabwawa makubwa ya kutunzia maji, na mabwawa hayo yanajazwa kwa overflows za wakati wa kipindi cha mvua. Sisi wenye mito usiyo na hesabu, na maziwa makubwa, eti tunaongelea upungufu wa maji? Watasemaje Wamisri, watasemaje Walibya, Mali, Ghana, Burkina Faso na mataifa mengine yaliyo karibu na jangwa la Sahara?

Tusipepese macho, ukweli ni kuwa tuna shida ya umeme na maji kutokana na viongozi wasio na maono, mipango wala weledi. Tanzania siyo nchi ya kuzungumzia upungufu wa maji.

Kwa matatizo haya yanayotukumba sasa, na mengine ambayo hatukustahili kuwa nayo, yanatufanya tuzungumzie upungufu wa akili na tatizo la kushindwa kupata viongozi wenye weledi na maono.
Watu wa Kilimanjaro walimuomba mama msaada wa kurekebisha skimu ya umwagiliaji ya Lower Moshi wakaishia kujibiwa bila aibu kuwa: wakati ninyi mnalilia maji ya kumwaga kwenye mashamba yenu wenzenu hawana maji ya kunywa. Huyu ndio muunguja halisi anayefikiri kilimo cha umwagiliaji ni kutumia maji vibaya!
 
Watu wa Kilimanjaro walimuomba mama msaada wa kurekebisha skimu ya umwagiliaji ya Lower Moshi wakaishia kujibiwa bila aibu kuwa: wakati ninyi mnalilia maji ya kumwaga kwenye mashamba yenu wenzenu hawana maji ya kunywa. Huyu ndio muunguja halisi anayefikiri kilimo cha umwagiliaji ni kutumia maji vibaya!
Duuuh
 
Na huyo anayeharibu hapo katumbuliwa, nilikutana naye recently kachoka ile mbaya...

Safi sana adui mwombee njaa ,wote laana itawatafuna ,wao walidhani wanamkomoa mbowe ,kumbe mbowe nyuma amebeba maisha ya watu wengi kwenye huo mnyororo ,imagine watu hao wote wawe wananung'unika kwa sababu ya hao wapuuzi ,ni lazima laana iwatafune tu.
 
Mambo mengine ni aibu hata kuyasikia! Yaani jamaa hakuna ubunifu kabisaaaaa
 
Acheni ujinga, yaani mna mtetea huyo mchina wenu anaye chota lita milioni 1 kwa saa na kusababisha ma milioni ya waTz kukosa maji, kwa nini asi chimbe kisima chake?? Huo ni uwekezaji au uhalibifu, Sometimes iachieni serikali ifanye yake,
Ebu acheni ujinga, huyo mchina alipaswa ashtakiwe kwa kuhujumu uchumi….,
Nioneshe mashine anayoitumia nami nitakwambia uongo wa serikali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom