Haya ni maajabu ya chama gani? (1) Katiba siyo kipaumbele cha nchi, (2) Makaburi mengine marufuku kuyafukua, tutashindwa kuyafukia (3) wanachama kujadili siasa kabla ya 2020 wakati mwenyekiti wao kasema siasa hadi 2020 (4) Kuota nchi ya viwanda bila kilimo cha kisasa na elimu bora (5) Kununua ndege kuhudumia 5% ya wananchi badala ya pembejeo kuhudumia 85% ya wananchi (6) Kula rambirambi za wahanga wa tetemeko la kule kwetu (7) Kumpa mtuhumiwa wa wizi wa Rada ya mabilioni kututungia na kutuandikia katiba ya nchi (8) Kutupilia mbali maoni ya wananchi juu ya katiba ya nchi yao (9) kuwa na mwanachama aitwaye Jeechaa (10) Kiongozi wake mkuu kugoma kwenda kuwapa pole wafiwa na wahanga wa tetemeko la ardhi kule...... (11) kugeuza viwanja vyote vya michezo, ofisi na majengo yaliyojengwa kwa kodi za watanzania wote na kufanya vyote hivi kuwa ni vyake.