Elections 2010 Maagizo ya NEC yabezwa na msimamizi wa uchaguzi wa Tarime

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Wakati NEC imetoa maelekezo ya kuwa wapigakura tuna uhuru wa kuwa mita 100 kutoka vituo vya kupiga kura na mapolisi wasitusumbue utata umejitokeza pale ambapo msimamizi wa uchaguzi wa Tarime alipoagiza kuwa wapigakura waishie majumbani kwao mara baada ya uchaguzi.

Kauli hii ya huyu msimamizi inakinzana na maagizo ya NEC yaliyotolewa hivi majuzi na Naibu Mwenyekiti wa NEC pale alipokuwa anajibu swali la mgombea ubunge jimbo la Bukoba Mjini Bw. Rwakatare.

NEC inaelekea maagizo yake bado hayajawafikia watendaji wake huko kwenye majimbo au wasimamizi wa uchaguzi wanabeza maelekezo ya mabosi wao. Hili linawezekana kabisa kutokana na NEC kuwatumia waajiriwa wa muda kutoka serikali za mitaa ambao hawana sauti juu ya ajira zao.

Inawezekana kabisa wasimamizi hawa wanapokea maagizo kutoka viongozi serikalini wagombeaji na wenye mkakakati wa kuchakachua matokeo ......
 
Elimu haijatolewa kwa wappiga kura, Mita 100, wengine wanasema Mita 200!!! Nini ni nini, na hata hzo mia naona ni nyingi mno, mwaka huu inatakiwa nek to neki....hakuna kuachiwa mtu nafasi ya kuchakachua! 50m, na si zaidi ya hizo! Na gari zote ziishie nje ya perimeta hiyo! kila kitu kinachoshuka na kuingia kwenye magari kionekane live! mida ya masihara imekwisha kitambo, tunataka HAKI!:photo:
 
kama chama kina mawakala kwanini wananchi wote wabaki sehemu ya kupigia kura?
kuna baadhi ya maeneo ni kawaida kuwa na vurugu hasa tarime nafikiri msimamizi analijua hilo.
nasikia huko hao jamaa wanatembea na mapanga na visu kama watu wanavyotembea na simu na leso huku
 
Kama mwafrika, mtanzania, mwanakijiji kuwa na kisu au panga ni sehemu ya vitu muhimu kama ulivyojifananisha wewe wa mjini kutembea na simu. Kijijini utampigia nani simu kwa ajili ya msaada, yakupasa uelewe mazingira na tamaduni za watu acha mawazo mgando hapo mbele ya PC yako.
 
sheria haikatazi watu kuwepo hapo, hata hiyo mita mia (100m), ni kama pendekezo tu la kibusara ili kuzuina uwezekano wa kutokea fujo
 
kama chama kina mawakala kwanini wananchi wote wabaki sehemu ya kupigia kura?
kuna baadhi ya maeneo ni kawaida kuwa na vurugu hasa tarime nafikiri msimamizi analijua hilo.
nasikia huko hao jamaa wanatembea na mapanga na visu kama watu wanavyotembea na simu na leso huku

Grow up brah!!
Ukisikia tu, unaanza kubwabwaja ovyo .... !!
 
kama chama kina mawakala kwanini wananchi wote wabaki sehemu ya kupigia kura?
kuna baadhi ya maeneo ni kawaida kuwa na vurugu hasa tarime nafikiri msimamizi analijua hilo.
nasikia huko hao jamaa wanatembea na mapanga na visu kama watu wanavyotembea na simu na leso huku

Hii nayo ni crap toka crap village kwa crapson wa .....
 
Back
Top Bottom