Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,337
Maafisa Afya nchini wametakiwa kurejesha upya (renew) leseni zao kabla ya Machi 5 mwaka huu na hatua kali zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo ikiwemo kufutiwa usajili.
Hayo yamesemwa na Msajili wa Baraza la Afya Mazingira Iddi Hoyange katika kikao cha Baraza la Afya kilichofanyika mkoani Morogoro.
Hoyange amesema endapo mwanataaluma atafutiwa usajili ni wazi kwamba hawezi kutekeleza tena majukumu ya Afisa Afya nchini
Aidha, amewataka wadaiwa wote kukamilisha malipo ya usajili ili kuepuka kufungiwa baada ya kufika muda huo wa mwezi mmoja.
Hoyange amesema Baraza limefanikiwa kupitisha muongozo wa maadili kwa maafisa Afya nchini kwa kufanyiwa marekebisho kwa lugha ya kiingereza na kutaka kila mwanataaluma kufuata miongozo iliyowekwa.
Hoyange amesema hadi kufikia kikao kingine cha baraza hilo kinachotarajia kufanyika baada ya miezi minne utakua umetafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ili iwe rahisi kusomeka na kueleweka kwa wadau wote.
Imetolewa na;
Wizara ya Afya Tanzania