Maafisa Usalama wavamia nyumba za Diddy, akakimbia msala na ndege yake binafsi inafuatiliwa huko Antigua Caribbean

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,692
JUST IN: Rapper Diddy's private jet has been tracked to the Caribbean islands after his homes were raided in relation to a s*x trafficking investigation.

The jet appeared to land on Antigua in the Caribbean according to flight tracking data.

At the moment, it is unknown if Diddy is actually on the plane or not.

TMZ is reporting that the jet "currently grounded" on Antigua.

"The plane is currently grounded there, although the flight data has yet to update and register him as having officially landed. In any case, it's definitely Diddy's jet ... no question," they reported.

Diddy's LA and Miami homes were raided on Monday in relation to a federal investigation into s*x trafficking, narcotics as well as firearms.
_20240326_034523.JPG


======================

MAREKANI: USALAMA WAVAMIA NYUMBA ZA DIDDY, MWENYEWE HAJULIKANI ALIPO
Nyumba ya Mfanyabiashara na Mwanamuziki Sean ‘Diddy’ Combs zilizopo Los Angeles na Miami zimevamiwa na Maafisa Usalama ikidaiwa wanafanya uchunguzi na upekuzi kuhusu tuhuma za Biashara ya Ngono na Biashara ya Binadamu zinazotajwa kuhusu staa huyo.

Maafisa wa HSI ambacho ni Chombo Kikuu cha Uchunguzi cha Idara ya Usalama wa Taifa ya Marekani wamewafunga pingu baadhi ya Watu waliokutwa katika nyumba ya Los Angeles wakiwemo Watoto wa Diddy ambao ni King na Justin huku baba yao akiwa hajulikani alipo.

Wakati hayo yakiendelea inadaiwa ndege Binafsi ya Diddy imeonekana ikiwa njiani kuelekea Visiwa vya Caribbean kwa mujibu wa Tovuti ya Flight Tracking Data.
WATOTO.png

King Justin.png
 
Jamaa alifanikiwa kibishara akawa Bilionaire lakini inaonyesha akili yake ni ya kitoto tu. Sasa anadhani anaweza kuikimbia serikali ya Marekani kwenda kujificha Antigua kweli? Kwa kawaida ukiwakimbia polisi ndipo unawapa confidence kuwa kweli una hatia
 
Huku tunamtaka mpaka ex president Trump.

Kama watu wamemfanya a sitting president Nixon mpaka kajiuzulu, wakikwambia "nobody is above the law" unaweza kuwa entertain kidogo hata kama bado kuna mapungufu mengi.
Kweli kama hivi unaamini kweli marekani ni balaa kabisa.

Tanzania hivi mfano kikwete tu,au tuseme mtoto wake anaweza kuwekwa ndani akikutwa na hatia?

Tuseme tu ukweli,hao jamaa wako mbali sana.
 
Kuna mahala pesa haifanyi kazi kabisaa hawa jamaa wao ni kufwata sheria ya Nchi yao inataka nini na haitaki nini, huku Afrika asingaliguswa ingalibakia kusema uchunguzi hauja kamilika miaka inakwenda. Utawla wa sheria kwakweli ni nguzo ya kuendesha Nchi bila hofu yoyote maana hamna aliye juu ya sheria kabisa.
 
Back
Top Bottom