Maafa Kahama: Magazeti ya bongo utata mtupu

Maafa Kahama: Magazeti ya bongo utata mtupu

Prezidah

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
750
Reaction score
182
Salaam waungwana,

Katika ukurasa wa kwanza (front page) wa karibu magazeti yote leo 05.03.2015 taarifa kubwa ni kuhusu maafa kahama yaliyotokana na mvua kubwa. Naungana nanyi kuwapa pole wafiwa wote pamoja na kuwaombea uponyaji wote waliopatwa na majeraha.

Kutoa/kupata habari ni jambo moja na kutoa/kupata habari sahihi nayo ni jambo jingine. Sasa nisiwachoshe kero yangu leo ni idadi ya watu waliofariki na majeruhi katika maafa hayo nani yupo sahihi? ??? Nimenukuu yaliyoandikwa kwenye magazeti yetu ili tujiulize kwa pamoja;

"At least 42 killed and dozens injured" ---- the citizen

"More than 40 died on spot & 82 injured"-----daily news

"Storm claims 38 lives & 82 others seriously injured"---the guardian

"Watu 40 wapoteza maisha, 85 wajeruhiwa"-----uhuru

"Mvua yaua 38 shinyanga, yajeruhi 82"----jambo leo

"Mvua yaua 38" ----- Habari leo

"Mvua ya mawe yaua 42 na kujeruhi 82 kahama"--'-'Raia Tanzania

"Barafu yafunika kijiji, Watu 42 wafariki dunia kahama, zaidi ya 91 wajeruhiwa"---Mtanzania

"Watu 39 wafariki, 59 mahututi"---Majira

"Gharika yaua 38, zaidi ya 82 wajeruhiwa"---Tanzania Daima

"Mvua yaua 38, yajeruhi 82"-----Nipashe

"Mvua ya mawe yaua watu 42 na kujeruhi wengine 91 kahama"----Mwananchi

Kati ya magazeti haya yapo ya serikali, vyama na hata kampuni moja lakini takwimu tofauti. Ingekuwa ni hesabu ya kawaida ningetafuta wastani then am done lakini hizi si namba tu bali maisha ya watu. Nisaidieni je tatizo ni waandishi wa habari hizi au wahariri? ??? Je hapa kuna weledi kweli?
 
Hiyo 42 wafariki na 82 majeruhi imetajwa Sana,huenda ikawa sahihi....inaonekana kila gazeti lina chanzo chake cha habari na ndiyo sababu ya mkanganyiko huo..
 
Kiukwer itakua hawapo sahih na wengne wapo sahih cha msing jua tuu maafa yametokea watu wamefark bas hiyo idad kamili tutaipata coz watu wengine wameendelea kupoteza maisha.
Pelen saaana
 
Cku ya tukio waliokufa walikuwa 42 ss hatujua km idadi iliongezeka wakazd hapo au la!
 
Ukiangalia taarifa hizo hazitofautiani sana. Unajua haya ni maafa, taarifa zake zabadirika kulingana na muda na kile wanachokiona katika field. Muda unavyosonga majeruhi wanaweza kufa; lakini pia watapata watu wengine (ni kama wanatafuta, maana si wanafanya uokozi) waliokumbwa na maafa pamoja na majeruhi. Sasa inategemea mwandishi alichukua taarifa za muda gani na kuamua kuziandikia habari. Maana kila chombo kina deadline yake ya kukusanya habari. Vyombo vikubwa vyenye nguvu kama Mwananchi utaona vinachapisha taarifa latest zaidi. Ndio maana hata idadi za vifo na majeruhi walizoandika ni kubwa.

"At least 42 killed and dozens injured" ---- the citizen
"Mvua ya mawe yaua watu 42 na kujeruhi wengine 91 kahama"----Mwananchi
 
Kiukwer itakua hawapo sahih na wengne wapo sahih cha msing jua tuu maafa yametokea watu wamefark bas hiyo idad kamili tutaipata coz watu wengine wameendelea kupoteza maisha.
Pelen saaana

Mkuu naungana na wewe lakini huu upukun.yuku ukiendelea hivi tutaingia kwenye machafuko wakati wa uchaguzi. Just imagine ndo matokeo ya ubunge/urais hayo
 
Ukiangalia taarifa hizo hazitofautiani sana. Unajua haya ni maafa, taarifa zake zabadirika kulingana na muda na kile wanachokiona katika field. Muda unavyosonga majeruhi wanaweza kufa; lakini pia watapata watu wengine (ni kama wanatafuta, maana si wanafanya uokozi) waliokumbwa na maafa pamoja na majeruhi. Sasa inategemea mwandishi alichukua taarifa za muda gani na kuamua kuziandikia habari. Maana kila chombo kina deadline yake ya kukusanya habari. Vyombo vikubwa vyenye nguvu kama Mwananchi utaona vinachapisha taarifa latest zaidi. Ndio maana hata idadi za vifo na majeruhi walizoandika ni kubwa.

Naomba niweke sawa mkuu hivi magazeti ya mwananchi, nipashe na the guardian yana bosi tofauti? Namaanisha mmiliki + mhariri
 
Source yao ya hizo namba ni nini?

Hao ndiyo sampuli ya akina Pasco na Manyerere Jackton, makanjanja tu.
Faiza, to me "age ain't nothing but a number!", kama vipi, sema tuu, I don't mind!.

Kwa wale wadogo, tunaanza sisi, ila kwa wakubwa, wanaanza wao!, nakuona Faiza unaanza!,

Sema tuu, mimi ndio zangu!.

Pasco
 
Back
Top Bottom