Maafa Dodoma: Mvua yasababisha Mafuriko Mpwapwa, Watu zaidi ya wanne wapotea

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Maafa Mpwapwa, watu wanne wafariki dunia baada ya Mvua kubwa kunyesha. Inadaiwa wamesombwa na mafuriko wakiwa wamelala. Hadi sasa miili ya watu watatu imeshapatikana, hivyo tupo kwenye kutafuta miili mingine zaidi.

Serikali ingesaidia kuleta vikosi vya uokoaji kusaidia.
16427263_1849402701984605_979886366526456850_n.jpg
16386985_1849402805317928_7913928458821398293_n.jpg
16195498_1849403131984562_1826767974556659739_n.jpg

Hapa watu waliposimama, kulikuwa na nyumba, imesombwa na maji na watu wote waliokuwa ndani
16266105_1849407165317492_6163664773997252724_n.jpg

16299557_1849395431985332_6355418398488840923_n.jpg
16265269_1849394988652043_7196739905910329454_n.jpg

Watu wanne wakiwamo watatu wa familia moja, wamefariki dunia baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Hata hivyo, viongozi mbalimbali wametoa takwimu zinazotofautiana kuhusu idadi ya vifo vilivyotokea.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema watu wanane walikuwa wameripotiwa kufariki dunia na kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ilikuwa inajiandaa kwenda eneo la tukio ili kujionea uharibifu uliotokea.

Lakini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema taarifa alizonazo ni za watu watatu waliopoteza maisha na kwamba bado hajapata taarifa sahihi za tukio ambalo lilitokea katika vijiji vya Mang’angu na Chinyika katika Kata ya Ving’awe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mmoja wa manusura, Beka Mlami (10) alisema walikuwa wamelala wakiwa watano katika nyumba yao mvua kubwa ilipoanza kunyesha kuanzia saa tatu usiku na ilipofika usiku wa manane nyumba yao iliyojengwa kwa udongo ilisombwa na maji.

Mbali na yeye, wengine waliokuwa katika nyumba hiyo ni Martha Sumisumi (60), Shukuru Donald (15) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mwanakianga, Bernadetha Sumisumi (9) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Ilolo na Joseph Sumisumi (12) ambaye alinusurika.

Beka alisema baada ya kuona maji yameingia ndani, aliwaambia ndugu zake wakimbie watoke nje na wakati wanajiandaa kuvaa nguo nyumba yao ilianguka na kuwaponda, lakini yeye alifanikiwa kutoka na kupanda juu ya bati.

Alisema baada ya kutoka nje ndipo gogo kubwa la mti lililosombwa na maji lilipopiga nyumba yao na kuanguka chini hivyo ndugu zake wengine kushindwa kutoka na hivyo kusombwa na maji.

Alisema baada ya kutoka nje alimwona ndugu yake mwingine Joseph akiwa anapelekwa na maji, lakini alifanikiwa kujiokoa.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Steven Noel alisema nyumba iliyosombwa na maji ilikuwa imejengwa karibu na korongo la maji, hivyo baada ya mvua kunyesha, maji yaliacha mkondo wake na kuingia kwenye makazi ya watu na kusababisha maafa hayo.

“Mvua ilisababisha mafuriko makubwa ambayo yalikuwa yamebeba na magogo makubwa ambayo yaliipiga ile nyumba na kuivunja katikati,” alisema Noel.

Alisema baada ya gogo la mti kuipiga nyumba hiyo, maji yalijaa ndani na kwa kuwa milango ilikuwa imefungwa, yalikosa njia ya kutokea na kuiangusha.

Noel alisema kulipopambazuka, walifukua na kuipata miili ya watu hao watatu huku mwili mwingine wa Jesca Lubeleje (19) mkazi wa Kijiji cha Chinyika ukiokotwa.
 
Maafa Mpwapwa, watu wanne wafariki dunia baada ya Mvua kubwa kunyesha. Inadaiwa wamesombwa na mafuriko wakiwa wamelala. Hadi sasa miili ya watu watatu imeshapatikana, hivyo tupo kwenye kutafuta miili nyingine zaidi.

Serikali ingesaidia kuleta vikosi vya uokoaji kusaidia.
View attachment 465614 View attachment 465615 View attachment 465616

Guys! Nimepoteza ndugu zangu watatu. Kwa bahati miili yao imepatikana ambapo mmoja ni mama mtu mzima aitwaye Martha Chalo Mbega (62), mtoto wa kaka yangu pamoja na wajukuu zake wawili. Wakati mafuriko yanatokea usiku wa manane, nimeambiwa kwamba, ndani walikuwa jumla ya watu watano, lakini wawili wakanusurika baada ya kukimbia.

Taarifa za wananchi katika eneo la tukio ni kwamba, wakati wameipata maiti ya mama huyo kutoka umbali wa takribani kilometa tano kutoka weneo la tukio, pia wameiokota maiti na mwanamke mwingine ambaye hajatambulika.

NIOMBEENI NA TUWAOMBEE MAREHEMU
 
Poleni sana mkuu, Mungu awatie nguvu wafiwa.
 
Pole sana kamanda
 
Soal sad poleni sana mkuu
 
Serikali hii sikivu inatoa msaada tu pindi ofisi za ccm au biashara za ccm zimeathiriwa, Wananchi msubirie mpaka uchaguzi ukifika mtakumbukwa. Na sasa hivi hakuna hata kampuni au watu watakaojotelea kutoa misaada kwa sababu Magufuli na wenzake wataichukuwa
 
Back
Top Bottom