Maadui wa Watanzania: Aongezeka mmoja

Ulimali

Member
Nov 5, 2010
51
1
Wana JF

Kwa muda mrefu tumekuwa na maadui watatu yaani Ujinga, maradhi na umasikini na tumekuwa tukipambanao mimi kwa mtazamo wangu ni kuwa ameongezeka adui mwingine ambaye CCM nasema hivyo kwa sababu CCM haijui kwanini Tanzania ni masikini na kama hujui tatizo hilo la umaskini si rahisi kuwa na strategy ya kulitatua.

Nadhani mtaniunga mkono kuwa wakati Mwl J.K.Nyerere anapata Uhuru wa Nchi hii alitangaza kuwa tunakabiliwa na maadui WATATU ambao ni, NJAA, UJINGA na MARADHI ila kwa bahati mbaya sana kwa mtazamo wangu na kwa watanzania wenye mtazamo kama wa kwangu ni dhahili mtakubaliana na mimi kuwa kwa sasa maadui hao wameongezeka na adui aliyeongezeka anaitwa adui ''UCHAMA''

Nasema UCHAMA ni adui wa nne kwasababu ya kile kinachoendelea ''SERIKALINI'' hasa huko Bungeni Dodoma maarufu kama mjengoni, imekuwa ni nadra sana kwa wafanya maamuzi wetu (Wabunge) kuweka maslahi ya taifa hasa katika maamuzi ya msingi, Kama utakuwa makini jambo hili lazima likutie shaka

Ni mangapi yamekuwa yakifanyika kinyume na maslahi ya TAIFA badala yake yanafanyika kwa maslahi vyama?, hoja Binafsi ngapi zinazimwa bungeni ''ETI'' kulinda heshima ya chama?, Wabunge wangapi wanazomewa bungeni hasa wakisema juu ya maslahi ya wananchi?, Wabunge wangapi wakionyesha nia thabiti ya kutetea maslahi ya Wamanchi wanazimwa na Wakuu wa vyama vyao?

Ni rahisi sana kujibu maswali hayo hapo juu na jibu ni rahisi kuwa kwa mwendo huu hatuwezi kupiga hatua maana ''UCHAMA'' imekuwa ndiyo nongwa kwa maendeleo yetu
Nawasilisha kwa uchungu!!

Huyo ni adui wa 5 ndugu, adui wa 4 huyu hapa:

[h=3]The Young Nyerere on the Fourth Enemy[/h]

On 17 May 1960 the radical Nyerere uttered the following revolutionary words archived in the Hansard of the 35th Parliamentary Session and reproduced in his book onFreedom Unity under the title Corruption as an Enemy of the People:

"...I would like to add, sir - and I don't want to elaborate on this, there is no point in elaborating - I want to add there is another enemy which we must add on the list of these enemies poverty, disease, ignorance, I think we must add another enemy... There is corruption. Now, sir, I think corruption must be treated with ruthlessness because I believe myself corruption and bribery is greater enemy to the welfare of a people in peacetime than war. I believe myself corruption in a country should be treated in almost the same way as you treat treason. If people cannot have confidence in their own Government, if people can feel that justice can be bought, then what hope are you leaving with the people? The only thing they can do is to take arms and remove that silly Government. They have no other hope..."​

Naomba muongozo wako ndugu mtoa Mada!!! keangu nimetumia kama neno la utani tu, unachokisema ni sahihi sana, wakati mwingine ukifatilia bunge, ni wabunge wachache sana kutoka chama pinzani au chama pinzani kuunga mkono hoja ya chama kingine, hili limekuwa ni la dhahiri sana, wakati mwingine hata uungwaji mkono wa hoja ni wakuonyesha tu sisi ni wengi ni nyinyi ni wachache, ni wabunge wachache sana wenye mtizamo wa kimaslahi ya taifa kama Mama Anna Kilango, wakati mwingine natamani ingekupo hata haja ya kuweka sheria ambayo ita enforce walau wapinzani wapate nafasi ya kuongoza sheghuli za bunge, kama mwenyekit au msaadizi, kwani ianyosemwa ni democrasia yenyewe haijitosholezi ukizingatia wanao tumika kuamua ni watu, pasipo kujali utashi wa kimantiki na umuhimu wa nafasi au jambo.

Adui aliyeongezeka ni RUSHWA. Lakini mimi siamini kama UJINGA bado ni adui kwa jamii ya Watanzania wa leo; kuna watoto wadogo hivi leo kukwea pipa mpaka China na elimu yao ya Std VII ni kawaida bado utawaita hao ni wajinga?

Kwa maoni yangu maadui waliobaki ni
1) RUSHWA
2) UMASKINI (unaosababishwa na namba moja)
3) MARADHI (yanayosababishwa na namba 2)

Tukiangamiza RUSHWA tutakuwa na rasilimali za kutosha kukabili UMASKINI wa Watanzania na hivyo kuwajengea uwezo wa kuangamiza MARADHI

Na MAZOEA YA WATANZANIA KWA CHAMA HIKI NI JANGA LINGINE LA TAIFA. Jamani tujifunze kutokana na historia, hili lichama limekwisha jifia, 2015 tulizike!

Nadhani mtaniunga mkono kuwa wakati Mwl J.K.Nyerere anapata Uhuru wa Nchi hii alitangaza kuwa tunakabiliwa na maadui WATATU ambao ni, NJAA, UJINGA na MARADHI ila kwa bahati mbaya sana kwa mtazamo wangu na kwa watanzania wenye mtazamo kama wa kwangu ni dhahili mtakubaliana na mimi kuwa kwa sasa maadui hao wameongezeka na adui aliyeongezeka anaitwa adui ''UCHAMA''

Nasema UCHAMA ni adui wa nne kwasababu ya kile kinachoendelea ''SERIKALINI'' hasa huko Bungeni Dodoma maarufu kama mjengoni, imekuwa ni nadra sana kwa wafanya maamuzi wetu (Wabunge) kuweka maslahi ya taifa hasa katika maamuzi ya msingi, Kama utakuwa makini jambo hili lazima likutie shaka

Ni mangapi yamekuwa yakifanyika kinyume na maslahi ya TAIFA badala yake yanafanyika kwa maslahi vyama?, hoja Binafsi ngapi zinazimwa bungeni ''ETI'' kulinda heshima ya chama?, Wabunge wangapi wanazomewa bungeni hasa wakisema juu ya maslahi ya wananchi?, Wabunge wangapi wakionyesha nia thabiti ya kutetea maslahi ya Wamanchi wanazimwa na Wakuu wa vyama vyao?

Ni rahisi sana kujibu maswali hayo hapo juu na jibu ni rahisi kuwa kwa mwendo huu hatuwezi kupiga hatua maana ''UCHAMA'' imekuwa ndiyo nongwa kwa maendeleo yetu
Nawasilisha kwa uchungu!!
hapo nikweli wla hakuna ubishi

sema adui wa 4 ni CCM...!.mbona nnazunguka namna hiyo? Kuna wengine tulikosa elimu ya privilage inayotolewa na sirikali hatutakuelewa!

Adui aliyeongezeka ni RUSHWA. Lakini mimi siamini kama UJINGA bado ni adui kwa jamii ya Watanzania wa leo; kuna watoto wadogo hivi leo kukwea pipa mpaka China na elimu yao ya Std VII ni kawaida bado utawaita hao ni wajinga?

Kwa maoni yangu maadui waliobaki ni

1) RUSHWA

2) UMASKINI (unaosababishwa na namba moja)

3) MARADHI (yanayosababishwa na namba 2)

Tukiangamiza RUSHWA tutakuwa na rasilimali za kutosha kukabili UMASKINI wa Watanzania na hivyo kuwajengea uwezo wa kuangamiza MARADHI

Vincent, ujinga bado ni adui! Mfano, mkubwa fulani akidanganya na wewe ukasema amedanganya, wewe ndio utakayeonekana una makosa na siyo aliyedanganya. Kama huu siyo ujinga ni nini? Kwenye daladala dreva akiendesha vibaya na ukatokea kulalamika kuwa anaweza kusababisha ajali, utasikia baadhi ya abiria wanasema: "ajali zimepangwa na Mungu. Kama Mungu hajapanga hata kama akiendesha vibaya hakuna ajali itakayotokea." Na huyo mlalamikaji akitaka kuchukua hatua mfano kwenda polisi anakosa ushirikiano kabisa kutoka kwa abiria wenzake ambao wanamgeukia na kuanza kusema "ana matatizo binafsi." Kama huu siyo ujinga ni nini? Kwa hiyo adui ujinga bado anaitesa jamii ya watanzania.

True

Ndugu Watanzania huwa tunapenda kulalamika ooh,adui ameongezeka wakati adui tumemuongeza wenyewe,pale tuliporuhusu chama kile kile cha ccm kiendelee kutawala.Tungepigia chama kingine kikashika hatamu mi nadhani tusingelalamika.Hata tusemeje ccm iko palepale haitaruhusu muwadhalilishe japo ni mada kweli inawalenga.Wee baba ni baba hawezi chezewa

Nukuu:...hakuna skl thabiti inayoendesha nchi bila kukusanya kodi,nchi zote zilizotoa kipaumbele ktk hili leo zinapiga hatua mf.Italia wamefanya hili ! ! na mkishakuwa na serikali corrupt hamuwezi kukusanya kodi bali mtawawatumikia wakubwa..mtawawambia nini ! ?.Watakujibu tu ahaaa unaniambia hivyooo basi kesho cji ! !.Serikali corrupt itabaki kukimbizana na vikodi vidogo vidogo tu kv barabarani basi !...hii ni sawa na ile niliyosema ya ubaguzi ukianza ubaguzi ile dhambi ya ubaguzi itakuandama tu na haitakuacha...mwisho wa nukuu.Now ktk hapa adui halisi ni nani kati ya corrupt,wakubwa,nyumba waliomo wakubwa au dhambi ?

Ni dhahiri wakati wa Nyerere watu walifunzwa kwamba inawapasa kupiga vita maadui watatu wakuu yaani UJINGA,UMASKINI na MARADHI ili wajikwamue kimaendeleo, lakini sasa Adui wameongezeka kwa idadi hadi kufikia wanne kama ifuatavyo CCM,UJINGA,MARADHI na UMASKINI.Kwa adui wa kwanza sasa ni adui mbaya zaidi kuwahi kutokea kwani ni chimbuko la ufisadi na chemchem ya ukosefu wa haki.
Adui huyu wa kwanza kwa kujitambua kuwa ni adui ametafuta A.K.A yake anajiita kuwa ni adui nyoka aliyejivua GAMBA,HIvyo basi ni wito umetolewa kwa Watanzania wote WAZALENDO na WENYE AKILI TIMAMU kupambana vilivyo na maadui hawa WANNE.

Mimi bado natafakari hivi nia ya uhuru wa Tanzania nini? La pili ni kwamba Nyerere kweli alishindwa vipi kujua hatari ya hiki chama chake? Wengi tunajua maradhi na hiki chama ccm ni makubwa na tuyazuie kabisa yasiendelee kuambukiza generations zingine. Lets stop them now...

Back
Top Bottom