MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA - 9th Dec 2021

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,295
2,000
Nilikuwa kwenye sherehe ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, haya ni baadhi tu ya maendeleo ya nchi yaliyopatikana kwa muda takribani miaka 8 tu baada ya kuutoa madarakani uongozi wa CCM, Rais wa wakati huo (Simtaji jina kwa sasa) anahutubia wananchi siku ya 9/12/2021 uwanja wa Taifa anaanza namna hii.

HIMA HIMA ------ Wananchi wote -- Tanzaniaaaaa
HIMA HIMA -------
Wananchi wote -- Tanzaniaaaaa

Ndugu wananchi, Leo hii ni baada ya miaka 6 tu ya uongozi wetu tangu 2015 tulipopewa mamlaka kuongoza dola, tukiwa sasa kwenye mwaka wa kwanza wa awamu hii ya Pili ya uongozi wetu nafurahi kuwatangazia wananchi baadhi ya mambo muhimu yaliyopatikana chini ya uongozi wetu!!

1. Kila mwananchi sasa ana bima ya afya, Hospitali na zahanati zote zinatoa huduma bora za afya.
2. Shule za Serikali zimerudisha hadhi yake ya kutoa Elimu bora, Elimu ya Msingi hadi Sekondari ni BURE: Vyuo vikuu vyote vya Umaa vinatoa elimu bora; migogoro na malalamiko ya mikopo nk yamepatiwa ufumbuzi wa kudumu.
3. Kila kijana anayehitimu shule ya msingi / Sekondari ambaye hakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya juu anaingia kwenye program maamlum ya Taifa ya ELIMU YA UFUNDI
4. Kila mwananchi anaishi makazi bora, hii ni baada ya kutoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi kwa wakulima vijijini
5. Reli mpya ya kisasa toka Dar - Mwanza - Kigoma, ambapo unasafiri kwa saa 4 tu toka Dar kwenda Mwanza / Kigoma inafanya kazi wa ufanisi.
6. Migogoro ya wakulima na wafugaji iliyodumu tangu tunapata uhuru wetu mwaka 1961 sasa imepatiwa suruhisho la kudumu.
7. Kwa mara ya kwanza taifa letu limewatambua WAKULIMA na WAFUGAJI kama wadau wakuu katika kukuza uchumi wa taifa letu.
8. Migogoro yote ya Ardhi, nafurahi kuwatangazia wananchi kwamba imepata ufumbuzi wa kudumu - Kila mwananchi ana haki ya kumiliki ardhi yake.

Ndugu wananchi, haya yote yametokana na kazi kubwa sana ya kudhibiti mapato na matumizi ya Serikali kuu, Serikali za Majimbo, pamoja na ushiriki wenu wananchi kuikataa na kutokomeza kabisa RUSHWA ambayo iliota mizizi miaka kumi iliyopita hasa wakati taifa linaingia kwenye uwekezaji pamoja na mikataba hasa ile ya maliasiri kama Madini, Misitu, Wanyama nk

Wananchi sasa baada ya kutokomeza hawa maadui watatu, yaani Ujinga, Maradhi na Umaskini waliowasumbua baba na mama zetu kwa miaka zaidi ya 52 ya uhuru wetu - sasa natanganza rasmi kwamba tunaingia kwenye MAPINDUZI YA VIWANDA, kwa lugha ya kigeni wanaita industrial Revolution; Mapinduzi haya ya viwanda katika nchi yetu yatahusu mabadiliko makubwa katika kilimo, utengenezaji wa bidhaa, Uchimbaji wa madini yetu na uchukuzi na masoko. Ndugu Wananchi ..........


.....itaendelea...


Let it be true..... bado nina imani na nchi yangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom