Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), iilianzishwa rasmi Disemba 17, 1968 ambapo Disemba 17, 2018 Bakwata itatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Maadhimisho ya miaka 50 ya baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA yana lengo la kuwapa picha halisi waislamu wa Tanzania walipotoka na wanakoelekea ili hatimaye kujenga umoja wa kweli baina ya waislamu kimkakati.
Maadhimisho hayo kufanyika jijini Dar es salaam kwa mambo yafuatayo;
1. Kongomano maalumu la siku moja litakalo fanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo Disemba 16, 2018.
2. Michezo ya viongozi wa kiislamu ikiwa pamoja na mpira wa miguu katika uwanja wa Jakaya Kikwete kuanzia alasiri, Disemba 16, 2018.
3. Maandamano makubwa (Zafa) Disemba 17, 2018 saa 9 alasiri kuanzia makao makuu BAKWATA mpaka ukumbi wa Diamond Jubilee.
5. Sherehe ya halaiki kwenye ukumbi huo wa Diamond Jubilee kuanzia saa 10 jioni baada ya maandamano makubwa (Zafa)
Watakao hudhuria Kongomano maalumu kutoka mikoani ni viongozi saba wenye sifa kama watakavyoelekezwa na Katibu mkuu wa Bakwata. Pamoja na waalikwa wengine watakaoalikwa kuwakilisha taasisi mbalimbali za kiislamu au kijamii.
Watakaohudhuria maandamano (Zafa) ni waislamu wote wapenda maendeleo ikiwa pamoja na wawakilishi wa Mikoa, Misikiti, Madrasa, Zawiya, Shule au kikundi chochote cha wapenda maendeleo ya waislamu na jamii kwa ujumla kutoka mkoa wowote nchini Tanzania.
Watakaohudhuria maandamano (Zafa) ni pamoja na watu wengine muhimu na mashuhuri wakiongozwa na viongozi wa Serikali na BAKWATA.
Mufti wa Sheikh Abubakar Zubairy bin Ally anaziomba Taasisi mbalimbali pamoja na Misikiti, Madrasa na Zawiya pamoja na vyuo vikuu na vyuo vikuu vya kiislamu kushiriki kwa hali na mali katika maadhimisho hayo.
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA ni chombo cha waislamu wote nchini, hivyo mnaombwa waumini wote wa kiislamu kushiriki kikamilifu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA bila kujali Taasisi na madhehebu
Wabillah Tawfiq.