Maadhimisho ya miaka 100 ya Ujasusi wa Urusi.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,273
Leo 10/11/2018 dunia ya Ujasusi inaungana na Urusi katika kuadhimisha miaka miamoja ya Ujasusi katika taifa hilo, Najaribu kuangazia jambo hili katika miimo ya kijasusi katika kurejea nyuma zaidi na kuyakuta mazalia mtawalia ya ukongwe wa Mji wa Sevastopol nchini Urusi ulioanzishwa tarehe 14 June 1783 miaka 236 sasa. Kila jasusi wa Urusi anapomaliza mafunzo yake kabla ya kuanza kazi rasmi hufunzwa kwa kutamka juu ya mji wa Sevastopol kwamba "Это место России в военную доблесть & славы, дорогие сердцам всех россиян" kwa lugha ya kitumwa (It is a place of Russia's military valour & glory, dear to the hearts of all Russians)

Eneo hili ndio moyo wa taifa la Urusi katika kuiangaza Urusi pande zote za nchi hiyo, ndiomaana pengine ni sababu tosha ya kuwalisha maneno hayo watumishi wa kada ya ujasusi wa shirika la ujasusi la FSB. Nchi yoyote duniani lazima iwe na kitu kinaitwa pin point, na kwa Urusi tangu miaka 235 iliyopita, mji huo ndio pin point yao, achilia mbali miji yenye mapori maalumu ya mafunzo ya kijasusi ya Zabaikalsk- Manzhouli, pia muundo huu unaweka utaratibu wa kila wizara, shirika, taasisi nk ya serikali lazima iwe na mwakilishi wa shirika la Ujasusi (person contact) wa FSB, wao wanaita jasusi mwangalizi. Mfano katibu wa wizara ya kilimo akiwa na jambo haendi moja kwa moja kwa waziri wake, ni lazima awasiliane na mtu wa ujasusi wa ngazi inayolingana na yeye, pia waziri haendi moja kwa moja kwa rais mpaka kwanza ashauriwe na mtu wa ujasusi.

Muundo huu haupo mbali, nchini Tanzani wakati Tawi Maalumu (SB) linaundwa baada ya uhuru na Mwalimu Nyerere hasa baada ya maasi ya 1964, mfumo ulibadilika kutoka ule wa Waingereza kwamba kila mkuu wa shirika/taasisi au wizara kuripoti kwa mkuu wa Nchi, na kuuweka uwe wa Kirusi ambapo kila wizara/shirika au taasisi ikawa na afisa usalama mwangalizi, leo mfumo unafanya kazi kwenye mashirika na taasisi tu, umeakisi mifumo ya FSB.

Lakini msingi wa "pin point" bado umesalia kuwa imara ambapo Zanzibar ni division no 1, na Dar ni 2, Tabora no 3 nk.. Zanzibar ni eneo mtawalia la kimbinu kwa Tanzania, Ili uilinde Tanganyika pande zote ni lazima usimame Zanzibar, na Ili uilinde Urusi yote ni lazima usimame Sevastopol,

Mageuzi aliyoyafanya Rais Boris mwaka 1994 yaliubadili mfumo wa ukusanyaji taarifu, jina la shirika na uendeshaji wa shirika la ujasusi la FSB ambalo awali liliitwa KGB, kutoka kuhami siasa za madaraka ya chama tawala na kwenda kwenye kuhami uchumi.

Hayo yalitukia Januari mwaka 1994, aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin, aliunda upya Shirika la Kijasusi nchini humo, maarufu kama FSB. Ikumbukwe kwanza, KGB ni kati ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani yaliyopata kutambulika. Mwaka 1983, kwa mfano, Jarida la Time liliripoti kuwa shirika hilo ni bora zaidi katika kukusanya taarifu za kijasusi.

Wakati Boris Yeltsin akiwa madarakani, KGB ilikuwa chini ya Wizara ya Usalama ya Urusi ikiongozwa na Jasusi gwiji wa medani kamanda Vladimir Putin. Uamuzi huo wa kuvunja wizara na shirika hilo lenye rekodi ya ubora duniani, linatusogeza katika swali la msingi. Je, kwa nini Yeltsin alichukua uamuzi huo? Kwa nini aliamua hivyo tena akipuuza rekodi kongwe na bora ya shirika hilo?

Maelezo yaliyotolewa nyuma ya uamuzi huo ni kwamba shirika hilo halikuweza kukabili changamoto za mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa kama alivyotaka Rais. Kwa lugha nyingine, KGB ilikuwa kikwazo kwa Rais Yelstin kuongoza nchi kwa kasi aliyoitaka hususan mabadiliko ya msingi ya kiuchumi na kisiasa.

Kwa sasa njia za uchumi kwa kiwango kikubwa zipo chini ya udhibiti wa shirika jipya la Ujasusi la SFB na pia biashara kubwa mbili muhimu kwa Urusi yaani biashara ya silaha na biashara ya Mafuta duniani vipo chini ya shirika la Ujasusi la FSB na Idara ya Ujasusi jeshini.

NB: Zingatia sio shirika la ujasisi ndilo linalofanya biashara moja kwa moja, bali makampuni yote makubwa nchini Urusi yanasaidiwa (Info's) na kulindwa na Shirika la Ujasusi la Urusi popote duniani yalipo, na zaidi nikuwa maslahi ya nchi kwanza mengine baadae....... Huo ndio ujasusi wa Kiuchumi ulivyo tunaposherekea miaka miamoja ya Ujasusi ya Urusi ya GRU, KGB na FSB.....

Wenzetu wakiwa wanasherekea mafanikio GRU KGB na FSB, sisi huku nchi ya kusadikika na vyombo vyetu vya dola tupo busy na kuangalia nani kaandika mtandaoni maneno ya sio kipendeza chama cha mapinduzi na mwenyekiti wake, wala hatuna habari na mikataba ya hovyo ya raslimali, wala hatuna habari na ufisadi, wala hatuna habari na usalama wa raia na mali zao, wala hatuna habari na kuporomoka kwa uchumi wa nchi.

Kwa undani zaidi soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola ma Kiuchumi kwa ofa maalumu ya 56,000 popote ulipo unaletewa.

+255715865544
+255755865544

Na Yericko Nyerere

FB_IMG_1541838059741.jpg
150px-Emblema_KGB.svg.png
 
View attachment 928582View attachment 928583
:cool:
 
Back
Top Bottom