Stopper3
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 625
- 1,030
Habari za wikiendi,
Rejea kichwa cha habari hapo juu.
Kumekuwa na michezo michafu inaendelea maabara za afya huku mtaani katika suala la UKIMWI.
Ipo hivi, kuna kasumba ukipata mpenzi/ mchepuko/ kipozeo basi mnachukuana kwenda kupima afya kwanza ili mkienda kwenye 5*6, 6*6 mjiachie wenyewe bila kutumia kondomu.
Mnapofika Maabara kunakuwa na kamchezo wanacheza hawa wapimaji wasio waadilifu na mpenzi/mchepuko/kipozeo wako, hapa usipokua makini unaenda kuungwa gridi ya taifa.
Mpenzi/ mchepuko/ kipozeo wako anaweza kumuandikia ki memo mpimaji akaambatanisha na noti ya TSH 10,000 au 5,000. Kimemo kinaweza kusomeka hivi "Mimi najijua nimeathirika, hivyo tumia damu yake kutoa majibu yetu sote"
Hicho ki memo anakua amekiandika muda, akifika hapo anakua anamkanyaga mtoa huduma, hivyo mtoa huduma atajiongeza tu. Kimemo kitaachwa mezani wakati mnanyanyuka kusubiri majibu.
Wengine wanawahi kutangulia maabara "kumseti" mtoa huduma, anmtoa kidogo anatumia damu ya mtu mwingine, anaipima kabisa kisha kipimo kinahifadhiwa ndani.
Ukiachana na mchezo huo mchafu wa maabara kuna wadada wanatembea na vipimo ambacho kinasoma Negative kabisa, kumbe yeye ni Positive.
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app