Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari Wandugu
Ni matumaini yangu mu wazima.
Ni jana tarehe 08/01/2018, baraza la mitihani la taifa lilitangaza matokeo ya upimaji ya kidato cha pili na darasa la nne. Mimi pia nikiwa ni mdau wa elimu, nikaona vyema niingie kwenye website yao niangalie maendeleo ya vijana wetu. Jambo la kushangaza tangu jana majira ya saa kumi jioni mpaka sasa naandika uzi huu sijaweza kuingia kwenye website ya NECTA. Majibu ni "the site you are requesting can't be reached". Maana yake nini; yawezekana website hii ipo katika marekebisho au imedukuliwa na kufungiwa na washenzi.
Hii ni aibu kwa wataalam wa IT wa taasisi hii. Wanajisikia je Watanzania wanapohangaika ku-access website yao. Kama hampo vizuri kwenye IT security ni bora kuleta watu wenye uwezo mkubwa ili kupambana na changamoto za IT. IT si lelema, inabidi kuwa current haswa kwa sababu hizi ndizo zama zake, kila siku kuna mbinu na utaalam mpya. Sasa kama nyinyi mmejifungia tu huko maofisini na kula viyoyozi mtateswa na hackers.
Ni bora nimesema kuliko kubaki na maumivu.