Ma-genius tukutane hapa

Ma-genius tukutane hapa

Shule zlikuwa kibasila,Azania,forodhani,kambangwa,,jangwani,zanaki,kisutu........tuliomalza 1997.
Hapo tambaza O level ilishaondolewa
Kama Kuna shule nmeisahau mtajazia
 
SEHEMU YA TATU.
Baada ya kurudi shule mwezi wa 3 huo nikapiga Msuli wa kufa mtu Namshukuru mungu necta nikapiga paper fresh nikapiga Div 2 ya mwanzo , Nikapangiwa Shule Iringa kusoma Comb ya EGM, kwenda huko iringa Piga Msuli, nikapata div 1 ya 8, nikachaguliwa UDSM Kozi ya Barchelor of arts in Economics mpaka hapo nlipograduate miaka kadhaa nyuma, now tupo tu bado hatujafikia malengo kwa asilimia 100 ila ndo tunaelekea huko, namshukuru mungu.

Hizi ni kumbu kumbu tu, now maisha ni kitaa tofauti na yale maisha ya shule maarifa yako ndo yatakayokusaidia mtaani.
KARIBUNI.
A genius is someone with extraordinary intellectual or creative abilities.In terms of IQ, genius has IQ of 140 (one person out of 240 people) or IQ f 180(one person out of 2,000,000 people)
Wee jamaa kujiita genius unafit walau hizo criteria?Au uliweza tu kukariri yaliyoandikwa na kina NEWTON na kuja kudanganya hapa?
 
kipindi hicho tution kwa dani kule mburahati madoto na mabibo kwa brather anaitwa yule jamaa...
 
Nimepata faraja kuona shule yangu pendwa ya primary ikitajwa...ni hakika kabisa miongoni mwa shule za msingi za serikali zenye kuheshimika Gilman Rutihinda hautoweza kamwe kuiacha nyuma, nilisoma miaka hiyo Mwalimu Mkuu akiwa ni Madame Songambele, alikuwa ni mpenda maendeleo kuanzia taaluma hadi mandhali ya shule. Mungu awabariki waalimu walionifundisha pale.
 
Habari za wakati huu,

Maisha ya uanafunzi hua na mapito mengi ila all in all hukuacha na kumbukumbu nyingi mbaya na nzuri sana, pengine zisizosahaulika maishani.

Leo naomba tu-share experince tofauti tofauti za kitaaluma na kimaisha tulizopitia kuanzia primary, secondary, Advance na maybe chuo,ukorofi, utundu, usela, mtu kuongoza darasa zima, kuwa tatu bora au kumi bora uliwezaje kufikia mafanikio hayo, ni msuli kazi, tuition, walimu wazuri class, marafiki watoboaji au ulikuwa na ndugu waliosoma

Hakuna kitu kizuri kama uwe mwanafunzi unayefanya vizuri darsani almost ni top 10 ndo huwa among'st the best in the class.

PRIMARY SCHOOL.
Wakati naanza darasa la kwanza sikusoma nursery nilianza moja kwa moja primary Mtoto wa kimaskini sijui A wala E na sikuwa na ndugu msomi hata mmoja ila balaa nililolifanya hapo primary bado watanikumbuka.

Mtihani wa kwanza wa mwezi wa sita nlikuwa mtu wa 30's hivi kati ya wanafunzi 180's. Nilikuwa naona kawaida tu kuja mwezi wa 12 nikaja kuwa mtu wa 42 nakumbuka nilifungua report nikafuta ile 2 ikabaki 4 nikapeleka nyumbani na hawakujua kitu.

Gari likaanza kuwaka taratibu kuingia darasa la pili mwezi wa sita nikawa wa kwanza watu shangwe unaitwa assemble pale siku ya kufunga shule mtu nyomi unapewa mazawadi mpaka raha yaani na umaarufu unaanziaga hapo.

Tukaenda wa 12 nakumbuka nlikuwa wa 7 nikasemwa sana home kwanini umefeli mwenyewe nilikuwa naona kawaida tu maana huwa sisomi nikirudi mimi ni kucheza mpira, goroli tu.

Baada ya hapo sasa balaa kubwa ndo likaanza tukaingia darasa la tatu mwezi wa sita nikawa wa kwanza, wa kumi na mbili wa kwanza, kuingia darasa la nne mwezi wa sita wa kwanza wa taifa wa kwanza, darasa la tano mwezi wa sita wa kwanza, mwezi wa kumi na mbili wa kwanza, nikawa maarufu sasa mtaa mzima, kuingia darasa la sita tukaanza na kufanya mitihani ya interschools ya kushindana shule na shule hapo nikawa nauwasha balaa tulianzia mock kata nikawakimbiza kata nzima shule kama 4 hivi, kuna shule moja ilikuwa iko vizuri sana kwa darasa la saba kipindi hiko inaitwa Gilman Rutihinda ipo Kigogo siku hiyo Jumamosi moja tukatoka na washkaji zangu wawili tukaenda pale piga pepa nikawa wa pili na marafiki zangu walibahatika kuingia top ten tu na wao ila mwisho mwisho hivi.

Mitihani yote ya darasa la sita ya mwezi wa sita na mwezi wa kumi na mbili nilikuwa wa kwanza. Tukaingia la saba hapa kwa kiasi fulani nilikuwa napiga msuli na nilikuwa nishajielewa piga sana pepa za kushindana nilikuwa sitoki top 3 mara nyingi tukishindana hata kama ni shule kumi.

Ila Kuna viumbe niliwapigia Salute ( MAGENIUS ) kuna jamaa mmoja alikuwa akiitwa David Mlay na jamaa mwingine alikuwa akiitwa Mateso, hawa jamaa walikuwa magenius balaa kipindi hiko. Huyu Mlay yeye tulifanya mitihani mingi ya kushindana ila sijawahi kumpita alikuwa kata jirani na mimi, Huyu Mateso yeye ndo alikuwa balaa alikuwa anajulikana sana shule za Manzese na Kinondoni yake

Kuna siku tulienda kufanya mtihani wa kushindana zikaja shule 40 hapo shuleni kwao kulikuwa na shule mbili zote tukazitumia bwana siku hiyo nilijua watu wanajua tulifanya jamaa akawa wa kwanza ana marks 240 out of 250 mimi mjomba nina 210'S huko nilichobahatika nikaingia kwenye first page ila hata top ten sikuwepo. Walitoa matokeo ya walioingia karatasi ya kwanza tu, ila kuna kijana wangu mmoja kutoka shuleni kwetu alikuwa wa tatu marks 230'S. Tuliendelea kufanya mitihani mingi ya kushindana ila mpaka karibu na necta. Necta darasa la saba tokeo nilikuwa wa 3 kishule ila nilipata matokeo mazuri tu average A kwenye 200+

Kilichoniuma sikubahatika kupangiwa shule ya vipaji boarding nikaishia kupangiwa Kibasila ambayo kwa dsm ndo miongoni mwa special schools zetu,

1. Mateso yeye alienda Ilboru
2. Mlay alienda Loyola
Magnus Ngole mhh umenikumbusha mabali kwa kuwa jina langu liliandikwa kwenye kila shule wakati huo mkoa wa dsm primary.any way ni mapito tu.
 
Ila ilikuwa marks 150
 
Dah nakumbuka Aron kandoro alvyotukimbza pale Kwa ibunga tuition center(mabibo) mwaka 1997 dogo alkuwa anasoma mlimani primary school.....
Kidato Cha kwanza alchaguliwa ilboru hakwenda akaenda zake mzizima,form four akapga one point 7,,,akapangiwa tena ilboru akapotezea,akaendelea mzizima comb pcm,form six akatia one point 3.....
Salute to him!!!!
Huyo jamaa ni nouma sana

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
kipindi hicho tution kwa dani kule mburahati madoto na mabibo kwa brather anaitwa yule jamaa...
Yule Dani alkuwa hatar,,pindi bila kuangalia notes enzi zle altuchanganya sana.....
Tulikuwa tunamuona jamaa wa ajabu!!!!
 
Hivi ambao hatukuwahi kuwa wa kwanza ila 5-9 consistently Sekondari yote darasa la around wanafunzi 120 na kunyoosha division I kali ni majiniasi, au tuna akili tu za darasani?
 
Na sisi tuliosoma shule ya kata na kupata one yenye A ya Basic Mathematics kisha kuna dvision three 4, four 26 na division 0 154 tusemeje? Mpaka leo hiyo sekondari hiyo hakuna amevunja recod yangu.
Baadaye watu walinipiga vita kuwa ni mbinafsi sana.
Leo hii sitaki mtu ajue hata nilimaliza four 4 hasa majirani wapya hapa sitaki kabisa kuitwa msomi na kama nilifika chuo kikuu ni siri yangu
 
Wilaya ya Njombe na Mdete pr. niliacha kumbukumbu pale haatasahau jina langu kwa kuibeba shule na kuongoza wilaya nzima ukiachana na mitihani ya ndani na inter school huko usiulize
 
O-LEVEL ( Mambo Yakaanza Kubadilika)

Baada ya kupangiwa kibasila high school hapo Temeke sikufurahi kabisa yani niliona wamenionea sana mimi nilihitaji nipelekwe shule yeyote ya boarding mkoani na kwa bahati mbaya kilikuwa kipindi kibaya maishani mwangu baba yetu alipata mitihani mikubwa sana maisha yakawa magumu mno tulikuwa tukiishi nyumba ya kupanga mzee akashindwa kulipa kodi alikuwa ana boma lake kibaha huko akauza kwa bei ya hasara then akaenda kununua shamba mkuranga, alipofika kule alifikia kwa jamaa yake mmoja akampa hifadhi kwenye moja ya nyumba zake za udongo na hela alokuwa nayo mzee asingeweza kumudu kujenga nyumba kama nyumba ilibidi na yeye ajenge nyumba ya miti tena mdogo mdogo maana hela yenyewe naona ilishaanza kuisha. kule shamba alienda na mama na watoto kama wawili maana sehemu ya kukaa kulikua hakuna, Sisi wengine tulitawanywa kwa ndugu na jamaa mjini, Baada ya muda kidogo mama yetu alianza kuumwa sana ( Figo zilifeli, akapofuka macho, alikonda sana kbla alikuwa mnene kiasi ) mzee akazidi kuchanganyikiwa na kuacha kutufikiria sana wanae.

Picha linaanza mimi nlipelekwa kwa jamaa yake mmoja hapo nyumbani kwake alikua ana garage yake vijana wake wanafanya kazi jamaa alichojali ni hiyo garage
Jamaa alikuwa hanijali kabisa nauli sipewi kula kwa shida shule nikawa siendi mara kwa mara. Roho ilikuwa inaniuma sana nikawa sina la kufanya, midterm ikapita sikufanya mtihani wa kumwambia sina mzee yeye hata kutokea pale hatokei. Nilikaa pale mpaka mwezi kama wa tisahivi form 1 ndo nikaondoka pale nlitoroka nikajipeleka kwa mama mmoja alikuwa jirani yetu zamani, Kukaa pale na kwenyewe ilikuwa balaaa unafanya kazi zote ndani wewe, sipewi nauli ya shule, kula kwa tabu, kusingiziwa wizi mpaka majirani ndo wakawa wananisaidia saidia kidogo tu nikaona hapa mimi shule basi nkamaliza form one perfomance ilikuwa ni mbovu ila nlikuwa mtu wa kati kati yaani nlikuwa sisomi kabisa, darasani nlikuwa ndo hvo siingi lakini nlikuwa nkifanya mitihani yeyote nilipata 30- 60 najibia uelewa wangu binafsi tu, nkaingia form two nkahama hayo maeneo nkawa nakaa na mabraza tu wa mitaani nikajitahidi ili nianze vizuri kidogo shuleila bado changamoto zilikuwa nyingi hasa kukosa nauli ya shule uniforms na baadhi ya ada za shule nyingine, So nkaendelea kibishi tu na Automatically nkaanza kama kuichukia shule utoro ukaongezeka sana kuna wenzangu nlienda nao pale kibasila walikuwa among Geniouses wa pale kibasila mpaka wakawa wananishangaa jamaa yetu kakutwa na nini?
Form two mwendo huo huo mbovu mpaka mwezi wa nane mzee alikua ana kijana wake mmoja hivi anakaa vingunguti (brother Hoki) god bless you. Japo jamaa alikuwa maskini sana lakini alijitahidi sana kunisaidia, alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha mikate akilipwa sh 5000 - 6000 per day,ila alikiwa akinipa nauli na hela za misosi japo ni ndogo sana ila alinisaidia kwa miezi ile mitatu tu nilipiga msuli wa kufa mtu necta form 2 nikajitahidi kiasi maana pale wanaojua niwengi ila nlipata wastani wa 68 out of 100 masomo 11. Kuingia form three nikapangiwa science nikapania sana na nikaanza vizuri nlikua nakaa na bro wangu mmoja hivi alikua anajitahd kunisapot nikawa nasoma sana na napiga tuition mchikichini, mwanzo mtihani wa kwanza kufanya ulikuwa midterm form 3 nakumbuka mathematics ulikuwa mgumu sana ule mtihani nikapiga banda, Phys pia Banda , baada ya hapo mambo yakaanza kubadilika pia nikaanza utoro kias hela ya kwenda mchikichini sina, Tukaenda mwezi wa sita pia nikajitahidi kiasi tu ila baada ya pale majanga yakaanza tena nlienda kukaa na brather mwengine yeye alikuwa hana maisha kabisa kwa hiyo nikaanza kuunga unga tena, mwisho wa siku nikaichukia kabisa shule masimango ya wanafunzi wenzangu na walimu yakanishinda nkahamia kwenye magame ps nkawa master ps mitaani, nikaanza kuwa kama watoto wa mitaani jioni naenda kwenye vigodoro. Nakumbuka mara ya mwisho form 3 kwenda shule ilikuwa mwezi wa 8, baada ya hapo si kwenda tena shule mpaka walimu walipompigia mama yangu mdogo kuwa wananiulizia nipo wapi washamaliza kusajili wanafunzi kwa ajili ya necta, Ndo na wao wanashtuka kuwa nlikua siendi shule maana hapo kati nlikuwa nkipiga simu nawaambia naenda shule kama wanapata hela japo kwa mwezi mara moja wananitumia, Wakafunga safari kutoka mkoani mpaka dar, kunipeleka shule.
Itaendelea
Pole Sana!
 
SEHEMU YA TATU.
Baada ya kurudi shule mwezi wa 3 huo nikapiga Msuli wa kufa mtu Namshukuru mungu necta nikapiga paper fresh nikapiga Div 2 ya mwanzo , Nikapangiwa Shule Iringa kusoma Comb ya EGM, kwenda huko iringa Piga Msuli, nikapata div 1 ya 8, nikachaguliwa UDSM Kozi ya Barchelor of arts in Economics mpaka hapo nlipograduate miaka kadhaa nyuma, now tupo tu bado hatujafikia malengo kwa asilimia 100 ila ndo tunaelekea huko, namshukuru mungu.

Hizi ni kumbu kumbu tu, now maisha ni kitaa tofauti na yale maisha ya shule maarifa yako ndo yatakayokusaidia mtaani.
KARIBUNI.
Hongera! Ulifanikiwa shughuli au ajira baada ya chuo?
 
Back
Top Bottom