Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 6,383
- 8,273
Ngoja kwanza nimalizie kucheki mechi ya Watani wa Jadi, ndio nifikirie kuja kuusoma huu uzi!
Huelewi maana ya geniusHabari za wakati huu,
Maisha ya uanafunzi hua na mapito mengi ila all in all hukuacha na kumbukumbu nyingi mbaya na nzuri sana, pengine zisizosahaulika maishani.
Leo naomba tu-share experince tofauti tofauti za kitaaluma na kimaisha tulizopitia kuanzia primary, secondary, Advance na maybe chuo,ukorofi, utundu, usela, mtu kuongoza darasa zima, kuwa tatu bora au kumi bora uliwezaje kufikia mafanikio hayo, ni msuli kazi, tuition, walimu wazuri class, marafiki watoboaji au ulikuwa na ndugu waliosoma
Hakuna kitu kizuri kama uwe mwanafunzi unayefanya vizuri darsani almost ni top 10 ndo huwa among'st the best in the class.
PRIMARY SCHOOL.
wakati naanza darasa la kwanza sikusoma nursery nilianza moja kwa moja primary Mtoto wa kimaskini sijui A wala E na sikuwa na ndugu msomi hata mmoja ila balaa nililolifanya hapo primary bado watanikumbuka. mtihani wa kwanza wa mwezi wa sita nlikua mtu wa 30's hivi kati ya wanafunzi 180's. nlikua naona kawaida tu kuja mwezi wa 12 nikaja kuwa mtu wa 42 nakumbuka nlifungua report nikafuta ile 2 ikabaki 4 nkapeleka nyumbani na hawakujua kitu. Gari likaanza kuwaka taratibu kuingia darasa la pili mwezi wa sita nikawa wa kwanza watu shangwe unaitwa assemble pale siku ya kufunga shule mtu nyomi unapewa mazawadi mpaka raha yaani na umaarufu unaanziaga hapo. Tukaenda wa 12 nakumbuka nlikuwa wa 7 nikasemwa sana home kwa nini umefeli mwenyewe nlikua naona kawaida tu maana huwa sisomi nkirudi mimi ni kucheza mpira, goroli tu. Baada ya hapo sasa balaa kubwa ndo likaanza tukaingia darasa la tatu mwezi wa sita nikawa wa kwanza, wa kumi na mbili wa kwanza, kuingia darasa la nne mwezi wa sita wa kwanza wa taifa wa kwanza, darasa la tano mwezi wa sita wa kwanza, mwezi wa kumi na mbili wa kwanza, nikawa maarufu sasa mtaa mzima, kuingia darasa la sita tukaanza na kufanya mitihani ya interschools ya kushindana shule na shule hapo nikawa nauwasha balaaa tulianzia mock kata nkawakimbiza kata nzima shule kama 4 hivi, kuna shule moja ilikuwa iko vizuri sana kwa darasa la saba kipindi hiko inaitwa Gilman Rutihinda ipo kigogo siku hiyo jmosi moja tukatoka na washkaji zangu wawili tukaenda pale piga pepa nikawa wa pili na marafiki zangu walibahatika kuingia top ten tu na wao ila mwisho mwisho hivi. Mitihani yote ya darasa la sita ya mwezi wa sita na mwezi wa kumi na mbili nlikuwa wa kwanza. Tukaingia la saba hapa kwa kiasi fulani nlikua napiga msuli na nlikuwa nshajielewa piga sana pepa za kushindana nlikua sitoki top 3 mara nyingi tukishindana hata kama ni shule kumi.
Ila Kuna viumbe nliwapigia Salute ( MAGENIUS ) kuna jamaa mmoja alikuwa akiitwa david Mlay na jamaa mwingine alikuwa akiitwa mateso hawa jamaa walikuwa magenious balaa kipindi hiko. Huyu mlay yeye tulifanya mitihani mingi ya kushindana ila sijawahi kumpita alikua kata jirani na mimi, Huyu mateso yeye ndo alikuwa balaa alikuwa anajulikana sana shule za manzese na kinondoni yake kuna siku tulienda kufanya mtihani wa kushindana zikaja shule 40 hapo shuleni kwao kulikuwa na shule mbili zote tukazitumia bwana bwana siku hiyo nilijua watu wanajua tulifanya jamaa akawa wa kwanza ana marks 240 out of 250 mimi mjomba nina 210'S huko nlichobahatika nkaingia kwenye first page ila hata top ten sikuwepo. walitoa matokeo ya walioingia karatasi ya kwanza tu, ila kuna kijana wangu mmoja kutoka shuleni kwetu alikuwa wa tatu marks 230'S. Tuliendelea kufanya mitihani mingi ya kushindana ila mpaka karibu na necta. Necta darasa la saba tokeo nlikuwa wa 3 kishule ila nlipata matokeo mazuri tu average A kwenye 200+
kilichoniuma Sikubahatika kupangiwa shule ya vipaji boarding nikaishia kupangiwa Kibasila ambayo kwa dsm ndo miongoni mwa special schools zetu,
1. Mateso yeye alienda Ilboru
2. Mlay alienda Loyola.
Nia si kujisifia ila ni kumshukuru Mungu.
Kaaahhh!!kumbe umesoma juzi hapa marks 250!!mitihani siku 2
Hata hongera sana dog all the best huko uliko
Inawezekana maana, maana mimi mwenyewe nawajua watu wengi ambao walishawahi kufanya vizuri primary ila baadae wakaja kuzingua olevel, na wengine walishawahi fanya vizuri olevel wakzingua primary, mimi mwenyewe baada ya kumaliza primary ndo nikaumaliza mwendo at least advance nlijitahidi ila bado ilikuwa kawaida kwa hiyo mambo hubadilika.Huyo Mwanao Mateso kama alienda Ilboru basi alikua muangalia Tv tu hakufanya maajabu yoyote coz pale Ilboru ukifika unasikia Story zote za Magenious toka miaka ya 70 na mimi nimesoma pale tena Currently ila sikuwahi sikia jina la Mateso.
Na wewe huenda ulienda kua kama Mwanao tu ulivyoenda secondary.
Wengine tumesoma ilboru kabisa tunaona kawaida tuKama hujasoma Mzumbe, Ilboru, Tabora boys au Kibaha unapata wapi ujasiri wa kujiita genius?
Yeah ukisoma pale Ilboru/Mzumbe/Tboys au kibaha huwez ijua Brand Ukiwa Ndani ila toka sasa Mwenyewe Nimepita Ilboru pale.Wengine tumesoma ilboru kabisa tunaona kawaida tu