Ma-Doctor na watambuzi hebu nijuzeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ma-Doctor na watambuzi hebu nijuzeni

Discussion in 'JF Doctor' started by FirstLady1, Aug 24, 2011.

1. FirstLady1

FirstLady1 JF-Expert Member

#1
Aug 24, 2011
Joined: Jul 29, 2009
Messages: 16,575
Likes Received: 541
Trophy Points: 280
Hivi kama hapo nyuma ulijifungua kwa Operation na watoto wote watakaofatia inakuwa ni operation pia ?

FL1

2. Lizzy

Lizzy JF-Expert Member

#2
Aug 24, 2011
Joined: May 25, 2009
Messages: 22,224
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
Sio lazima...inategemea na sababu ya mtu kufanya hivyo mara ya kwanza!!Kama kulikua na complications wataangalia mara inayofuatia ikiwa zitakuwepo au la...kama hazitakuwepo basi unaweza kutumia njia ya kawaida!

Na kama ulifanya vile tu bila kua na matatizo yoyote mara ya pili waweza kuamua kutumia njia ya kawaida.

3. FirstLady1

FirstLady1 JF-Expert Member

#3
Aug 24, 2011
Joined: Jul 29, 2009
Messages: 16,575
Likes Received: 541
Trophy Points: 280
nakushukuru sana my dear Lizzy kwa kunielewesha

Maana naplan sasa nianze mikiki ya kuiongeza dunia ila nikawaza mmh first time haka ka binti kangu kalinitesa mpaka nukasema naapa sitarudia tena Ila sasa nimetamani tena ndo najiuliza hivi next baby mungu akinijaalia itakuwaje tena?

4. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#4
Aug 24, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 234
Trophy Points: 160
Kama alivyokueleza dada Lizzy, kurudia tena kujifungua kwa caesarean section (c/s) kunategemea na sababu iliyopelekea ukajifungua kwa njia hiyo in the first place.

Kuna sababu tunaziita 'absolute indication', ukiwa na hii basi uzazi wako wote utakuwa kwa c/s. Sababu hizi zinajumuisha mwanamke kuwa mfupi sana chini ya 150cm, mara nyingi hawa nyonga (pelvis) yao inakuwa ndogo kuweza kuruhusu an average baby to pass kutonana na kutowiana kati ya kitangulizi cha mtoto na nyonga (cephalo-pelvis disproportion (CPD)); mwanamke mwenye ulemavu unaoathiri sehemu ya nyonga na hivyo mtoto hawezi kupita; na kama ulishajifungua kwa c/s mara 2 au zaidi.

Lakini sabau nyingi za c/s huwa sio lazima zijirudie...mfano mtoto mkubwa, kitovu kutokeza nje ya uke kabla mtoto hajazaliwa (cord prolapse), mtoto kuchoka (hii ni sababu mara nyingi sana), uchungu kuchukua muda mrefu sana (prolonged labor), kifafa cha mimba, kitangulizi cha miguu (breech presentation), kupasuka kizazi etc..

Kwa sababu ambazo si lazima zijirudie, daktari/mkunga anaweza kumpa mama mjamzito nafasi ya kujifungua kawaida kwa uangalizi wa karibu huku ukimpima mara kwa mara mama kuhusu maendeleo yake ya uchungu na uwezo wa kovu la kwenye kizazi lililotokana na c/s ya uzazi uliopita kuhimili uchungu, tunaita 'trial of scar'. Ila sharti hapa ni kuwa mama huyo awe amejifungua kwa c/s si zaidi ya mara moja.

5. FirstLady1

FirstLady1 JF-Expert Member

#5
Aug 24, 2011
Joined: Jul 29, 2009
Messages: 16,575
Likes Received: 541
Trophy Points: 280
thanks Riwa Nadhani nina urefu mzuri tu wa haja na pia tatizo langu mtoto aligoma kabisa kugeuka na alikaa vibaya tumboni mpaka hatua za mwisho miezi ya saba na nane nikawa chini ya uangalizi wa Ma DR mpaka pale nilipofanikiwa kujipatia kababy kangu salama salimi ingawa kwa operation
Ila sasa napenda kuongeza baby mwingine..Naomba msaada wa kimawazo labda ni mazoezi gani natakiwa kufanya katika kipindi chote hicho ili isijejirudia kama mwanzo
natanguliza shukrani ..

6. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#6
Aug 24, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 234
Trophy Points: 160
tatizo hilo lililopelekea ukafanyiwa c/s sio absolute...sio lazima kuwa next pregnancy mtoto atakaa tena vibaya. hivyo utafanyiawa trial of scar ambapo unazalia hospitali chini ya uangalizi wa karibu wa daktari. wengi tu wameshajifungua kawaida baada ya c/s katika uzazi wa kwanza.

7. Sajenti

Sajenti JF-Expert Member

#7
Aug 24, 2011
Joined: Apr 24, 2008
Messages: 3,673
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
..Riwa kuna wanawake wengine wanadai hawapendi kujifungua kwa njia ya kawaida eti kukwepa maumivu so hupenda kuzaa kwa operation. Nina mtuninaye mfahamu ana watoto wawili wote aliomba mwenyewe azalishwe kwa operation na tumbo ukiliona utadhani binti wa miaka 12...

8. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#8
Aug 24, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 234
Trophy Points: 160
Yeah, zamani ilikuwa vigumu kidogo, lakini siku hizi na maobstetrician wamejaa tele, na mwanamke ana haki ya kuomba services stahiki...wapo kadhaa ambao wanaopt c/s kuepuka uchungu! na wanahudumiwa, lakini kwenye private hospitals zaidi..

9. Nyalotsi

Nyalotsi JF-Expert Member

#9
Aug 24, 2011
Joined: Jul 20, 2011
Messages: 5,104
Likes Received: 552
Trophy Points: 280
hiyo trial of scar uwe na private doc, kwenye hospital za mh jk utaishia kurupture uterus. B careful with ur next pregnancy!

10. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#10
Aug 25, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 234
Trophy Points: 160
Ahsante Nyalotsi kwa kulileta hili...maana ya trial of scar ni hapo kwenye kupima uwezo wa hilo kovu kwenye kizazi lililotokana na uzazi uliopita kwa operation, na kuona kama litaweza himili uchungu wa uzazi husika. Unahitaji uangalizi wa karibu wa daktari au nesi/mkunga mzoefu ambaye mara kwa mara atapima strength ya hilo kovu against progress ya labor, ili usifikie hali ya kuchanika kizazi (kurupture uterus). Kwa kweli kama hamna uwezekano wa uangalizi wa hali ya juu....don't try the scar!

11. Rubi

Rubi JF-Expert Member

#11
Aug 25, 2011
Joined: Oct 5, 2009
Messages: 1,623
Likes Received: 48
Trophy Points: 145
Hivi wewe ni yuleyule FL1 au ni pacha wako maana yule wa zamani kuna siku kama kichwa changu kizuri ingawa avata mpya ila jina ni lilelile alikuwa akipongwezwa katikia siku yake ya kuzaliwa na kuulizwa umri akasema ana miaka 40 (2years imepita kama sikosei) na tena akasema anakaribia kupata wajukuu. au wajukuu ndo hao watoto wa uzeeni? Ufafanuzi please.

By the way kila la kheri.

12. FirstLady1

FirstLady1 JF-Expert Member

#12
Aug 26, 2011
Joined: Jul 29, 2009
Messages: 16,575
Likes Received: 541
Trophy Points: 280
hahaha Rubi bado ni ka safari karefu ka kufika 40 mungu anisaidie
Labda wakati najibu hiyo post nilikuwa na hangover
Mbona umepotea sana mpendwa
Miss you big time

13. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#13
Aug 26, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,508
Likes Received: 2,250
Trophy Points: 280
heeh! mi nilitaka nikuambie unipe dawa ya ku-rewind! all the best. kuna ndugu yangu alijifungua kwa njia ya kawaida a year after kufanyiwa operation ya kutoa mtoto aliefia tumboni wa miezi sita na uvimbe mkubwa sana. tatizo lake alikuwa na maumivu sana ya mshono,ila kujifungua ilikuwa chapchap,uchungu 2 hrs then kitu mwake. kama ukiwa active, unatembea na kupanda ngazi u will be ok. kila la kher mpenzi

14. FirstLady1

FirstLady1 JF-Expert Member

#14
Aug 26, 2011
Joined: Jul 29, 2009
Messages: 16,575
Likes Received: 541
Trophy Points: 280
thanks swirry ngoja sasa nianze harakati wish me luck

15. Nyalotsi

Nyalotsi JF-Expert Member

#15
Aug 26, 2011
Joined: Jul 20, 2011
Messages: 5,104
Likes Received: 552
Trophy Points: 280

kuna msemo wa kwenye vtab unasema First caeserian section alwayz controverse badala ya alwayz c/s..be careful coz medical issues never read books. unaweza kukutana nayo ww tofaut na wa2 walivyozoea!

16. Visenti

Visenti JF-Expert Member

#16
Aug 26, 2011
Joined: Jul 24, 2008
Messages: 1,031
Likes Received: 17
Trophy Points: 133
Mkuu Riwa amechanganua vizuri sana, kwa kuongeza, kanuni nyingine ni kuwa, kama umepata siza mbili (C/S) bila kujali sababu zilizopelekea , uzazi wa tatu lazima iwe C/S!, kwa lugha nyingine ni kuwa kama una 2 previous C/S, hiyo ni ABSOLUTE indication ya C/S kwa mimba inayofuata, na C/S ya tatu inaambatana na kufungwa kizazi permanently hata kama mimba zote umekosa watoto, though in rare circumstances unaweza pewa nafasi nyingine but under very close monitoring.

17. FirstLady1

FirstLady1 JF-Expert Member

#17
Aug 28, 2011
Joined: Jul 29, 2009
Messages: 16,575
Likes Received: 541
Trophy Points: 280
nina moja tu hata hivyo nawashukuru wote kwa ushauri kwa vile ninae Gyna wangu pia iyabidi nijaribu kuongea nae zaidi
Mbarikiwe

18. S

Sista Sophia Member

#18
Aug 29, 2011
Joined: Feb 6, 2010
Messages: 52
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Una kumbu kumbu nzuri sana wewe, hata mimi nakumbuka alisema ana 40s tena kuna kipindi alisema hata kuolewa alichelewa. Kweli humu JF kuna watu wala si wa kuwaamini wanachoongea. Sasa una 40 wataka kuzaa mtoto mwingine wa nini?

19. FirstLady1

FirstLady1 JF-Expert Member

#19
Aug 29, 2011
Joined: Jul 29, 2009
Messages: 16,575
Likes Received: 541
Trophy Points: 280
Sister Sofia unajua hapa Ndani kuna Ma FL wawili kwa hiyo mmoja anaweza kuongea mkadhani ni mie, hata sikumbuki tena kama nilisema nina miaka 40 labda was joking
mama unajua hapa JF sio kila info ni ya kuamini sana ..kuna wakati mtu anakuuliza katika Jokes na wewe unajibu hivo hivo ,kuna wakati mtu anakuuliza akiwa serious na wewe unajibu hivo hivo..
Lakini mie sio mzee kivile jamani .. bado niko kwenye mkakati wa kuongeza familia..

karibu kwangu Sister Sofia

20. nachid

nachid JF-Expert Member

#20
Aug 31, 2011
Joined: Apr 14, 2011
Messages: 898
Likes Received: 50
Trophy Points: 45

my wyf mara ya kwanza ni operation thn second tym madoctorz wakaniambia lazima iwe operation it waz last year, mke wangu hakuwa na tatizo lolote bt baada tu ya kucheck mshono ndo ikawa tabu

Loading...