M4C yashika kasi Geita

M4C yashika kasi Geita

Nakwambia mwaka huu,
NYOKA ANAPIGWA MTAMA AKIAMKA ANAKIMBIA,
SISIMIZI ANAPIGWA KWENZI NA HAFI ANAVUMILIA,
TEMBO ANAKALISHWA KWENYE KIGODA NA MAKALIO YANAENEA NA BATA ANAONGEZEWA.
 
uploadfromtaptalk1368285054219.jpg
Huyu ndo diwani wa Kata ya Kalangalala Mhe. Kagoma, akiwa na Katibu wa CHADEMA Geita.
 
Huyu ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Geita ambaye amevua gamba na kuvaa gwanda mapema mwaka huu akihutubia umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa M4C.Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Kiukweli,huyu Daudi Sunzu Katwale Ntinonu,ni mtu wa uhakika ambao HADEMA wamebahatika kumpata na hasa katika harakati hizi za kukitengeneza chama,ni mtu mwenye msimamo katika ukweli,ni mtu asiyependa Rushwa wala mishiko kama ile ambayo tumekuwa tukisikia inatolewa kwa baadhi ya viongozi wa CCM na hasa wakati wa uchaguzi ndani ya chama,ni mtu ambaye anajisimamia na akiamua ameamua huwa arudi nyuma.Hizi ni badhi ya sifa ambazo zilimfanya achukiwe na badhi ya viongozi wa CCM na hasa wale wa ngazi za juu,wakati huo Katibu Mkuu akiwa Yusuf Makamba alimjengea Bifu na tangu hapo wakaanza kumvuruga kila kona,ana upeo mkubwa sana katika masuala ya siasa.

Kama CHADEMA watamtumia vizuri na hasa katika Mkoa wa Geita tunaweza kusema mengine kwenye uchaguzi ujao,na kwa sasa kuna kundi lake kubwa sana ambalo linajipanga hivi sasa kwenda CHADEMA kumfuata ili kuunganisha nguvu waliyokjuwa nayo ndani ya CCM ana kundi kubwa wakiwemo viongozi wa ngazi mbalimbali,na kama wakienda walahi nakwambieni CCM itakuwa na wakati mgumu sana uchaguzi ujao kwa sababu ni kwanza ni kundi kubwa,lakini pili ni watu wenye misimamo na uwezo pia wa kifedha(wana shughuli zao halali zinazowapa kipato),kufikiri,na kujituma.
 
Watu wakichangia vuguvugu,ni kweli kwamba watu wameichoka CCM.
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1368296149563.jpg
    uploadfromtaptalk1368296149563.jpg
    70.8 KB · Views: 57
Nimeishi sana Geita naifahamu vilivyo na nimetoka huko kuja hapa Dar katikati ya mwaka jana,ni vigumu sana kwa CHADEMA kuchukua kata ya Kalangalala kwa sababu kwenye eneo hilo bado watu wana ushabiki wa mdomoni lakini sio wa moyoni.nasema hivyo kwa sababu mwaka wa Chadema kuchukua jimbo hilo ilikuwa ni uchaguzi wa mwaka 2010 uchaguzi uliomuingiza madarakani Donald Max,huyu Max alikuwa hapendwi hata ha WanaCCM wenzake na walitoa ushirikiano Mkubwa sana kwa CDM lakini mwisho wa siku wakashindwa,natambua kwamba Max harudi Bungeni uchaguzi ujao lakini jimbo ni vigumu kwenda CDM isipokuwa litachukuliwa na mtu mwingine kupitia CCM.

Kata ya Kalangalala iko chini ya CHADEMA na nadhani umemuona Mheshimiwa Diwani.
 
Katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Geita Ignas karashani akihutubia mkutano,anasema Chadema imekuja na Mwarobaini wa matatizo ya watanzania.
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1368296278208.jpg
    uploadfromtaptalk1368296278208.jpg
    102.1 KB · Views: 57
View attachment 93284
Huyu ndo diwani wa Kata ya Kalangalala Mhe. Kagoma, akiwa na Katibu wa CHADEMA Geita.

Kama wewe ni mgeni hapo Geita uliza ili uambiwe usijifanye unajua,Diwani wa kata ya Kalangalala anaitwa Peter Donald na sio Kagoma,kama ulivyoandika,Huyo Kagoma ni Diwani wa Kata ya Buselesele ni Diwani wa kata hiyo tangu mwaka 2000,na mwaka 2010 aliamua kujiunga CHADEMA akitokea CUF ambapo amekuwa Diwani wa Awamu mbili na bado ataendelea kuwa Diwani wa kata hiyo kwa sababu anakubalika,anajituma na anataekeleza wajibu wake,labda tu kama CHADEMA watamvuruga,ni mtu ambaye Dk.Magufuli anamuogopa sana.
 
Kata ya Kalangalala iko chini ya CHADEMA na nadhani umemuona Mheshimiwa Diwani.

Najua hilo na namjua kuliko wewe Mkuu kwa sababu nilimchangia shilingi 500000 kwa ajili ya mafuta wakati wa kampeni zake kwa sababu nilitaka ashinde hiyo kata.lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba akigombea uchaguzi ujao wala hashindi,muulize mwanachadema yeyote hapo Geita na hasa kwenye huo mkutano kama upo,ingawa kata hiyo itaendelea kuongozwa na CHADEMA kwa sababu kuna wajanja,huyu ameshindwa kutekeleza yale ambayo wakazi wa Geita walitarajia,na tayari hivi karibui alijikuta akiingia kwenye tuhuma za fedha za mamlaka ya mji.akapigiwa sana kelele.
 
Katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Geita Ignas karashani akihutubia mkutano,anasema Chadema imekuja na Mwarobaini wa matatizo ya watanzania.

Tatizo la Karashani Bwana ni uroho wa madaraka tu na hili kama kuna kiongozi yeyote wa chadema ambaye atakuwa anatembelea Thread hii na hasa wale wa huko Geita atakubaliana na mimi,kwa sababu moja ya mambo pia yaliyomtoa kwenye chama cha Mapinduzi hapohapo Geita ni uroho wa madaraka,alifika tu Geita akiwa bao mgeni akagombea wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007,aliposhindwa tu akahamia CHADEMA,na hata huko chadema sasa hivi nasikia kuna vuguvugu la madaraka na miongoni mwa watu wanaoliwasha ni yeye,na tayari kuna baadhi ya watu wametimuliwa wilayani hapo kwa sababu zao hizo za kugombea madaraka kwa sababu kila mmoja anaangalia ubunge wa mwaka 2015.
 
kuna jamaa mmoja anaitwa Msukuma ni wa ccm anapendwa sana kupita kiasi,vhadema tuwe makini naye sana.
 
Nakwambia mwaka huu,
NYOKA ANAPIGWA MTAMA AKIAMKA ANAKIMBIA,
SISIMIZI ANAPIGWA KWENZI NA HAFI ANAVUMILIA,
TEMBO ANAKALISHWA KWENYE KIGODA NA MAKALIO YANAENEA NA BATA ANAONGEZEWA.

Mkuu hapa umeniacha sina mbavu.na hiyo id imenifanya nifikri ya kuwa yule msanii wa tanga kafufukia Jf?.
 
Nadhani utakuwa unamzungumzia Karashani mwingine,huyu hawahi kuwa mwanachama wa CCM,na wala hana uroho wa madaraka.
 
Nimeishi sana Geita naifahamu vilivyo na nimetoka huko kuja hapa Dar katikati ya mwaka jana,ni vigumu sana kwa CHADEMA kuchukua kata ya Kalangalala kwa sababu kwenye eneo hilo bado watu wana ushabiki wa mdomoni lakini sio wa moyoni.nasema hivyo kwa sababu mwaka wa Chadema kuchukua jimbo hilo ilikuwa ni uchaguzi wa mwaka 2010 uchaguzi uliomuingiza madarakani Donald Max,huyu Max alikuwa hapendwi hata ha WanaCCM wenzake na walitoa ushirikiano Mkubwa sana kwa CDM lakini mwisho wa siku wakashindwa,natambua kwamba Max harudi Bungeni uchaguzi ujao lakini jimbo ni vigumu kwenda CDM isipokuwa litachukuliwa na mtu mwingine kupitia CCM.
ww ushatoka Geita,sisi tupo hadi mda huu,tunajua na tunayaona yanayotokea.uchaguzi ulopita yaan 2010,matokeo yalichakachuliwa walio wengi tunajua! ukweli watu washaamka sana c kama usemavyo!
 
ww ushatoka Geita,sisi tupo hadi mda huu,tunajua na tunayaona yanayotokea.uchaguzi ulopita yaan 2010,matokeo yalichakachuliwa walio wengi tunajua! ukweli watu washaamka sana c kama usemavyo!

Sikia Mkuu,nimehama Geita lakini nina biashara zangu hapo Geita,Nyarugusu,Lwamgasa pamoja na Nyakagwe,na haipiti wiki sijaja Geita labda kama niko nje ya nchi.kwa hiyo bado mimi ni mkazi wa Geita kwa sababu nimewekeza vitu vingi hapo mjini.Muulize Ntinonu akwambie,naijua Geita vizuri kuliko wewe,nazijua siasa za Geita kuliko wewe,nawajua watu wa Geita kuliko wewe.na siku zote mimi huwa nasimamia ukweli wala sio ushabiki,na mtu yeyote anayeshabikia masuala kisiasa ama kwa mapenzi yake bila kufanya upembuzi yakinifu huwa sielewani nao.so naomba usizungumze kishabiki hapa.Tatizo lenu mmevamia hivi vyama na spidi mpaka mnataka kuwashinda waliovianzisha!.
 
Nadhani utakuwa unamzungumzia Karashani mwingine,huyu hawahi kuwa mwanachama wa CCM,na wala hana uroho wa madaraka.

Mkuu hebu jaribu kutumia akili za kichwani wakati mwingine,samahani lakini kama nitakuwa nimetumia maneno makali.una nafasi tupeane taarifa humu ndani za ikiwa ni pamoja na mustakabali mzima wa siasa za Geita kwa faida ya watu wengine?!
 
Huyu ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Geita ambaye amevua gamba na kuvaa gwanda mapema mwaka huu akihutubia umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa M4C.Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Maelezo yako tuu yanaonesha jinsi gani huzifahamu siasa za Geita mkuu, kama hufahamu hata kama diwani wa kata ya Kalangalala ni wa CHADEMA hatuwezi kuargue!
 
Back
Top Bottom