M4C-OPD ndani ya Geita - Jan 27, 2014

M4C-OPD ndani ya Geita - Jan 27, 2014

@Mods;Mmefanya makosa kuunganisha thread yangu na ile ya Nyang'wale kwani mkutano ninaoleta updates unafanyika Geita mjini hivyo naomba utenganishwe ili habari iwe valid.

teh,teh kutakuwa na mod yupo training,sasa yupo kwny somo la kuunga threads.pole shekulu
 
'ukiwa unafanya usafi lazima vumbi litimke'.sasa tumetoa taka nyumba ni safi.by JJMnyika.Zitto teh,teh,teh
 
Kamanda Mnyika anasema waraka ule ulikuwa na mambo mengi machafu zaidi ya masuala ya uongozi. CCM kupitia mamluki wanataka kuwapandikiza viongozi wa juu ambao hawataitisha maandamano na kufanya mikutano ya kupigania haki za Watanzania.

"Wananchi mko tayari kwa hilooo..hapanaaa" Wananchi mnaounga mkono maamuzi ya chama wanyoshe mikono juu (umati mzima unanyosha mikono juu kuunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza wasaliti. Hatimaye Mhe.Mnyika anamaliza vile muda si rafiki na kudokeza kwamba amepokea waraka wa siri wa CCM wakiratibu kuhujumu uchaguzi wa serikali za mitaa.

Pia anasema wamepokea nyaraka za siri kutoka GGM pamoja na malalamiko ya watumishi wa idara ya afya Geita...CHADEMA itawatetea watanzania wote na kuiamuru serikali kutokusaini mikataba mipya na wawekezaji wanaowadhulumu wana Geita waishio kimasikini wakati kuna utajiri mkubwa hapa.

(Kamanda Mnyika amemaliza na umati unamshangilia kisha anamkaribisha Kamanda Said Issa Mohammed!
 
Niko kwenye mkutano Geita watu ni nyomi, Mbowe amemaliza kuhutubia na ameondoka na amemwacha Mnyika anaendelea kuhutubia.
bahati mbaya ka simu kangu hakana uwezo wa kuweka picha.
Mwombe LEMA Blackberry hapo.
 
@Mods;Mmefanya makosa kuunganisha thread yangu na ile ya Nyang'wale kwani mkutano ninaoleta updates unafanyika Geita mjini hivyo naomba utenganishwe ili habari iwe valid.

Acha kulia lia wewee usimpfundishe mods kzi
 
Niko kwenye mkutano Geita watu ni nyomi, Mbowe amemaliza kuhutubia na ameondoka na amemwacha Mnyika anaendelea kuhutubia.
bahati mbaya ka simu kangu hakana uwezo wa kuweka picha.

Huna lolote upo kwenu kisuji unajishaua upo geita
 
Jamani utoke Kakola,namba 9,Lushimba,Kanegele,Bumanda hadi Kharumwa kwa mguu. Acha uongo, shenzytype.

Watu hawa wanahamu ya ukombozi, mimi natoka huko Nyarugusu wameamka kwa kweli, uchaguzi ujao jembe na nyundo wajipange vinginevyo hali ni mbaya. Pia watu kutembea umbali huo inawezekana maana wako komited. Mbona hujahoji yule jamaa alie endesha baiskeli kutoka Geita hadi Magogoni dar kwa baiskeli? Au umesahau? Hoji sasa kama ni kweli!!!
 
Thread zikija magamba wanapata taabu kuchangia.Lakini hali yenyewe ndiyo hiyo,mmepoteza hela bure kumpa Zito,lakini bhakti mbaya haijazaa matunda.Na kijana mjuaji katawanya hela yote hawezi hata kurudisha.
 
...UPDATES;

Kamanda Said Issa Mohammed anasema muda wa mkutano umeisha na wandishi wa habari ni mashahidi lakini mimi sifanyi mkutano bali naanza darasa na darasa halina mwisho hata kama ni saa nane usiku.

"Makamanda chama chenu kipo salama...(umati unapiga makofi).Wenye hila wanatafuta namna ya kuua chama lakini wameshindwa. CHADEMA si chama cha Wakristo wala Waislamu,si chama cha wachaga wala wapemba...! CHADEMA ina viongozi wa dini zote,kabila zote na kanda zote. Kamanda Mohammed anasema Quran inasema anayemwamini Mungu haachi kuwa mtiifu kwake hata kama Imamu aliyekuwa anampenda amefukuzwa msikini.

Kama kuna wanaCHADEMA waliokuwa watiifu wa Zitto na siyo CHADEMA, kama wanao ukweli mwingine zaidi ya usaliti uliotendeka basi waondoke nae (watu wanashangilia kwa nderemo na vifijo.

Hatimaye Kamanda Issa Mohammed amemaliza huku akiacha gumzo Geita kwa hoja zake nzito. Anauamsha umma kwa kusema CCM... Wananchi wanajibu kwishaaaa!
 
CHADEMA katika jimbo la Kigoma Kaskazini.

1. 2000 walikuwapo madiwani 11.
2. 2005 walipungua na kubakia sita(6)
3. 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili(2)

My take
Kama hii hali ingefumbiwa Macho, 2015 Kungekuwa na Madiwani Sifuri Kabisa na hata Jimbo kulipoteza.

M4C - OPD Ndio Talk of the Town (Habari ya Mujini) Kwa Sasa
 
Hasira zenu haziwezi kuubadili ukweli, Chadema kwa sasa ni kama wanateleza hivi, hawazuiliki wananikera kutokumsamehe zitto, hilo tu

mkuu anasamehewa aliyeomba msamaha....zitto na kibuli chake cdhan ka anaweza kuomba samahan......!!!!!!
 
Kamanda Mnyika amekuwa lulu kwa wachimbaji wadogo pale aliposema, "askari wanaotumika na mafisadi kuwapiga risasi vijana wenzetu wanaojitafutia riziki kwenye magwangala ni ni vilaza na wanatakiwa kuacha mara moja"
 
Chadema ndani ya Geita ni nouma, balaaa tupu. Mbowe, Mnyika, Salim, Waitara wametisha jamani natamani mngekuwepo mjionee wenyewe 1390843054083.jpg 1390843054083.jpg
 
M4C - OPD Katiba ( UnderCover Chafua Zitto ). Kwanini msimalize Katiba Mpya kisha Mkaja na OP Maalum kwa ajili Yake? Issue Close kwa Walalahoi ila bado Hot kwa Wenye Vyeo. Mnatuchanganya.
 
Kamuche; Unajichanganya mwenyewe kutokana na kutokuwa na msimamo au uelewa finyu.Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa hapa Geita ni kuhusu katiba mpya,rasilimali za taifa na maendeleo kwa taifa, kuheshimu utu na thamani ya kila raia wakiwemo wachimbaji wadogo, kupiga vita propaganda za udini,ukabila,ukanda,rangi n.k Wewe unachanganywa na lipi?
 
Last edited by a moderator:
Mbowe kasema kama noma na iwe noma, awa Magamba lazima wang'oke, kiukweli kama wanageita tunaahidi kutoa support ya kutosha awa jamaaa waendeee tumechoka, takwimu alizotoa Mnyika juu ya dhahabu zilizovunwa na mgodi wa GGM ukilinganisha na pato ambalo serikali limepata toka mwaka 2000 ni aibu hata kuweka hizo figure hapa jukwaani!!

Picha ya hapo chini ni wananchi wakimpokea mheshimiwa Mbowe akiwa anatua na Chopa, ilibidi askari wafanye kazi ya ziada kuwazuia wananchi wadikaribie sana Chopa kwa sababu za kiusalama!!!
 

Attachments

  • 1390843903377.jpg
    1390843903377.jpg
    43.9 KB · Views: 71
Back
Top Bottom