M4C-OPD ndani ya Geita - Jan 27, 2014

M4C-OPD ndani ya Geita - Jan 27, 2014

kanumbu: kisimu nilichotembea nacho hakiwezi ku upload picha but mtazipata muda si mrefu. Ningependa nidokeze uwepo wa Kamanda J.J.Mnyika a.k.a Waziri Mkuu wa Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mhe.Said Issa Mohamed. Usalama umeimarisha, upande wa kusini mwa jukwaa nawaona polisi wamesimama kwa mbali huku wakimsikiliza Mhe.Mbowe!
 
Last edited by a moderator:
kanumbu: kisimu nilichotembea nacho hakiwezi ku upload picha but mtazipata muda si mrefu. Ningependa nidokeze uwepo wa Kamanda J.J.Mnyika a.k.a Waziri Mkuu wa Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mhe.Said Issa Mohamed. Usalama umeimarisha, upande wa kusini mwa jukwaa nawaona polisi wamesimama kwa mbali huku wakimsikiliza Mhe.Mbowe!

Chadema ni raha tupu..
 
Last edited by a moderator:
...UPDATES:

Mhe.Mbowe anadokeza kwamba CHADEMA inamjenga kila raia wa taifa hili kujiamini na kutetea haki bila kuogopa chochote.

"Ndiyo maana kipindi kile Spika wa bunge Makinda alijaribu kutumia ubabe kuzima hoja zetu lakini walishindwa. Baadaye Kikwete alituita ikulu tukaenda Mimi Mbowe,Mhe.Mbatia na Prof.Lipumba. Kikwete alituomba tusitishe maandamano ya umoja wa vyama vya upinzani nchi nzima nasi tukasimama tukamwambia sharti madudu yaliyopitishwa na wabunge wa CCM kuhusu bunge la katiba yatupiliwe mbali na turudi tena bungeni kujadili...Rais Kikwete kwa kuogopa nguvu ya umma na ukweli uliojulikana wazi alikubaliana na msimamo wetu na matunda yake ni hii (ameonyesha rasimu ya katiba mpya)" Wananchi wanashangilia.

Mhe.Mbowe anaongeza kwamba CCM walifikia hatua ya kumtuhumu Mhe. Warioba eti anachukua maoni ya CHADEMA tu alipopendekeza serikali tatu,je hayakuwa maoni yenu wananchi? (Watu wanamshangilia Mhe. Mbowe huku wengine wakisema CCM ilikufa na Nyerere).
 
Khaaaa kumbe serikali ina helkopta moja mmmmmmhhhhhhiiiiii
 
@Mods;Mmefanya makosa kuunganisha thread yangu na ile ya Nyang'wale kwani mkutano ninaoleta updates unafanyika Geita mjini hivyo naomba utenganishwe ili habari iwe valid.
 
kanumbu: kisimu nilichotembea nacho hakiwezi ku upload picha but mtazipata muda si mrefu. Ningependa nidokeze uwepo wa Kamanda J.J.Mnyika a.k.a Waziri Mkuu wa Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mhe.Said Issa Mohamed. Usalama umeimarisha, upande wa kusini mwa jukwaa nawaona polisi wamesimama kwa mbali huku wakimsikiliza Mhe.Mbowe!

EEE BHANA EEE NIMECHELEWA SANA KUJUA KAMA MNYIKA KUMBE NI WAZIRI MKUU wa DAR ES SALAAM ! ASANTE KWA TAARIFA KAMANDA !
 
Last edited by a moderator:
...UPDATES: Mhe.Mbowe anadokeza kwamba CHADEMA inamjenga kila raia wa taifa hili kujiamini na kutetea haki bila kuogopa chochote."Ndiyo maana kipindi kile Spika wa bunge Makinda alijaribu kutumia ubabe kuzima hoja zetu lakini walishindwa.Baadaye Kikwete alituita ikulu tukaenda Mimi Mbowe,Mhe.Mbatia na Prof.Lipumba.Kikwete alituomba tusitishe maandamano ya umoja wa vyama vya upinzani nchi nzima nasi tukasimama tukamwambia sharti madudu yaliyopitishwa na wabunge wa CCM kuhusu bunge la katiba yatupiliwe mbali na turudi tena bungeni kujadili...Rais Kikwete kwa kuogopa nguvu ya umma na ukweli uliojulikana wazi alikubaliana na msimamo wetu na matunda yake ni hii (ameonyesha rasimu ya katiba mpya)" Wananchi wanashangilia. Mhe.Mbowe anaongeza kwamba CCM walifikia hatua ya kumtuhumu Mhe.Warioba eti anachukua maoni ya CHADEMA tu alipopendekeza serikali tatu,je hayakuwa maoni yenu wananchi? (Watu wanamshangilia Mhe.Mbowe huku wengine wakisema CCM ilikufa na Nyerere).

HAKIKA KILA ANAYETU UPDATE MAMBO HAYA MUNGU atamlipa , UBARIKIWE MKUU .
 
UPDATES;

Mhe.Mbowe anaongeza kwamba katiba ni mali ya wananchi hivyo ni kufirisika sera kwa CCM kudai eti msimamo wao ni serikali mbili.

Anasema tunaelekea kwenye bunge la katiba, tunajua tuko wachache lakini tunaenda kupambana kufa na kupona kusimamia maslahi ya taifa.Katiba hii ianishe wazi namna rasilimali za taifa zitakavyowafaidisha wananchi, dhahabu ya Geita iwafaidishe wanageita...Kila mwananchi aheshimiwe na kulindwa kwa mujibu wa katiba hata kama ni masikini,kilema au mnyonge...(wananchi wanashangilia).

Anasema endapo "tutashindwa kwa uchache wetu tutarudi kwenu wananchi...tunaomba mtuunge mkono...(makofi yanapigwa kila upande).

Kamanda Mbowe anasema CHADEMA inajua hila za CCM, wanatumia magazeti yao kama Jamboleo, Mzalendo na uhuru wakipamba eti CHADEMA kuna mgogoro wakati lengo ni kuwapotosha wananchi wasahau mambo ya msingi kama katiba eti wamzungumzie Zitto, "Hili si level yangu namwachia Mhe. Mnyika kijana mwenzake"

Mhe. Mbowe anamaliza kwa kusema CHADEMA itahakikisha daftari la kupiga kura!
 
Pamoja daima,naipenda chadema na viongozi wake&wanacdm wote.
 
...UPDATES:

Mhe.Mbowe amemaliza kuongea kisha amepanda chopa kuelekea Mwanza. Hatimaye Mbunge wa Ubungo, Kamanda J.J.Mnyika anapanda jukwaani na kushangiliwa na umati mkubwa wa watu. Kamanda Mnyika anasema "ikiwa unafagia nyumba yako lazima vumbi litatimka lakini baadaye litatulia.

Zitto ni rafiki yangu tangu siku nyingi tangu 1999 chini ya taasisi NATIONAL FORUM iliyokuwa inahamasisha vijana wajiunge na siasa. Serikali ikafutilia mbali taasisi yetu. Hadi kipindi hicho Zitto hakuwa mwanachama wa CHADEMA lakini nikamshawishi na akajiunga na CHADEMA kisha tukagombea ubunge kama vijana mwaka 2005 ambapo mwenzangu alishinda lakini mimi niliibiwa kura na kesi kuzungushwa mahakamani kisha niliapa CCM wao ndio watakaohangaika mahakamani mwaka 2010 kwamba wameibiwa kura na ikawa hivyo(watu wanashangilia)." Mhe. Mnyika anasema, mwaka 2009 nilinasa mawasiliano kati ya Zitto na Mhariri mmoja wakilenga kukivuruga chama.
 
Niko kwenye mkutano Geita watu ni nyomi, Mbowe amemaliza kuhutubia na ameondoka na amemwacha Mnyika anaendelea kuhutubia.
bahati mbaya ka simu kangu hakana uwezo wa kuweka picha.
 
Back
Top Bottom