M4C-OPD ndani ya Geita - Jan 27, 2014

M4C-OPD ndani ya Geita - Jan 27, 2014

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,395
Reaction score
1,112
Previously:

Kwa hisani ya Bwana Rogers J Ruhega, Kaimu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Geita

Wanachama wote wa CHADEMA na wote wapenda mabadiliko na uhuru wa kweli, wazalendo wote na wapenda maendeleo wa Geita, mnakaribishwa sana na mnaomba kuendelea kuwaalika wengine katika mkutano huo mkubwa sana wa kufungua mwaka utakaofanyika Geita mjini ndani ya kata ya kalangalala.

Mkutano huo utafuatiwa na kikao cha baraza la mashauriano la CHADEMA Mkoa wa Geita litakalokuwa na lengo kubwa la kutathimini shughuli ya ujenzi wa chama kupitia programe ya CHADEMA ni msingi ndani ya majimbo yote sita yaliyomo ndani ya Mkoa wa Geita.

Wadau; muda na eneo husika la wapi mkutano utakapofanyikia tutazidi kufahamishana jinsi siku zinavyozidi kukaribia, please stay tuned!

Mwaka 2014 ni mwaka wa maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya ukombozi mkuu wa uhuru wa mara pili 2051.

Updates:

Hatimaye Kamanda wa anga awasili kwa helikopta na umati mkubwa unamshangilia Mhe.Mbowe. Hali ya hewa si nzuri sana kwani mvua imenyesha na manyunyu yanaendelea lakini watu wanazidi kumiminika kuja katika uwanja wa magereza hapa Geita Mjini. Nitakuwa nawapa kila updates!
...UPDATES:

Mhe.Mbowe anadokeza kwamba CHADEMA inamjenga kila raia wa taifa hili kujiamini na kutetea haki bila kuogopa chochote.

"Ndiyo maana kipindi kile Spika wa bunge Makinda alijaribu kutumia ubabe kuzima hoja zetu lakini walishindwa. Baadaye Kikwete alituita ikulu tukaenda Mimi Mbowe,Mhe.Mbatia na Prof.Lipumba. Kikwete alituomba tusitishe maandamano ya umoja wa vyama vya upinzani nchi nzima nasi tukasimama tukamwambia sharti madudu yaliyopitishwa na wabunge wa CCM kuhusu bunge la katiba yatupiliwe mbali na turudi tena bungeni kujadili...Rais Kikwete kwa kuogopa nguvu ya umma na ukweli uliojulikana wazi alikubaliana na msimamo wetu na matunda yake ni hii (ameonyesha rasimu ya katiba mpya)" Wananchi wanashangilia.

Mhe.Mbowe anaongeza kwamba CCM walifikia hatua ya kumtuhumu Mhe. Warioba eti anachukua maoni ya CHADEMA tu alipopendekeza serikali tatu,je hayakuwa maoni yenu wananchi? (Watu wanamshangilia Mhe. Mbowe huku wengine wakisema CCM ilikufa na Nyerere).

UPDATES;

Mhe.Mbowe anaongeza kwamba katiba ni mali ya wananchi hivyo ni kufirisika sera kwa CCM kudai eti msimamo wao ni serikali mbili.

Anasema tunaelekea kwenye bunge la katiba, tunajua tuko wachache lakini tunaenda kupambana kufa na kupona kusimamia maslahi ya taifa.Katiba hii ianishe wazi namna rasilimali za taifa zitakavyowafaidisha wananchi, dhahabu ya Geita iwafaidishe wanageita...Kila mwananchi aheshimiwe na kulindwa kwa mujibu wa katiba hata kama ni masikini,kilema au mnyonge...(wananchi wanashangilia).

Anasema endapo "tutashindwa kwa uchache wetu tutarudi kwenu wananchi...tunaomba mtuunge mkono...(makofi yanapigwa kila upande).

Kamanda Mbowe anasema CHADEMA inajua hila za CCM, wanatumia magazeti yao kama Jamboleo, Mzalendo na uhuru wakipamba eti CHADEMA kuna mgogoro wakati lengo ni kuwapotosha wananchi wasahau mambo ya msingi kama katiba eti wamzungumzie Zitto, "Hili si level yangu namwachia Mhe. Mnyika kijana mwenzake"

Mhe. Mbowe anamaliza kwa kusema CHADEMA itahakikisha daftari la kupiga kura!

...UPDATES:

Mhe.Mbowe amemaliza kuongea kisha amepanda chopa kuelekea Mwanza. Hatimaye Mbunge wa Ubungo, Kamanda J.J.Mnyika anapanda jukwaani na kushangiliwa na umati mkubwa wa watu. Kamanda Mnyika anasema "ikiwa unafagia nyumba yako lazima vumbi litatimka lakini baadaye litatulia.

Zitto ni rafiki yangu tangu siku nyingi tangu 1999 chini ya taasisi NATIONAL FORUM iliyokuwa inahamasisha vijana wajiunge na siasa. Serikali ikafutilia mbali taasisi yetu. Hadi kipindi hicho Zitto hakuwa mwanachama wa CHADEMA lakini nikamshawishi na akajiunga na CHADEMA kisha tukagombea ubunge kama vijana mwaka 2005 ambapo mwenzangu alishinda lakini mimi niliibiwa kura na kesi kuzungushwa mahakamani kisha niliapa CCM wao ndio watakaohangaika mahakamani mwaka 2010 kwamba wameibiwa kura na ikawa hivyo(watu wanashangilia)." Mhe. Mnyika anasema, mwaka 2009 nilinasa mawasiliano kati ya Zitto na Mhariri mmoja wakilenga kukivuruga chama.

Kamanda Mnyika anasema waraka ule ulikuwa na mambo mengi machafu zaidi ya masuala ya uongozi. CCM kupitia mamluki wanataka kuwapandikiza viongozi wa juu ambao hawataitisha maandamano na kufanya mikutano ya kupigania haki za Watanzania.

"Wananchi mko tayari kwa hilooo..hapanaaa" Wananchi mnaounga mkono maamuzi ya chama wanyoshe mikono juu (umati mzima unanyosha mikono juu kuunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza wasaliti. Hatimaye Mhe.Mnyika anamaliza vile muda si rafiki na kudokeza kwamba amepokea waraka wa siri wa CCM wakiratibu kuhujumu uchaguzi wa serikali za mitaa.

Pia anasema wamepokea nyaraka za siri kutoka GGM pamoja na malalamiko ya watumishi wa idara ya afya Geita...CHADEMA itawatetea watanzania wote na kuiamuru serikali kutokusaini mikataba mipya na wawekezaji wanaowadhulumu wana Geita waishio kimasikini wakati kuna utajiri mkubwa hapa.

(Kamanda Mnyika amemaliza na umati unamshangilia kisha anamkaribisha Kamanda Said Issa Mohammed!

...UPDATES;

Kamanda Said Issa Mohammed anasema muda wa mkutano umeisha na wandishi wa habari ni mashahidi lakini mimi sifanyi mkutano bali naanza darasa na darasa halina mwisho hata kama ni saa nane usiku.

"Makamanda chama chenu kipo salama...(umati unapiga makofi).Wenye hila wanatafuta namna ya kuua chama lakini wameshindwa. CHADEMA si chama cha Wakristo wala Waislamu,si chama cha wachaga wala wapemba...! CHADEMA ina viongozi wa dini zote,kabila zote na kanda zote. Kamanda Mohammed anasema Quran inasema anayemwamini Mungu haachi kuwa mtiifu kwake hata kama Imamu aliyekuwa anampenda amefukuzwa msikini.

Kama kuna wanaCHADEMA waliokuwa watiifu wa Zitto na siyo CHADEMA, kama wanao ukweli mwingine zaidi ya usaliti uliotendeka basi waondoke nae (watu wanashangilia kwa nderemo na vifijo.

Hatimaye Kamanda Issa Mohammed amemaliza huku akiacha gumzo Geita kwa hoja zake nzito. Anauamsha umma kwa kusema CCM... Wananchi wanajibu kwishaaaa!
 
Kwa hisani ya Bwana Rogers J Ruhega, Kaimu Katibu wa Chadema Mkoa wa Geita

Wanachama wote wa Chadema na wote wapenda mabadiliko na uhuru wa kweli, wazalendo wote na wapenda maendeleo wa Geita, mnakaribishwa sana na mnaomba kuendelea kuwaalika wengine katika mkutano huo mkubwa sana wa kufungua mwaka utakaofanyika Geita mjini ndani ya kata ya kalangalala.

Mkutano huo utafuatiwa na kikao cha baraza la mashauriano la Chadema Mkoa wa Geita litakalokuwa na lengo kubwa la kutathimini shughuli ya ujenzi wa chama kupitia programe ya Chadema ni msingi ndani ya majimbo yote sita yaliyomo ndani ya Mkoa wa Geita.

Wadau; muda na eneo husika la wapi mkutano utakapofanyikia tutazidi kufahamishana jinsi siku zinavyozidi kukaribia, please stay tuned!

Mwaka 2014 ni mwaka wa maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya ukombozi mkuu wa uhuru wa mara pili 2051.

Hapo kwenye red,ulimaanisha hivyo?
 
endelea kutumika hapo wenzio wanapiga ruzuku wanaenda kununua majumba dubai huku wakivinjari na mahawara zake wee upo tu hapo
 
Hapo kwenye red,ulimaanisha hivyo?

Ni ypingg error ndugu yangu nilikuwa naamanisha 2015,

Mods naomba muundoe uzi huu ubaki ule niliorekebisha mwaka 2015 badala ya 2051.

Ahsante kwa ushirikiano.
 
Kwa hisani ya Bwana Rogers J Ruhega, Kaimu Katibu wa Chadema Mkoa wa Geita

Wanachama wote wa Chadema na wote wapenda mabadiliko na uhuru wa kweli, wazalendo wote na wapenda maendeleo wa Geita, mnakaribishwa sana na mnaomba kuendelea kuwaalika wengine katika mkutano huo mkubwa sana wa kufungua mwaka utakaofanyika Geita mjini ndani ya kata ya kalangalala.

Mkutano huo utafuatiwa na kikao cha baraza la mashauriano la Chadema Mkoa wa Geita litakalokuwa na lengo kubwa la kutathimini shughuli ya ujenzi wa chama kupitia programe ya Chadema ni msingi ndani ya majimbo yote sita yaliyomo ndani ya Mkoa wa Geita.

Wadau; muda na eneo husika la wapi mkutano utakapofanyikia tutazidi kufahamishana jinsi siku zinavyozidi kukaribia, please stay tuned!

Mwaka 2014 ni mwaka wa maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya ukombozi mkuu wa uhuru wa mara pili 2051.

Wewe Nyamigota nilishakwambia kwamba huwa unakurupuka sana,na ndiyo tabia yako miaka yote,na hata kwenye kazi unakurupuka tu!

Badilika vinginevyo itafika hata huo mwaka 2051 unaousema kwamba utakuwa ni wa uhuru na ukombozi bado msifanikiwe,wenzakomtunawaza uchaguzi wa mwakam2015 wewe unawaza 2051!!
 
Ni ypingg error ndugu yangu nilikuwa naamanisha 2015,

Mods naomba muundoe uzi huu ubaki ule niliorekebisha mwaka 2015 badala ya 2051.

Ahsante kwa ushirikiano.

Ni ypingg error kama ulivyoonesha hapo juu au Typing error?!

Dogo mboma unaweweseka?!

Jitahidi urudi pale katoro primary walau unaweza kujua unachokiandika,ingawa wanafunzi ni wengi na walimu ni wachache lakini waweza kutoka hapo ulipo na kusogea mbele kidogo!
 
Kwa hisani ya Bwana Rogers J Ruhega, Kaimu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Geita

Wanachama wote wa CHADEMA na wote wapenda mabadiliko na uhuru wa kweli, wazalendo wote na wapenda maendeleo wa Geita, mnakaribishwa sana na mnaomba kuendelea kuwaalika wengine katika mkutano huo mkubwa sana wa kufungua mwaka utakaofanyika Geita mjini ndani ya kata ya kalangalala.

Mkutano huo utafuatiwa na kikao cha baraza la mashauriano la CHADEMA Mkoa wa Geita litakalokuwa na lengo kubwa la kutathimini shughuli ya ujenzi wa chama kupitia programe ya CHADEMA ni msingi ndani ya majimbo yote sita yaliyomo ndani ya Mkoa wa Geita.

Wadau; muda na eneo husika la wapi mkutano utakapofanyikia tutazidi kufahamishana jinsi siku zinavyozidi kukaribia, please stay tuned!

Mwaka 2014 ni mwaka wa maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya ukombozi mkuu wa uhuru wa mara pili 2051.

karibu sana kamanda tupo pamoja
 
karibu sana Geita, hayo ndio mambo sasa.
 
Ni ypingg error kama ulivyoonesha hapo juu au Typing error?!

Dogo mboma unaweweseka?!

Jitahidi urudi pale katoro primary walau unaweza kujua unachokiandika,ingawa wanafunzi ni wengi na walimu ni wachache lakini waweza kutoka hapo ulipo na kusogea mbele kidogo!

huna lolote,elimu yako imekusaidia nn kama si kukufanya mtumwa wa buk7 tu!!!???
 
Mimi sio wewe unaetumiwa na mbowe na dk slaa pamoja BAVICHA!

Muulize huyo huyo Nyamigota atakwambia na yeye mwenyewe hajui hata kama nimemuajiri!
 
Good, we will always support you Mh Mbowe. Remember, 'mti wenye matunda ndo upigwa mawe".
 
Back
Top Bottom